Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA
MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! 1

2. Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu
uchawi tu unazidi kuendelea. 1

3. Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila
jambo ni lenye kuthibiti. 3

4. Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
4

5. Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu! 5

6. Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea
jambo linalo chusha; 6

7. Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige
walio tawanyika, 7

8.
Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni
siku ngumu. 8

9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja
wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa. 9

10. Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika
mimi nimeshindwa, basi ninusuru! 10

11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo
miminika. 11

12. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji
kwa jambo lilio kadiriwa. 12

13. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
13

14. Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa
alivyo kuwa amekanushwa. 14

15. Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je,
yupo anaye kumbuka? 15

16. Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
16

17. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi
kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka? 17

18. Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu
na maonyo yangu? 18

19. Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika
siku korofi mfululizo, 19

20.
Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio
ng'olewa. 20

21. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
21

22. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi
kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka? 22

23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji. 23

24.
Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi?
Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa! 24

25. Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu
sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi! 25

26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
26

27. Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili
kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili. 27

28. Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila
sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika. 28

29. Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja. 29

30. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
30

31. Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa
kama mabuwa ya kujengea uwa. 31

32. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi
kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye? 32

33. Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji. 33

34. Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo
kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri. 34

35. Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo
anaye shukuru. 35

36. Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao
waliyatilia shaka hayo maonyo. 36

37. Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho
yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu! 37

38. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya
kuendelea. 38

39. Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!< 39

40. Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini
yupo anaye kumbuka? 40

41. Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni. 41

42.
Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika
kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza. 42

43. Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa
vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani? 43

44. Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
44

45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
45

46. Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni
nzito zaidi na chungu zaidi. 46

47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
47

48. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe:
Onjeni mguso wa Jahannamu! 48

49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
49

50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa
jicho. 50

51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu.
Lakini yupo anaye kumbuka? 51

52. Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
52

53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa. 53

54. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
54

55. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.
55
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani