Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Alif Lam Mim 1

2. Warumi wameshindwa, 1

3. Katika nchi iliyo karibu. Nao
baada ya kushindwa kwao watashinda 3

4. Katika miaka michache. Amri ni
ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. 4

5. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu
humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. 5

6. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi hawajui. 6

7. Wanajua hali ya dhaahiri ya
maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera. 7

8. Je! Hawajifikirii nafsi zao?
Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake ila kwa Haki na
kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa
watakutana na Mola wao Mlezi. 8

9. Je! Hawatembei katika ardhi
wakaona ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi
kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyo istawisha
wao. Na Mitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu
ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao. 9

10. Kisha ulikuwa mwisho wa walio fanya ubaya ni
kuzikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawa wanazifanyia maskhara. 10

11. Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha
mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake. 11

12. Na itapo simama Saa wakosefu watakata tamaa. 12

13. Wala hawatakuwa na waombezi miongoni mwa walio kuwa
wakiwashirikisha na Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao. 13

14. Na siku itapo simama Saa, siku hiyo watagawanyika. 14

15. Ama walio amini na wakatenda mema watafurahishwa
katika Bustani. 15

16. Na ama walio kufuru na wakazikanusha Ishara zetu na
mkutano wa Akhera, hao basi watahudhurishwa katika adhabu. 16

17. Basi Subhanallah! Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni na
asubuhi, 17

18. Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na
alasiri na adhuhuri. 18

19. Hukitoa kilicho hai kutokana na kilicho kufa, na
hukitoa kilicho kufa kutokana na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa
kwake. Na kama hivyo ndivyo mtavyo fufuliwa. 19

20. Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kwa udongo.
Kisha mmekuwa watu mlio tawanyika kote kote. 20

21. Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu
kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma
baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri. 21

22. Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na
kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa
wajuzi. 22

23. Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na
mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo
Ishara kwa watu wanao sikia. 23

24. Na katika Ishara zake hukuonyesheni umeme kwa
kukutieni khofu na tamaa. Na hukuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo
huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu
wanao zingatia. 24

25. Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi
zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapo kuiteni mwito mmoja tu, hapo mtatoka
kwenye ardhi. 25

26. Na vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote
vinamt'ii Yeye. 26

27. Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha
ataurudisha mara nyengine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye
mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye
hikima. 27

28.
Amekupigieni mfano kutokana na nafsi zenu. Je! Katika
hao iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyo
kuruzukuni, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyo
ogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivi tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye
akili. 28

29. Bali walio dhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao
pasina kujua. Basi nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha apotee? Wala
hao hawatakuwa na wa kuwanusuru. 29

30. Bali walio dhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao
pasina kujua. Basi nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha apotee? Wala
hao hawatakuwa na wa kuwanusuru. 30

31. Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na shikeni
Sala, na wala msiwe katika washirikina. 31

32. Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na
wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho. 32

33.
Yakiwapata watu madhara humwomba Mola wao Mlezi nao
wametubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi miongoni
mwao humshirikisha Mola wao Mlezi, 33

34. Kwa kuyakataa tuliyo wapa. Basi stareheni. Mtakuja
jua! 34

35. Au tumewateremshia hoja ambayo kwayo ndio wanafanya
ushirikina? 35

36. Na watu tunapo waonjesha rehema huifurahia, na
ukiwasibu uovu kwa iliyo yatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa. 36

37. Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia
riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye? Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu
wanao amini. 37

38. Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri.
Hayo ni kheri kwa watakao radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa.
38

39. Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha
akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika
hao mnao washirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye
ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo mshirikisha naye. 39

40. Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha
akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika
hao mnao washirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye
ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo mshirikisha naye. 40

41. Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya
mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda
wakarejea kwa kutubu. 41

42. Sema: Safirini duniani muangalie ulikuwaje mwisho wa
walio tangulia. Wengi wao walikuwa washirikina. 42

43. Basi uelekeze uso wako kwenye Dini Iliyo Nyooka kabla
ya kufika Siku hiyo isiyo zuilika, inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu
watatengana. 43

44. Anaye kufuru basi ukafiri wake utakuwa juu yake
mwenyewe, na anaye tenda mema, basi wanazitengezea nafsi zao. 44

45. Ili awalipe walio amini na wakatenda mema kutokana na
fadhila yake. Hakika Yeye hawapendi makafiri. 45

46. Na katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo
bishara njema, na ili kukuonjesheni baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yende
kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru. 46

47. Na hakika tulikwisha watuma Mitume kwa kaumu zao, na
wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale walio fanya ukosefu. Na
ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini. 47

48. Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma pepo zikayatimua
mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande
mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapo wafikishia awatakao katika
waja wake, mara hao huwa na furaha. 48

49. Na ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata
tamaa. 49

50. Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu,
jinsi anavyo ihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo ndiye bila ya
shaka Mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu. 50

51. Na tunge utuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya
manjano, juu ya hayo wange endelea kukufuru. 51

52. Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala
viziwi wakasikia wito wakisha geuka kukupa mgongo. 52

53. Wala wewe huwaongoi vipofu na upotovu wao.
Huwasikilizishi ila wanao ziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walio nyenyekea. 53

54. Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na
udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu
unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza. 54

55. Na siku itapo simama Saa wakosefu wataapa kwamba
hawakukaa duniani ila saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyo kuwa wakipotozwa. 55

56. Na walio pewa ilimu na Imani watasema: Hakika nyinyi
mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii
ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui. 56

57. Basi Siku hiyo hautawafaa walio dhulumu udhuru wao,
wala haitotakiwa toba yao. 57

58. Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika
hii Qur'ani. Na ukiwaletea Ishara yoyote hapana shaka walio kufuru watasema:
Nyinyi si chochote ila ni waongo. 58

59. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga muhuri kwenye
nyoyo za wasio jua. 59

60. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya
haki. Wala wasikupaparishe hao wasio kuwa na yakini. 60
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma
hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al
Barwani