Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Je! Imekufikia khabari ya msiba wa
kufudikiza?
1

2. Siku hiyo nyuso zitainama, 2

3.
Zikifanya kazi, nazo taabani. 3

4.
Ziingie katika Moto unao waka 4

5.
Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka. 5

6.
Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye
miba. 6

7.
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. 7

8. Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. 8

9.
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao, 9

10.
Katika Bustani ya juu. 10

11.
Hawatasikia humo upuuzi.Humo imo chemchem inayo
miminika. 11

12.
Humo imo chemchem inayo miminika. 12

13.
Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa, 13

14. Na bilauri zilizo pangwa, 14

15. Na matakia safu safu, 15

16. Na mazulia yaliyo tandikwa. 16

17.
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
17

18. Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? 18

19. Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? 19

20. Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? 20

21.
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
21

22.
Wewe si mwenye kuwatawalia. 22

23.
Lakini anaye rudi nyuma na kukataa, 23

24.Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa
kabisa24

25. Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. 25

26. Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao! 26
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu
ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii
qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani