Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo,
1

2. Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.
2

3. Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.
3

4. Na hakika wewe una tabia tukufu. 4

5. Karibu utaona, na wao wataona, 5

6. Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu. 6

7. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani
aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. 7

8. Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. 8

9. Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.
9

10. Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa,
10

11.
Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.
11

12. Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi,
12

13. Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu.
13

14. Ati kwa kuwa ana mali na watoto! 14

15. Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za
uwongo za watu wa zamani! 15

16.
Tutamtia kovu juu ya pua yake. 16

17. Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale
wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi.
17

18. Wala hawakusema: Mungu akipenda! 18

19. Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako
Mlezi, nao wamelala! 19

20. Likawa kama usiku wa giza. 20

21. Asubuhi wakaitana. 21

22. Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka
kuvuna. 22

23. Basi walikwenda na huku wakinong'onezana, 23

24. Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni.
24

25. Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio
hilo. 25

26. Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea!
26

27. Bali tumenyimwa! 27

28. Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini
hamumtakasi Mwenyezi Mungu? 28

29.
Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi
tulikuwa wenye kudhulumu. 29

30. Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.
30

31.
Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!
31

32. Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora
kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. 32

33. Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso
ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua! 33

34. Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa
Mola wao Mlezi. 34

35. Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? 35

36. Mna nini? Mnahukumu vipi? 36

37. Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?
37

38. Kuwa mtapata humo mnayo yapenda? 38

39. Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya
Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia? 39

40.
Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya?
40

41. Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao
wakiwa wanasema kweli. 41

42. Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa
kusujudu, lakini hawataweza, 42

43. Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na
hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima 43

44. Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya!
Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. 44

45. Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni
imara. 45

46. Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama
hiyo? 46

47. Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? 47

48. Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe
kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. 48

49. Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake
Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. 49

50. Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya
miongoni mwa watu wema. 50

51. Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho
yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. 51

52. Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu
wote. 52
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani