Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1. Naapa kwa Mji huu! 1

2.Nawe unaukaa Mji huu. 2

3. Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. 3

4. Hakika tumemuumba mtu katika taabu. 4

5. Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? 5

6. Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. 6

7. Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
7

8. Kwani hatukumpa macho mawili? 8

9. Na ulimi, na midomo miwili? 9

10. Na tukambainishia zote njia mbili? 10

11. Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya
milimani. 11

12. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya
milimani? 12

13.
Kumkomboa mtumwa; 13

14. Au kumlisha siku ya njaa 14

15. Yatima aliye jamaa, 15

16. Au masikini aliye vumbini. 16

17. Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana
kusubiri na wakausiana kuhurumiana. 17

18. Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. 18

19. Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa
shari wa kushotoni. 19

20. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.
20
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani