Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA
MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Naapa kwa mbingu yenye
Buruji! 1

2. Na kwa siku iliyo ahidiwa! 2

3. Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa! 3

4.
Wameangamizwa watu wa makhandaki 4

5. Yenye moto wenye kuni nyingi, 5

6. Walipo kuwa wamekaa hapo, 6

7. Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia
Waumini. 7

8. Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini
Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa, 8

9. Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi
Mungu ni shaahidi wa kila kitu. 9

10. Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini
wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu
ya kuungua. 10

11. Hakika walio amini na wakatenda mema watapata
Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. 11

12. Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
12

13. Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza
tena, 13

14. Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi, 14

15. Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu, 15

16.
Atendaye ayatakayo. 16

17. Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi? 17

18. Ya Firauni na Thamudi? 18

19. Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha.
19

20. Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. 20

21. Bali hii ni Qur'ani tukufu 21

22. Katika Ubao Ulio Hifadhiwa. 22
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani