Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Ole wao hao wapunjao! 1

2.
Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
2

3. Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani
hupunguza. 3

4.
Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa 4

5.
Katika Siku iliyo kuu, 5

6. Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu
wote? 6

7.
Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka
yamo katika Sijjin. 7

8.
Unajua nini Sijjin? 8

9.
Kitabu kilicho andikwa. 9

10.
Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! 10

11.
Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. 11

12.
Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka,
mwenye dhambi. 12

13.
Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa
kale! 13

14.
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio
kuwa wakiyachuma. 14

15.
Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka
watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. 15

16.
Kisha wataingia Motoni! 16

17.
Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa
mkiyakadhabisha. 17

18.
Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka
yamo katika I'liyyin. 18

19.
Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? 19

20.
Kitabu kilicho andikwa. 20

21.
Wanakishuhudia walio karibishwa. 21

22.
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika
neema. 22

23.
Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. 23

24.
Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
24

25.
Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
25

26.
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie
wenye kushindana. 26

27.
Na mchanganyiko wake ni Tasniim, 27

28.
Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. 28

29.
Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa
wakiwacheka walio amini. 29

30 Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. 30

31.
Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
31

32.
Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa
walio potea. 32

33.
Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. 33

34.
Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
34

35.
Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
35

36.
Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa
wakiyatenda? 36
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii
qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al
Barwani