Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama
ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa. 1

2. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama
ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa. 2

3. Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye
kushukuru, au mwenye kukufuru. 3

4. kika HaSisi tumewaandalia makafiri minyororo na
pingu na Moto mkali. 4

5. Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo
changanyika na kafuri, 5

6. Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu,
wakiifanya imiminike kwa wingi. 6

7. Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari
yake inaenea sana, 7

8. Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake,
masikini, na yatima, na wafungwa. 8

9. Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi
Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. 9

10. Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo
siku yenye shida na taabu. 10

11. Basi Mwenyna raha na furahaezi Mungu atawalinda na
shari ya siku hiyo, na atawakutanisha. 11

12. Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri
kwa vile walivyo subiri. 12

13 Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo
jua kali wala baridi kali. 13

14 Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya
matunda yataning'inia mpaka chini. 14

15 Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya
vigae, 15

16 Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.
16

17 Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na
tangawizi. 17

18 Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.
18

19 Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka,
ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa. 19

20 Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme
mkubwa. 20

21 Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi,
na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi
atawanywesha kinywaji safi kabisa. 21

22 Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu
zimekubaliwa. 22

23 Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo.
23

24 Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii
miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru. 24

25 Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na
jioni; 25

26 Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati
mrefu. 26

27 Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na
wanaiacha nyuma yao siku nzito. 27

28 Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na
tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao. 28

29 Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika
Njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi. 29

30 Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ilimu, Mwenye hikima. 30

31
Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye
kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu. 31
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani