Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA
MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1.
Arrah'man, Mwingi wa
Rehema 1

2.
Amefundisha Qur'ani. 2

3. Amemuumba mwanaadamu, 3

4.
Akamfundisha kubaini. 4

5. Jua na mwezi huenda kwa hisabu. 5

6. Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
6

7. Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani, 7

8. Ili msidhulumu katika mizani. 8

9. Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika
mizani. 9

10. Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. 10

11. Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
11

12. Na nafaka zenye makapi, na rehani. 12

13. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha 13

14.
Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo. 14

15. Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto. 15

16. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha. 16

17. Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi
mbili. 17

18. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 18

19.
Anaziendesha bahari mbili zikutane; 19

20. Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane. 20

21. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 21

22. Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
22

23. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 23

24. Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo
undwa kama vilima. 24

25. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 25

26. Kila kilioko juu yake kitatoweka. 26

27. Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu
na ukarimu. 27

28. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 28

29.
Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi.
Kila siku Yeye yumo katika mambo. 29

30. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 30

31.
Tutakuhisabuni enyi makundi mawili. 31

32. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 32

33. Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya
kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
33

34. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 34

35.
Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala
hamtashinda. 35

36. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 36

37.
Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
37

38. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 38

39. Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
39

40. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 40

41.
Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi
watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. 41

42. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 42

43. Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
43

44.
Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto
yanayo chemka. 44

45. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 45

46. Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake
Mlezi atapata Bustani mbili. 46

47. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 47

48.
Bustani zenye matawi yaliyo tanda. 48

49. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 49

50. Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
50

51. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 51

52. Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
52

53. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 53

54. Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri
nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu. 54

55. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 55

56. Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao;
hajawagusa mtu kabla yao wala jini. 56

57. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 57

58. Kama kwamba wao ni yakuti na marijani. 58

59. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha. 59

60. Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
60

61. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 61

62. Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
62

63. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 63

64. Za kijani kibivu. 64

65. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 65

66. Na chemchem mbili zinazo furika. 66

67. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 67

68. Imo humo miti ya matunda, na mitende na
mikomamanga. 68

69. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 69

70. Humo wamo wanawake wema wazuri. 70

71. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 71

72.
Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
72

73. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 73

74.
Hajawagusa mtu wala jini kabla yao. 74

75. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 75

76.
Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia
mazuri. 76

77. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha? 77

78.
Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu
na ukarimu. 78
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani