Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul
Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. 1

2. Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?
2

3. Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. 3

4. Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa
idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. 4

5. Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
5
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani