Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
1

2. Na itakapo toa ardhi mizigo yake! 2

3. Na mtu akasema: Ina nini? 3

4. Siku hiyo itahadithia khabari zake. 4

5. Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!

6. Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe
vitendo vyao! 6

7. Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! 7

8. Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! 8
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani