Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Mbingu itapo chanika, 1

2. Na nyota zitapo tawanyika, 2

3. Na bahari zitakapo pasuliwa, 3

4. Na makaburi yatapo fukuliwa, 4

5. Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho
bakisha nyuma. 5

6. Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola
wako Mlezi Mtukufu? 6

7. Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
7

8. Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
8

9. Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
9

10. Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
10

11.
Waandishi wenye hishima, 11

12.
Wanayajua mnayo yatenda. 12

13.
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
13

14. Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
14

15.
Wataingia humo Siku ya Malipo. 15

16. Na hawatoacha kuwamo humo. 16

17. Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku
gani? 17

18. Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni
siku gani? 18

19. Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu
ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. 19
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani