Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

74.Surat Al-Muddaththir


image
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

image
1.Ewe uliye jigubika!
1

image
2.Simama uonye!
2

image
3.Na Mola wako Mlezi mtukuze!
3

image
4.Na nguo zako, zisafishe.
4

image
5.Na yaliyo machafu yahame!
5

image
6.Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.
6

image
7.Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!
7

image
8.Basi litapo pulizwa barugumu,
8

image
9.Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.
9

image
10.Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.
10

image
11.Niache peke yangu na niliye muumba;
11

image
12.Na nikamjaalia awe na mali mengi,
12

image
13. Na wana wanao onekana,
13

image
14.Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa.
14

image
15.Kisha anatumai nimzidishie!
15

image
16.Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!
16

image
17.Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana.
17

image
18.Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.
18

image
19.Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!
19

image
20.Tena ameangamia! Vipi alivyo pima!
20

image
21.Kisha akatazama,
21

image
22.Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
22

image
23.Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
23

image
24. Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa.
24

image
25.Haya si chochote ila kauli ya binaadamu.
25

image
26.Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
26

image
27.Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?
27

image
28.Haubakishi wala hausazi.
28

image
29.Unababua ngozi iwe nyeusi.
29

image
30.Juu yake wapo kumi na tisa.
30


Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright � 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani