Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1.
Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na
washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana, 1

2. Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye
wasomea kurasa zilizo takasika, 2

3. Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka. 3

4. Wala hawakufarikiana walio pewa Kitabu ila baada ya
kuwajia hiyo bayana. 4

5. Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu
kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo
ndiyo Dini madhubuti. 5

6. Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na
washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio
viumbe waovu kabisa. 6

7. Hakika walio amini na wakatenda mema, hao ndio bora
wa viumbe. 7

8. Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima,
zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao
waradhi naye. Hayo ni kwa anaye mwogopa Mola wake Mlezi. 8
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani