Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Inayo gonga! 1

2. Nini Inayo gonga? 2

3. Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
3

4. Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio
tawanyika; 4

5. Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
5

6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
6

7. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. 7

8. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
8

9. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! 9

10. Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? 10

11. Ni Moto mkali! 11
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani