Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. 1. Hatukukunjulia kifua chako? 1

2. Na tukakuondolea mzigo wako, 2

3. Ulio vunja mgongo wako? 3

4. Na tukakunyanyulia utajo wako? 4

5. Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
5

6. Hakika pamoja na uzito upo wepesi. 6

7. Na ukipata faragha, fanya juhudi. 7

8. Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie. 8
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani