Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

1. KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

2. Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa
viumbe vyote;

3. Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;

4. Mwenye kumiliki siku ya malipo.

5. Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada.

6. Tuongoe njia iliyonyooka.

7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa,
wala walio potea.
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa una
ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani