Tarjuma ya Quran Tukufu kwa
kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1.Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! 1

2.Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! 2

3.Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
3

4.Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za
vidole vyake! 4

5.Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku
zilioko mbele yake. 5

6.Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? 6

7. Basi jicho litapo dawaa, 7

8.Na mwezi utapo patwa, 8

9.Na likakusanywa jua na mwezi, 9

10.Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
10

11.La! Hapana pa kukimbilia! 11

12.Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
12

13.Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo
yaakhirisha. 13

14. Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. 14

15.Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. 15

16. Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia
haraka. 16

17.Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
17

18. Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
18

19.Kisha ni juu yetu kuubainisha. 19

20.Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
20

21.Na mnaacha maisha ya Akhera. 21

22. Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, 22

23.Zinamwangallia Mola wao Mlezi. 23

24.Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. 24

25.Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa
mgongo. 25

26.La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya
koo, 26

27. Na pakasemwa: Nani wa kumganga? 27

28. Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko
kufariki; 28

29.Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, 29

30.Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako
Mlezi! 30

31.Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali. 31

32.Bali alikanusha, na akageuka. 32

33.Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. 33

34.Ole wako, ole wako! 34

35.Kisha Ole wako, ole wako! 35

36. Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
36

37.Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
37

38.Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu
akamuumba na akamtengeneza vilivyo. 38

39.Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
39

40. Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?
40
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani