Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA
MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. WANAULIZANA nini? 1

2. Ile khabari kuu, 2

3. Ambayo kwayo wanakhitalifiana. 3

4. La! Karibu watakuja jua. 4

5. Tena la! Karibu watakuja jua. 5

6. kaKwani hatukuifanya ardhi ma tandiko? 6

7. kama Na milima vigingi? 7

8. Na tukakuumbeni kwa jozi? 8

9. Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? 9

10. Na tukaufanya usiku ni nguo? 10

11. Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
11

12. Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? 12

13. Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; 13

14. Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka
mawinguni, 14

15. Ili tutoe kwayo nafaka na mimea. 15

16.Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. 16

17. Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,
17

18. Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa
makundi, 18

19. Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango. 19

20. Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
20

21. Hakika Jahannamu inangojea! 21

22. Kwa walio asi ndio makaazi yao, 1

23. Wakae humo karne baada ya karne, 23

24.
Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,
24

25. Ila maji yamoto sana na usaha, 25

26. Ndio jaza muwafaka. 26

27. Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.
27

28. Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. 28

29. Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
29

30. Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
30

31. Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, 31

32. Mabustani na mizabibu, 32

33. Na wake walio lingana nao, 33

34. Na bilauri zilizo jaa, 34

35.
Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo, 35

36. Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha
kutosha. 36

37. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao,
Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! 37

38. Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu.
Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.
38

39. Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike
njia arejee kwa Mola wake Mlezi 39

40. Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu
kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri
atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! 40
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani