Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA
LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

1.
Naapa kwa pepo zinazo tawanya, 1

2. Na zinazo beba mizigo, 1

3. Na zinazo kwenda kwa wepesi. 3

4. Na zinazo gawanya kwa amri, 4

5.
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli,
5

6. Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
6

7.
Naapa kwa mbingu zenye njia, 7

8.
Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo
khitalifiana. 8

9.
Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. 9

10.
Wazushi wameangamizwa. 10

11.
Ambao wameghafilika katika ujinga. 11

12.
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? 12

13.
Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. 13

14.
Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa
mkiyahimiza. 14

15.
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na
chemchem. 15

16.
Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao
walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. 16

17.
Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. 17

18.
Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. 18

19.
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na
asiye omba. 19

20.
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
20

21.
Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? 21

22.
Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.
22

23.
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika
haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. 23

24.
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao
hishimiwa? 24

25.
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye
akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. 25

26.
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.
26

27.
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? 27

28.
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe
na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. 28

29.
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na
akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! 29

30.
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako
Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. 30

31.
AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa?
31

32.
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,
32

33.
Tuwatupie mawe ya udongo, 33

34.
Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa
ajili ya wanao pindukia mipaka. 34

35.
Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.
35

36.
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye
Waislamu! 36

37.
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa
adhabu chungu. 37

38.
Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni
na hoja wazi. 38

39.
Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema:
Huyu ni mchawi au mwendawazimu! 39

40.
Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa
baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. 40

41.
Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa
kukata uzazi. 41

42.
Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya
kama kilio nyambuka. 42

43.
Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa:
Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. 43

44.
Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua
moto wa radi nao wanaona. 44

45.
Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye
kujitetea. 45

46.
Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa
watu wapotovu. 46

47.
Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika
Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. 47

48.
Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna
gani Sisi! 48

49.
Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
49

50.
Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni
mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. 50

51.
Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na
Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
51

52.
Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila
walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. 52

53.
Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
53

54.
Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. 54

55.
Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
55

56.
Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu
Mimi. 56

57.
Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.Hakika
Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. 57

58.
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye
nguvu, Madhubuti. 58

59.
Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama
fungu la wenzao. Basi wasinihimize. 59

60.
Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa.
60
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa una
ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani