Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

80.Surat A'basa


image
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

image
1. Alikunja kipaji na akageuka,
1

image
2. Kwa sababu alimjia kipofu!
2

image
3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
3

image
4. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
4

image
5. Ama ajionaye hana haja,
5

image
6. Wewe ndio unamshughulikia?
6

image
7. . Na si juu yako kama hakutakasika.
7

image
8. Ama anaye kujia kwa juhudi
8

image
9. Naye anaogopa,
9

image
10. Ndio wewe unampuuza?
10

image
11. Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
11

image
12. . Basi anaye penda akumbuke.
12

image
13. Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
13

image
14. Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
14

image
15. Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
15

image
16. Watukufu, wema.
16

image
17. Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
17

image
18. Kwa kitu gani amemuumba?
18

image
19. Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
19

image
20. Kisha akamsahilishia njia.
20

image
21. Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
21

image
22. Kisha apendapo atamfufua.
22

image
23. La! Hajamaliza aliyo muamuru.
23

image
24. . Hebu mtu na atazame chakula chake.
24

image
25. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
25

image
26. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
26

image
27. Kisha tukaotesha humo nafaka,
27

image
28. Na zabibu, na mimea ya majani,
28

image
29. Na mizaituni, na mitende,
29

image
30. Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
30

image
31. Na matunda, na malisho ya wanyama;
31

image
32. Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
32

image
33. Basi utakapo kuja ukelele,
33

image
34. Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
34

image
35. Na mamaye na babaye,
35

image
36. Na mkewe na wanawe
36

image
37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha
37

image
38. Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
38

image
39. Zitacheka, zitachangamka;
39

image
40. Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
40

image
41. Giza totoro litazifunika,
41

image
42. Hao ndio makafiri watenda maovu
42


Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright � 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani