Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1.
Kumekushughulisheni kutafuta wingi, 1

2Mpaka mje makaburini!

3. Sivyo hivyo! Mtakuja jua! 3

4. Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! 4

5.
Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
5

6. Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! 6

7.
Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
7

8. Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.
8
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani