Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA
MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea,
1

2. Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia
2

3. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.
3

4. Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku
ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! 4

5. Basi subiri kwa subira njema.Hakika wao wanaiona iko
mbali, 5

6. Hakika wao wanaiona iko mbali, 6

7. Na Sisi tunaiona iko karibu. 7

8. Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo
yayushwa. 8

9. Na milima itakuwa kama sufi. 9

10. Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. 10

11. Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu
lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, 11

12. Na mkewe, na nduguye, 12

13. Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, 13

14. Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
14

15. La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa,
15

16. Unao babua ngozi ya kichwa! 16

17.
Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka.
17

18. Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. 18

19. Hakika mtu ameumbwa na papara. 19

20. Inapo mgusa shari hupapatika. 20

21. Na inapo mgusa kheri huizuilia. 21

22. Isipo kuwa wanao sali, 22

23. Ambao wanadumisha Sala zao, 23

24. Na ambao katika mali yao iko haki maalumu 24

25. Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba;
25

26. Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, 26

27. Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao
Mlezi. 27

28. Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika
nayo. 28

29. Na ambao wanahifadhi tupu zao. 29

30. Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono
yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi 30

31. Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio
wanao ruka mipaka. 31

32. Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,
32

33. Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,
33

34. Na ambao wanazihifadhi Sala zao. 34

35. Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. 35

36. Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho
tu? 36

37.
Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa
kushoto! 37

38. Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo
ya neema? 38

39. La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na
wanacho kijua. 39

40. Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na
magharibi zote kwamba Sisi tunaweza 40

41.
Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi
hatushindwi. 41

42. Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka
wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, 42

43. Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba
wanakimbilia mfundo, 43

44. Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo
ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. 44
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani