Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA
MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. T'aa Siin Miim. (T'.S.M.) 1

2. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. 2

3. Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi
Waumini. 3

4. Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni
Ishara zikanyenyekea shingo zao. 4

5. Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman
ila wao hujitenga nao. 5

6. Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia
khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. 6

7. Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha
humo, ya kila namna nzuri? 7

8. Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao
hawakuwa wenye kuamini. 8

9. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu
Mwenye kurehemu. 9

10. Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia:
Fika kwa watu madhaalimu, 10

11. Watu wa Firauni. Hawaogopi? 11

12.
Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe.
12

13. Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu
haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun. 13

14. Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa
wasije kuniuwa. 14

15.
Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza
yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. 15

16. Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni
Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 16

17.
Waachilie Wana wa Israili wende nasi. 17

18.
(Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni,
na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? 18

19. Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa
miongoni mwa wasio na shukrani? 19

20.
(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa
miongoni mwa wale walio potea. 20

21.
(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa
miongoni mwa wale walio potea. 21

22. Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe
umewatia utumwani Wana wa Israili? 22

23.
Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa
walimwengu wote? 23

24.
Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na
viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini. 24

25. (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi?
25

26. (Musa) akasema: Ndiye Mola
wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza. 26

27. (Firauni) akasema: Hakika
huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. 27
1

28. (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na
Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini. 28

29. (Firauni) akasema:
Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga
gerezani. 29

30. Akasema: Je! Ijapo kuwa
nitakuletea kitu cha kubainisha wazi? 30

31. Akasema: Kilete basi, kama
wewe ni katika wasemao kweli. 31

32. Basi akaitupa fimbo yake,
mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri. 32

33. Na akautoa mkono wake, na
mara ukawa mweupe kwa watazamao. 33

34. (Firauni) akawaambia
waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu. 34

35. Anataka kukutoeni katika
nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani? 35

36. Wakasema: Mpe muda yeye na
nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo. 36

37. Wakuletee kila mchawi
bingwa mtaalamu. 37

38. Basi wakakusanywa wachawi
wakati na siku maalumu. 38

39. Na watu wakaambiwa: Je!
Mtakusanyika? 39

40. Huenda tutawafuata wachawi
wakiwa wao ndio watakao shinda. 40

41. Basi walipo kuja wachawi
wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda? 41

42. Naam! Na hakika mtakuwa
katika watu wa mbele. 42

43. Musa akwaambia: Tupeni
mnavyo taka kutupa. 43

44. Basi wakatupa kamba zao na
fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye
kushinda. 44

45. Musa tena akatupa fimbo
yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua. 45

46. Hapo wachawi walipinduka
wakasujudu. 46

47. Wakasema: Tunamuamini Mola
Mlezi wa walimwengu wote. 47

48. Mola Mlezi wa Musa na
Harun. 48

49. (Firauni) akasema: Je!
Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye
kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa
kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote. 49

50. Wakasema: Haidhuru, kwani
sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. 50

51. Hakika sisi tunatumai Mola
wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini. 51

52. Na tulimuamrisha Musa kwa
wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa. 52

53. Basi Firauni akawatuma
mijini wapiga mbiu za mgambo. 53

54. (Wakieneza): Hakika hawa ni
kikundi kidogo. 54

55. Nao wanatuudhi. 55

56. Na sisi ni wengi, wenye
kuchukua hadhari. 56

57. Basi tukawatoa katika
mabustani na chemchem, 57

58. Na makhazina, na vyeo vya
hishima, 58

59. Kadhaalika; na
tukawarithisha hayo Wana wa Israili. 59

60. Basi wakawafuata lilipo
chomoza jua. 60

61. Na yalipo onana majeshi
mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana!
61

62. (Musa) akasema: Hasha!
Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! 62

63. Tulimletea wahyi Musa
tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa
kama mlima mkubwa. 63

64. Na tukawajongeza hapo wale
wengine. 64

65. Tukawaokoa Musa na walio
kuwa pamoja naye wote. 65

66. Kisha tukawazamisha hao
wengine. 66

67. Hakika bila ya shaka katika
hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini. 67

68. Na kwa hakika Mola wako
Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 68

69. Na wasomee khabari za
Ibrahim. 69

70. Alipo mwambia baba yake na
kaumu yake: Mnaabudu nini? 70

71. Wakasema: Tunaabudu
masanamu, daima tunayanyenyekea. 71

72. Akasema: Je! Yanakusikieni
mnapo yaita? 72

73. Au yanakufaeni, au
yanakudhuruni? 73

74. Wakasema: Bali tumewakuta
baba zetu wakifanya hivyo hivyo. 74

75. Je! Mmewaona hawa mnao
waabudu- 75

76. Nyinyi na baba zenu wa
zamani?
76

77. Kwani hakika hao ni adui
zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 77

78. Ambaye ndiye aliye niumba,
na Yeye ndiye ananiongoa, 78

79. Na ambaye ndiye ananilisha
na kuninywesha. 79

80. Na ninapo ugua ni Yeye
ndiye anaye niponesha. 80

81. Na ambaye atanifisha, na
kisha atanihuisha. 81

82. Na ambaye ndiye ninaye
mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo. 82

83. Mola wangu Mlezi! Nitunukie
hukumu na uniunganishe na watendao mema. 83

84. Na unijaalie nitajwe kwa
wema na watu watakao kuja baadaye. 84

85. Na unijaalie katika warithi
wa Bustani za neema. 85

86. Na umsamehe baba yangu,
kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu. 86

87. Wala usinihizi Siku watapo
fufuliwa. 87

88. Siku ambayo kwamba mali
hayato faa kitu wala wana. 88

89. Isipo kuwa mwenye kumjia
Mwenyezi Mungu na moyo safi. 89

90. Na Pepo itasogezwa kwa
wachamngu. 90

91. Na Jahannamu itadhihirishwa
kwa wapotovu. 91

92. Na wataambiwa: Wako wapi
mlio kuwa mkiwaabudu 92

93. Badala ya Mwenyezi Mungu?
Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe? 93

94. Basi watavurumizwa humo wao
na hao wakosefu, 94

95. Na majeshi ya Ibilisi yote.
95

96. Watasema, na hali ya kuwa
wanazozana humo: 96

97. Wallahi! Kwa yakini
tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri, 97

98. Tulipo kufanyeni ni sawa na
Mola Mlezi wa walimwengu wote. 98

99. Tulipo kufanyeni ni sawa na
Mola Mlezi wa walimwengu wote. 99

100. Basi hatuna waombezi.
100

101. Wala rafiki wa dhati.
101

102. Laiti tungeli pata kurejea
tena tungeli kuwa katika Waumini. 102

103. Hakika katika haya ipo
Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. 103

104. Na hakika Mola wako Mlezi
ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 104

105. Kaumu ya Nuhu
waliwakadhibisha Mitume. 105

106. Alipo waambia ndugu yao,
Nuhu: Je! Hamchimngu? 106

107. Hakika mimi kwenu ni Mtume
muaminifu. 107

108. Basi Mcheni Mwenyezi
Mungu, na nit'iini mimi. 108

109. Na sikutakini juu yake
ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 109

110. Basi Mcheni Mwenyezi
Mungu, na nit'iini mimi. 110

111. Wakasema: Je! Tukuamini
wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini? 111

112. Akasema: Nayajuaje waliyo
kuwa wakiyafanya? 112

126. Hisabu yao haiko ila kwa
Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua! 113

114. Wala mimi si wa kuwafukuza
Waumini. 114

115. Mimi si cho chote ila ni
Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri. 115

116. Wakasema: Ikiwa huachi,
ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. 116

117. Akasema: Mola wangu Mlezi!
Hakika watu wangu wamenikanusha. 117

118. Basi hukumu baina yangu na
wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. 118

119. Kwa hivyo tukamwokoa yeye
na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. 119

120. Kisha tukawazamisha
baadaye walio bakia. 120

121. Na hakika Mola wako Mlezi
ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 121

122. Kina A'd waliwakanusha
Mitume. 122

123. Alipo waambia ndugu yao,
Hud: Je! Hamchimngu? 123

124. Hakika mimi kwenu ni Mtume
muaminifu. 124

125. Basi mcheni Mwenyezi
Mungu, na nit'iini mimi. 125

126. Wala sikutakeni juu yake
ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 126

127. Je! Mnajenga juu ya kila
mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi? 127

128. Na mnajenga majengo ya
fakhari kama kwamba mtaishi milele! 128

129. Na mnapo tumia nguvu
mnatumia nguvu kwa ujabari. 129

130. Na mnapo tumia nguvu
mnatumia nguvu kwa ujabari. 130

131. Basi mcheni Mwenyezi
Mungu, na nit'iini. 131

132. Na mcheni aliye kupeni
haya mnayo yajua. 132

133. Amekupeni wanyama wa
kufuga na wana. 133

134. Na mabustani na chemchem.
134

135. Hakika mimi ninakukhofieni
adhabu ya Siku Kubwa. 135

136. Wakasema: Ni mamoja kwetu,
ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha. 136

137. Haya si chochote ila ni
mtindo wa watu wa tokea zamani. 137

138. Wala sisi hatutaadhibiwa.
138

139. Wakamkanusha; nasi
tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa
wengi wao wenye kuamini. 139

140. Na hakika Mola wako Mlezi
ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 140

141. Kina Thamud waliwakanusha
Mitume. 141

142. Alipo waambia ndugu yao
Saleh: Je! Hamumchimngu? 142

143. Hakika mimi kwenu ni Mtume
muaminifu. 143

144. Basi mcheni Mwenyezi
Mungu, na nit'iini. 144

145. Wala sikutakini ujira juu
yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 145

146. Je! Mtaachwa salama
usalimina katika haya yaliyopo hapa? 146

147. Katika mabustani, na
chemchem? 147

148. Na konde na mitende yenye
makole yaliyo wiva. 148

149. Na mnachonga milimani
majumba kwa ustadi. 149

150. Basi mcheni Mwenyezi
Mungu, na nit'iini mimi. 150

151. Wala msit'ii amri za walio
pindukia mipaka, 151

152. Ambao wanafanya ufisadi
katika nchi, wala hawatengenezi. 152

153. Wakasema: Hakika wewe ni
miongoni mwa walio rogwa. 153

154. Wewe si chochote ila ni
mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
154

155. Akasema: Huyu ngamia jike;
awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku
maalumu. 155

156. Wala msimguse kwa uwovu,
isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa. 156

157. Lakini wakamuuwa, na
wakawa wenye kujuta. 157

158. Basi ikawapata adhabu.
Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. 158

159. Na hakika Mola wako Mlezi
ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 159

160. Watu wa Lut'i
waliwakanusha Mitume. 160

161. Alipo waambia ndugu yao,
Lut'i: Je! Hamumchimngu? 161

162. Hakika mimi kwenu ni Mtume
muaminifu kwenu. 162

163. Basi mcheni Mwenyezi Mungu
na nit'iini mimi. 163

164. Wala mimi sikutakini ujira
juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 164

165. Je! Katika viumbe vyote
mnawaingilia wanaume? 165

166. Na mnaacha alicho
kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka
mipaka! 166

167. Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo
acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji! 167

168. Akasema: Hakika mimi ni
katika wanao kichukia hichi kitendo chenu. 168

169. Mola wangu Mlezi! Niokoe
mimi na ahali zangu na haya wayatendayo. 169

170. Basi tukamwokoa yeye na
ahali zake wote, 170

171. Isipo kuwa kikongwe katika
walio kaa nyuma. 171

172. Kisha tukawaangamiza wale
wengine. 172

173. Na tukawanyeshea mvua,
basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa. 173

174. Hakika katika hayo ipo
Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini. 174

175. Na hakika Mola wako Mlezi
bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 175

176. Watu wa Machakani
waliwakanusha Mitume. 176

177. Shuaibu alipo waambia: Je!
Hamfanyi mkamchamngu? 177

178. Hakika mimi kwenu ni Mtume
muaminifu. 178

179. Basi mcheni Mwenyezi
Mungu, na nit'iini mimi. 179

180. Wala sikutakini ujira juu
yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 180

181. Timizeni kipimo sawa sawa,
wala msiwe katika wanao punja. 181

182. Na pimeni kwa haki iliyo
nyooka; 182

183. Wala msiwapunje watu vitu
vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi. 183

184. Na mcheni aliye kuumbeni
nyinyi na vizazi vilivyo tangulia. 184

185. Wakasema: Hakika wewe ni
katika walio rogwa. 185

186. Na wewe si chochote ila ni
mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo. 186

187. Hebu tuangushie vipande
kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. 187

188. Akasema: Mola wangu Mlezi
anajua zaidi mnayo yatenda. 188

189. Basi walimkanusha, na
ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa.
189

190. Hakika katika hayo ipo
Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. 190

191. Na hakika Mola wako Mlezi
bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 191

192. Na bila ya shaka hii ni
Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. 192

193. Ameuteremsha Roho
muaminifu, 193

194. Juu ya moyo wako, ili uwe
katika Waonyaji, 194

195. Kwa ulimi wa Kiarabu ulio
wazi. 195

196. Na hakika bila ya shaka
haya yamo katika Vitabu vya kale. 196

197. Je! Haikuwa kwao ni Ishara
kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili? 197

198. Na lau kuwa tungeli
iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, 198

199. Na akawasomea, wasingeli
kuwa wenye kuamini. 1990

200. Namna hivi tunaingiza
katika nyoyo za wakosefu. 200

201. Hawataiamini mpaka waione
adhabu chungu. 201

202. Basi itawafikia kwa
ghafla, na hali hawana khabari. 202

203. Na watasema: Je, tutapewa
muhula? 203

204. Basi, je, wanaihimiza
adhabu yetu? 204

205. Waonaje kama
tukiwastarehesha kwa miaka, 205

206. Kisha yakawafikia waliyo
kuwa wakiahidiwa, 206

207. Yatawafaa nini yale waliyo
stareheshewa? 207

208. Wala hatukuangamiza mji wo
wote ila ulikuwa na waonyaji 208

209. Kuwa ni ukumbusho. Wala
Sisi hatukuwa wenye kudhulumu. 209

210. Wala Mashet'ani
hawakuteremka nayo, 10

211. Wala haitakiwi kwao, na
wala hawawezi. 11

212. Hakika hao wametengwa na
kusikia. 12

213. Basi usimwombe mungu
mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa. 13

214. Na uwaonye jamaa zako
walio karibu nawe. 14

215. Na watwae kwa upole wanao
kufuata miongoni mwa Waumini. 15

216. Na ikiwa watakuasi basi
sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda. 16

217. Na umtegemee Mtukufu
Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 17

218. Ambaye anakuona unapo
simama, 18

219. Na mageuko yako kati ya
wanao sujudu. 19

220. Hakika Yeye ndiye Mwenye
kusikia Mwenye kujua. 20

221. Je! Nikwambieni nani
wanawashukia Mashet'ani? 21

222. Wanamshukia kila mzushi
mkubwa mwingi wa dhambi. 22

223. Wanawapelekea yale wanayo
yasikia; na wengi wao ni waongo. 23

224. Na watungaji mashairi ni
wapotofu ndio wanawafuata. 24

225. Je! Huwaoni kwamba wao
wanatangatanga katika kila bonde? 25

226. Na kwamba wao husema
wasiyo yatenda? 26

227. Isipo kuwa wale walio
amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na
wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao
geuka. 27
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una
ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright © 22
August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani