HADITHI ZA ALIF LELA U LELA

KITABU CHA KWANZA

 1. SEHEMU YA 1

 2. SEHEMU YA 2

 3. SEHEMU YA 3

 4. SEHEMU YA 4

 5. SEHEMU YA 5

 6. SEHEMU YA 6

 7. SEHEMU YA 7

 8. SEHEMU YA 8

 9. SEHEMU YA 9

 10. SEHEMU YA 10

 11. SEHEMU YA 11

 12. SEHEMU YA 12

 13. SEHEMU YA 13

 14. SEHEMU YA 14

 15. SEHEMU YA 15

 16. SEHEMU YA 16

 17. SEHEMU YA 17

 18. SEHEMU YA 18

 19. SEHEMU YA 19

 20. SEHEMU YA 20

 21. SEHEMU YA 21

 22. SEHEMU YA 22

 23. SEHEMU YA 23

 24. SEHEMU YA 24

 25. SEHEMU YA 25

 26. SEHEMU YA 26

 27. SEHEMU YA 27

 28. SEHEMU YA 28

 29. SEHEMU YA 29

 30. SEHEMU YA 30

 31. SEHEMU YA 31

 32. SEHEMU YA 32

 33. SEHEMU YA 33

 34. SEHEMU YA 34

 35. SEHEMU YA 35

 36. SEHEMU YA 36

 37. SEHEMU YA 37

 38. SEHEMU YA 38

 39. SEHEMU YA 39

 40. SEHEMU YA 40

 41. SEHEMU YA 41

 42. SEHEMU YA 42

 43. SEHEMU YA 43

 44. SEHEMU YA 44

 45. SEHEMU YA 45

 46. SEHEMU YA 46

 47. SEHEMU YA 47

 48. KITABU CHA PILI
ALIF LELA U LELA.UTANGULIZI
Hizi ni hadithi zilizoenea duniani kote na zimekuwa zikisimuliwa kwa watot na hata watu wazima. Hadithi hizi zina asili ya bara la arabu. Hadithi hizi zimekuwa zikitafasiriwa kwenye lugha nyingi sana. Neno ALIF LELA U LELA lina maana miaka elfu moja na moja. Na hadithi hizi hufhamika kwa lugha ya kiingereza kama ARABIAN NIGHT.Hadithi hizi zimetafasiriwa katika lugha nyingi mpaka katika lugha za kiswahili. Changamoto ya masimulizi haya ni kuwa yamesheheni lugha ngumu sana kulinganisha na uhalisia wa maisha yetu ya leo. Hivyo inakuwa vigumu kuelewa baadhi ya manenno nini hasa kimekusudiwa. Pia tamaduni zilizotumiwa na wahusika wa hadithi hizi ni za kiarabu, kihindi na kiajemi kiasi kwamba ni ngumu kuelewa baadhi ya vipengele.Baada ya kuliona hili nimejaribu kutohoa hadithi hizi na kuziweka katika lugha iliyo rahisi kabisa na inayoendana na mazingira ya wakati huu. Hadithi hizi nimezigawa kwenye vitabu kadahaa na tayari kitabu cha kwanza kimekamilika kikiwa na hadithi zaidi ya 60. Unaweza kupata hadithi hizi kama PDF kwa bei poa.KIAPO CHA SULTANI.
Hapo zamani sana katika nchi za Uajemi , china na hindi kulitokea sultani aliyefahamika kwa kuwa na upendo kwa watu wake na nguvu pia ya kijeshi na kuitawala. Watu wake walimpenda sana na yeye aliwapenda. Sultani huyu alikuwa na watoto wawili ambao ni Shahriyar ambaye ndiye mkubwa na mwingine ni Shahzanam ambaye ndiye mdogo.Watoto hawa pia walitambulika kwa ushujaa walio nao na uhodari katika mambo mbalimbali, hususan katika fani ya kupanda farasi. Sultani huyu alipofariki utawala wake akamwachia mwanaye mkubwa ashike madaraka yake. Na mwanae mdogo akabakia anatawala maeneo mengine katika utawala wa baba yake. Huyu mdogo akaelekea maeneo ya Samarkand na huyu mkubwa akabaki palepale.Sultan Shahriyar alikuwa na mke wake aliyempenda sana kwa muda mrefu. Hakuwahi kuamini kama itaweza kutokea sikumoja akamsaliti. Ilitokea sikumoja akamkuta mkewake anazini na mtumwa wake. Kitendo hiki kilimuuma sana na akamuuwa mkewe na yule mtumwa. Kutokea hapo akaapa kutokumwamini mwanamke yeyote duniani. Na kitendo hiki kilimfanya ajiwekee utataratibu mpya wa maisha nao ni kuoa kila siku mke mpya na kisha humuuwa ifikapo asubuhi.Hivyo mambo yakawa kama hivi kila siku jioni bibi harusi mpya mwanamwari huolewa na na ikifika asubuhi huuliwa. Kitendo hiki kiliendelea kwa muda mpaka watu wakawa wanaogopa. Ikiwa nyumba moja watu wanalia kwa kufiwa na bint yoa nyumba nyingine hufanyika harusi. Sultani alikuwa na waziri wake maalum ambaye alikuwa amepewa kazi hii ya kumletea mfalme wanawari na kutekeleza amri ya kuwauwa kila ifikapo asubuhi.Waziri huyu aliyepewa kazi hii alikuwa na watoto wawili aliyewapenda sana, mmoja aliitwa Schehra-zade ambaye ndiye mkubwa na Dinar-zade ambaye ndiye mdogo. Schehra-zade alipata upendo mkubwa kutoka kwa baba yake. Alipewa taaluma mbalimbali za matibabu, sanaa, kuandika, masimulizi , kazi za mikono na nyingine nyingi. Ukiacha mbali na taaluma hizi pia alijulikana kwa uzuri wake ulioaminika kuwashinda wanawake wote katika nchi hiyo. Mabinti wawili hawa walipendana zaidi kila mmoja.Ilitokea siku moja katika mazungunzo waziri mkuu akiwa na mabinti zake wanaongea Schehra-zade alitowa ombi kutoka kwa baba yake ambalo lilionekana kumshangaza sana.
“baba ninaombi ila niahudi kwanza kuwa utanitekelezea” alizungumza Schehra-zade kumwambia baba yake. “naahidi nitalitekeleza kama lipochini ya uwezo wangu” alisikika waziri mkuu akimjibu binti yake.
“ninataka kukomesha tabia ya kikatili ya sultani kuuwa mabint” mmmmhhh mwanangu kipenzi, vip utaweza kumaliza tabia hii ya sultani wetu? Ni maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kati ya waziri na mwanae. “baba ninataka unipeleke mimi kwa sultani niwe mkewe” alizungumza Schehra-zade. Mwanangu unafahamu fika kuwa ukuolewa punde tu ifikapo asubuhi nitaamriwa nikuuwe” alizungunza waziri kwa masikitiko makubwa.Schehra-zade aliendelea kusisitiza ombi lake la kutaka kuolewa na sultani ili akamalize tabia yake ya kuuwa mabinti. Waziri nae hauacha kumsihi mwanae asithubutu kijiingiza kwenye matatizo haya makubwa. Wazii akawa anamwambia mwanae “ hivi mwanangu unataka nikufanye kitugani mpaka uachane na msimamo wako huo? Au unataka yakupate yalompata mke wa mfugaji?” kwa shauku Schehra-zade akauliza “kwani baba ni kitu gani kilimpata mke wa mfugaji” mmmmhh.. Ni habari kubwa lakini nitatakusimulia hadithi yake” alizingumza waziri na kuanza kusimulia hadithi hiiKISA CHA MFUGAJI NA MKEWE.
Hapo zamani kulikuwa na mfugaji maarufu sana na alikuwa ni tajiri na mfanyabiashara aliyekuwa na mafanikio makubwa. Alikuwa anaelewa lugha za wanyama. Alipata tunu hii kwa sharti kuwa asisimulie kwa yeyote mazungumzo ya wanyama na pindi tu akisimulia alichokisikia atakufa hapohapo. Alikuwa akifurahia sana kuwaona wanyama wake na kujuwa nini wanazungumza. Alikuwa na banda lake la wanyama ambapo ndani kulikuwa na ng’ombe na punda, ambapo kazi ya kuwasimamia wanyama hawa alimpa mtumwa wake.Sikumoja alipkuwa amekaa pembeni mwa banda hilo akasikia mazungumzo ya kustaajabisha kati ya punga na ngo’mbe. Ngombe akamwambia punda “ nakuonea wifu kwa raha unayoipata. Wakati mimi ninashinda juani kulima shamba la bwana wetu wewe mwenzangu unaogeshwa na kupambwa na kazi yako ni kummeba bwana wetu, wananipiga, wananifunga majembe yao shingoni. Nakuonea wivu natakani ningekuwa wewe” punda akamwambia ng’ombe “usijali nitakueleza jambo ukilifanya katu hautalimishwa tena.. Kesho akija mfanyakazi mpige mateke na mtishe kwa pembe zako na umfukuze. Kataa kula chakula chao. Ukifnya hivi katu hawata kulimishwa tena”Siku iliyofuata ng’ombe akafanya kama alivyoshauriwa na punda, akamtisha mfanyakazi na akamkimbiza akataka kumchoma kwa pembe zake. Alikataa kula chakula. Siku iliyofuata mfanyakazi akakuta kile chakula alichokilet jana kipo vilevile hivyo akatoa taarifa kwa bwana wake. Mfugaji akamuamuru mfanyakazi wake amchukuwe punda kwenda kulima amfanyie mazoezi. Hivyo siku ile punda akapew mazoezi ya kulima na akalima pia kwa jembe la kubuluza (plau). Jioni akarudi akiwa amechoka sana.Kufika hapa waziri akamwambia mtoto wake Schehra-zade “binti yangu hivi unataka kuangamia kama punda alivyomshauri mwenzie vibaya na akaumia mwenyewe?” Schehra-zade akamwambia baba yake “baba bado msimamo wangu upo pale pale nipeleke kwa sultani nikakomeshe tabia yake. Lakini baba bado sijajuwa mke wa mfugaji kilichompata?” alizungumza Schehra-zade kutaka hadithi iendelee. Waziri akaendelea kumsimulia Schehra-zade hadithi hiiSiki moja mfugaji akiwa na mkewe wameketi karibu na banda la wanyama hawa ili kujuwa nini punda atamshauri mwenzie. Akamsikia punda akimwambia ng’ombe “rafiki yangu nakupa ushauri unisikilize vizuri. Nimemsikia bwana wetu akimwambia mfanya kazi kuwa kama hali yako utaendelea nayo basi uchinjwe na upelekwe buxher ukauzwe nyama. Hivyo nakushauri kesho utii amri ya mfanya kazi hivyo atadhani kuwa ulukuwa umeumwa na sasa umepona” ngo’ombe alionekana kutii ushauri huu. Hapo mfugaji akacheka sanaa. Kicheko hiki kilistaajabisha hata mkewe. Mkewe akataka kujua kinachomchekesha akamjibu ni siri na nikikwambia nitakufa ila naweza kusema kuwa ninacheka kwa sababu ya mazungumzo kati ya punda na ng’ombe.Mke huyu alionekana kuwa na msimamo wa kutaka kujuwa hasa nini mazungumzo hayo nini kilisemwa mpaka akacheka. Akaahidi kama asipomwambia atarudi kwao. Ugomvi ukawa mkubwa ikafikia hatuwa ya kuita ndugu waje kusuluhisha. Mfugaji akabaki na msimamo wake kuwa kama atasema atakufa paohapo na mke akafikia kusema kama asipi niambaia na mimi nitajiuwa. Hali hii iliendelea kwa muda mpaka kufikia hali mbaya zaidi. Mfugaji akiwaza nimwambie ili nife kwa kumridhisha mke wangu au nisimwambie. Na nisipo mwambia atajiuwa. Ni mawazo ya mfugaji. Ugomvi uliendelea kwa siku kadhaa bila ya maelewano pale ndani.Siku moja alikaa nyumbani kwake ghafla akamuona mbwa wake aliyempenda sana anamkimbilia jogoo la kuku. Kisha akamuelezea mambo yote yaliyompata bwana wake yaani mfugaji na mkewe. Hapo jogoo akacheka sana kisha akamwambia “bwana wako ni mpumbavu kweli, hivi hauniono mimi nina wake zaidi ya hamsini hapa na ninafanya ninalo taka, lakini yeye ana mke mmoja tuu pia anampa wakatimgumu hivi. Akieleza siri atakufa hapa dawa ni ndogo tu. Achukuwe fimbo mzuuri kisha amtandike kisawasawa, bila shaka atarudisha akili yake.” Baada ya maneno haya jogoo likawika na kuondoka zake kwa mwendo wa madaha.Mfugaji alifikiri atumie ule ushauri wa jogoo, asubuhi ya siku ilofata mke wa mfugaji aliendelea na vurumai lake. Mfugaji akaagiza aletewe bakora nzuri na kutekeleza ushauri wa jogoo. Mambo yakatulia nyumbani na hakuleta vurumai liole tena. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii waziri akamwambia Schehra-zade “binti yangu, je unataka na mimi nitumie uamuzi wa jogoo?” Schehra-zade akamwambia baba yake “hapana baba ila mi nadhani hadithi hii hainitoshelezi kubadili uamuzi wangu”. Basi waziri baada ya mazungumzo marefu akakubaliana na maamuzi ya mwanae na kukubali kumpeleka kuwa bibi harusi kwa sultan kwa usiku uliofuata.Siku ile waziri akaenda kwa sultan kwa masikitiko na majonzi akamweleza sultan kiola ambacho kilitokea kati ya yeye na binti yake. “sultan Schehra-zade anataka kwa heshima yako awe mkeo japo kwa usiku mmoja tu. Nimejaribu kumnasihi na kumkataza kwa hali zote nilizoziweza lakini imeshindikana” ni mameno ya waziri alo,mwabia sultan. “Unajuwa fika kuwa asubhi baada ya harusi itabidi ushukuwe amri ya kumuuwa na ukishindwa na wewe pia utauliwa na kichwa chako kutundikwa.” ni mameno ya mfalme akisikika anamwambia waziri. Baaada ya mazungumzo marefu Waziri akarudi nyumbani kwa majinzi na kumueleza binti yake ajiandae kwa harusi jiono ilofata.
Schehra-zade akamueleza mdogo wake Dinar-zade “mdogo wangu ninaombi unifanyie huenda likawa ndio la mwisho kabla sijauliwa au likanusuru maisha yangu na maisha ya mabinti wengine wa nchi hii”. Nilipi hilodada? Dinar-zade alimuuliza dada yake. Schehra-zade akaendelea kumweleza “nitakapokuwa nimeingia kwa mfalme nitamwomba ruhusa ya kuwa na wewe katika chumba kile ili nipate kukuaga kabla sijauliwa. Hivyo nikipewa ruhusa hivyo itakapofika saa 11 alfajiri niamshe kisha uliombe nikusimulie hadithi nzuri iwe kama furaha ya kuagana”. Mdogo wake akakubaliana na wazo hilo la dada yake.Hal ilikuwa kama hivyo na harusi ikafanyika kati ya sultan na bint wa waziri mkuu. Bibi harusi akaingia kwenye jumba la kifalme huko akakutana na sura ya sultani. Kwa madaha na manjinjo akamuomba ombi lake la kuruhisiwa kuwa na mdogo wake usiki ule katika chumba kimoja ili aweze kumuaga kesho asubhi kabla ya kuuliwa. Sultan akakubali ombi lile na kuamuru Dinar-zade aletwe na chemba maalumu ikaandaliwa ndani pale. Mambo yakawa kama hivyo usiku haukuwa mrefu kati ya mabint wawili hawa. Ilipofika lisaa limoja kabla ya kupambazuka Dinar-zade akamwambia dada yake “dada yangu kipenzi, naomba unifurahishe kwa kunisimulia hadithi nzuuri iwe kama furaha ya mwisho ya kuagana kabla ya kuuliwa” Schehra-zade kabla ya kumjibu mdogo wake akaomba ruhusa kwa sultan ili amruhusu aweze kutimiza matakwa ya mdogo wake kipenzi. “hakuna shida msimulie tuu ….”’ ni maneno ya mfalme. Hapo Schehra-zade akaanza kusikumulia hadithi kama ifuatavyo.HADITHI YA JINI NA MFANYA BIASHARA.
Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara aliyejulukana kwa utajiri mkubwa sana wa mali na watoto. Alifahamika nchi nzima na aliishi maisha ya upendo na familia yake. Alitoka sikumoja katika safari zake za kibiashara. Alikuwa amepanda farasi akiwa na mfuko uiojaa tende na maji. Alifanya biashara kwa raha na amani na kuanza kurejea baada ya miezi miwili.Siku ya nne baada ya kuanza safari ya kurudi alpita katika jangwa lililofahamika kwa jina la uwanja wa ujinini. Jina hili lilitumika miaka mingi iliyopita na huenda sasa limesahaulika. Mfanyabiashara huyu alipopita eneo hili akaona kuna mti wenye kivuli, hivyo akaamua kuketi ili apate kula chakula. Hivyo akawa anakula tende na kutupa punde pembeni. Alifanya hivi mpaka alipo maliza kula. Karibia na mti ule kulikiwa na kijieneo chenye maji hivyo alipomaliza kula tende zake akanawa mikono na akaswali swala zake.Wakati yupo pale ghafla kulitokea upepo mkali sana na kimbunga, vumbi lilitanda eneo lile. Upepo uliambatana na moshi kisha kukatokea jini kubwa sana. “NITAKUUWA KAMA ULIVYOMUUWA MWANAGU”
ni maneno ya jini yaliyosikika yakimwambia mfanya biashara. Nimefanya nini mpaka ninastahili kuuwawa?” mfanyabiashara akimwambia jini. Jini likaendelea “chagua nikuuwe namna gani.… Wakati ulipokuwa unakula tende zako ukawa unatupa punje na mwanangu alipita eneo lile ukampiga na punje yako akafa papo hapo. Hivyo lazima nikuuwe kama ulivyomuuwa mwanagu”Mfanyabiashra akaendelea kumuomba jini msamaha “nisamehe mkuu, sikukusudia kumuuwa mwanao” jini kwa hasira likawa linajibu, “hakuna msamaha wala huruma hapa nitakuuwa kama ulivyomuuwa mwanangu”. Jini likatowa upanga wake kuuweka tajari kwa ajili ya kumuuwa mfanya biashara.Mpaka kufika hapa Schehra-zade aligunduwa kuwa asubuhi imefika tayari na sultani anatakiwa akaswali na akahudhurie kikao cha baraza. “…. Mmmh ni hadithi nzuri sana dada nimeipenda kweli, hivi mwisho wake utakuweje?, mfanyabiashara atauliwa, au jini litamsamehe?” ni maswali aliyokuwa Dinar-zade akimuuliza dad yake Schehra-zade. “mmh ni nzuri kweli na bado huko mbele ni nzuri zaidi kama sultani ataniruhusu niishi ili kesho nikusimulie muendelezo wa hadithi hii” Schehra-zade alikuwa akimjibu mdogo wake. Sultani akamruhusu asiuliwe ali aje kuimalizia hadithi yake nzuri.Siku ile sultani alitoka akiwa na tabashahsa na hata waziri wake alishangaa kuona sultani ametoka akiwa na tabasamu bla ya kutowa amri ya kumuuwa Schehra-zade kama ilivyo kawaida yake. Sultani alifanya kazi zake za kawaida huku akiwa na shauku la kutaka kujuwa mwendelezo wa kisa cha jini.Usiku uliingia na ilipokaribia alfajiri, sultani hakusubiri akamwambia Schehra-zade “maliza mwendelezo wa hadithi yako, ninashauku la kuta kujuwa mwisho wake”. Basi Schehra-zade akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-Basi yule mfanya biashara alivyoona jini anakaribia kumkata upanga akapiga magoti na kumwambia jini “tafadhali mkuu nina neno naomba unisikilize, nina familia mkuu na nina madeni naomba unipe muda angalau nikaiage familia yangu na kulipa madeni yangu”. “Unataka nikuachie ili ukimbie?” ni jini akimjibu mfanya biashara. “hapana na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa nitarejea hapa hapa, naweka ahadi mbele ya Mwenyezi Mungu” haya maneno aliyasema mfanya biashara.Baada ya kufikiri jini likamuuliza “haya ni muda wa siku ngapi nikupe” naomba unipe mwaka mmoja” akamjibu. Basi jini lile likakubali kichukuwa ahadi ile na likamwacha mfanya biashara papepale na likotoweka. Mfanya biashara akaondoka akiwa na mjonzi makubwa. Alipofika kwake akaieleza familia yake yote yaliyompata.Hakuwa na muda wa kupoteza akalipa madeni yake na kuweka akiba ya kuweza kutumiwa na familia yake pindi atakapo ondoka. Mwaka haukuwa mrefu hatimaye miezi 12 ikawadia. Mfanya biashara kwa majonzi na masikitiko akaaga familia na akaondoka kwenda kutekeleza ahadi yake. Alifika eneo la tukio na kumsubiri jini aje.Katika hali kama hivyo akiwa amekaa kumsubiri jini katokea mzee mmoja akiwa na mbuzi wake. Alistaajabu mzee yule kuona mtu eneo lile hatari. Akmuuliza hasa yaliyomkuta kukaa eneo lile, akampa kisa kizima. Kiasha yule mzee kamwambia “nitakaa hapa hapa na mimi nishuhudie kitakacho tokea”. Punde akatokea mzee mwingine akiwa na mbwa wawili weusi. Naye akataka habari ya kilichowakuta wenzie wale mpaka wakakaa pale. Akasimuliwa kisa kizima, na yeye akabaki pale ili ashuhudie kitakacho endelea. Akaja mzee wa tatu akiwa na mbwa wake mwekundu na akapewa habari na akakaa ili aone kitakacho endelea.Punde wakaona moshi uliofatana na upepo na likatokea jini kubwa lililoshika upanga mkononi mwake. Jini lile haliku msemesha yeyoye likamfuata mfanya biashara na kumwambia “simama ili nikuuwe kama ulivyo muuwa kijana wangu sasa hivi sina huruma leo”.Pale yule mzee mwenye mbuzi akajitupa miguuni mwa jini kisha kwa hisia kubwa kamwambia “ewe mkuu wa majini wa eneo hili, naomba usikiklize hadithi yangu na huyu mbuzi nilyekuwa naye hapa. Kama utaiona inastaajabisha kuliko tukio hadithi ya mwanao na mfanya biashara huyu, iwe kama fidia ya kupunguzia adhabu:. Jini lifafikiri kwa muda na kisha likasema “vizuri sana ebu tuangalie hadithi yako”. Basi mzee yule akaanza kusimulia hadithi yake kama ifuatavyo;-HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE.
Mkuu sasa nakwenda nakwenda kukuhadithia habari ya ngu na huyu mbuzi niliye naye. Kwanza tambua huyu mbuzi unayemuona hapa ni mke wangu wa ndoa niliyeishi naye kwa muda wa miaka 30 bila ya kupata mtoto. Pale nyumbani kulikuwa na mtumwa hivyo nikamfanya mwanangu kwa maandishi.Mke wangu kumbe kitendo hiki hakukipenda kitendo kile. Nilitoka kwa ajili ya shughuli za kibiashara huyu mke wangu alijifundisha uchawi na akambadili mtoto wangu na mama yake kuwa ng’ombe. Kisha akawapeleka kwa mfanya kazi wangu wa shambani ili awalishe na kkuwatunza.Haikupita muda nikarudi kutoka safarini kwangu, na nikamuuliza kuhusu mtoto wangu na mama yake lakini akanijibukuwa mama wa mtoto wangu amefariki inapata miezi miwili sasa. Na kuhusu mtoto wangu ametoweka nyumbani na hafahamiki alipo. Jambo hili lilinishangaza sana lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kumtafuta bila ya mafanikio.Ulipofika msimu wa sikukuu nilimwambia mfanyakazi wangu aniletee ng’ombe aliyenona ili nimchinje kwa ajili ya kusherehekea sikukuu. Nililetewa ng’ombe mmoja mzuri sana mwenye afya. Jambo lililonishangaza wakati nataka nimchinje ng’ombe huyu alikuwa akitoa machozi na akiniangalia kwa huruma. Kwakweli jambo hili halijawahi kutokea. Nikaagizwa arudishwe na niletewe mwengine.Mkewangu alikasirika kuona ng’ombe anarudishwa, akanifata na kunisisitiza nimchinje. Nikamweleza mfanyakazi wangu amchinje yeye mii siwezi. Basi akamchinja ng’ombe yule. Jambo la ajabu ni kuwa ijapokuwa ng’ombe yule alikuwa amenenepa lakini hakuwa na nyamba ila ni mifupa mitupu. Nilishangazwa sana. Nikaagiza niletewe mwengine, na akaletwa ndama mmoja aliyenenepa vizuri. Huyu pia alifanya kama yule wa mwanzo alikuwa akitowa machozi na akajilaza miguuni mwangu kama anaomba aachiwe asiuliwe.Huruma ilinijaa na nikaamua aondolewe aletwe mwingine. Mke wangu akanilazimisha ili nimchinge. Nikamuweka vizuri ili kuanza kumchinja, niliweka kisu kooni na nilipokaribia kumchinja aliniangalia kwa jinjo la unjonge na huku akitowa machozi. Kisu kilianguka na nikashindwa kumchinja. Nikaagiza arudishwe. Mke wangu alikasirika sana lakini mara hii sikubadili kauli yannguSiku ilofata mfanyakazi wangu alinifata kwa mazungumzo ya faragha akanieleza kuwa binti yake ana taaluma ya uchawi hivyo anataka kuzungumza na wewe faragha. Ilibidi nikutane nae, mazungumzo yake yaninistaajabisha sana. “mkuu ulipoondoka mkeo alijifunza uchawi na akambadili mtoto wako na yule mama yake kuwa ng’ombe. Yule ulomchinja jana ni mama yake na yule ng’ombe mdogo ulomrudisha ndiye mwanao. Nitaweza kumrudisha mwanao kawaida kwa masharti, kwanza uniwachie mkeo nimpe adhabu, na pili uniozeshe mwanao.” haya yalikuwa maneno ya binti wa mfanyakazi wangu. Nilikubaliana na masharti yale.Yule binti akachukuwa maji na akatamka maneno nisiyoyajuwa kisha akammwagia yule ng’ombe, papo hapo akawa katik umbo labinadamu. Nilifulahi sana. Kama mashart tulokubaliana alimfata mke wangu na kutamka maneno flani na mke wangu akageuka kuwa mbuzi huyu ambaye unamuona.Ni muda mrefu sasa hatujaonana na mwanangu hivyo nimetoka ili kama nitaweza kupata taarifa zake zozote. Hivyo nimeona ubaya kumuacha mke wangu huyu mbuzi chin ya uangalizi wa watu wengine. Nikaona bora nimchukuwe. Hii ndio stori yangu ewe mkubwa katika majini.“naam nakubaliana na stori yako, kweli inasikitisha hivyo nitampunguzia adhabu huyu mtu” ni maneno ya jini akimwambia mzee wa kwanza. Baada ya huyu mzee wa kwanza kuzungumza, mzee wa pili akapiga magoti kwa lile jini akaliambia, “ewe mkuu katika majini naomba usikilize na mimi stori yangu na hawa mbwa wawili, kama utaona inasikitisha zaidi naomba umpunguzie adhabu huyu mtu”.HADITHI YA MZEE WA PILI NA MBWA WAWILI WEUSI.
Mzee wa pili akapewa ruhusa ya kusimulia stori yake na mbwa wawili weusi. “kwanza utambue ewe mkuu wa majini kuwa hawa mbwa unaowaona ni ndugu zangu wa baba na mama mmoja, stori ilikuwa hivi”Baba yety alikuwa ni tajiri mkubwa katika mji tuliokuwa tukiishi. Alipofariki alituachia mali kubwa na tukaigawa mafungu matatu kulingana na idadi yetu. Tuligawana sawa kwa sawa. Ndugu zangu hawa wakajikita kwenye biashara za nje na ndani ya mji. Wakawa wanasafirisha bdhaa kwenda miji mbali mbali, na hata kwenye visiwa.Mimi niliamua kufungua duka hapa mjini na kwa neema za Allah biashara ikawa nzuri. Mali yangu ilifikia mara tatu ya ile niliopata kutoka kwenye urithi. Sikumoja ndugu zangu walitoka kibiashara, walikaa kwa muda wa miezi isiyopunguwa miwili. Baada ya hapo nikaona kuna watu wawili wamesimama mbele ya duka langu. Sikuwatambuwa watu hawa kutokana na mavazi yao. Walikuwa wamevaa mavazi yaliyochakaa ama yaliyookotwa jaani. Niliataajanu kuona wana nifahamu, baada ya kuzingatia zaidi nikagunduwa ni ndugu zangu.Nikawapa mavazi na chakula kisha wakanihadithia mkasa wao. Walikuwa wamepata ajali na malizao zote zimetokomea majini. Nikachukuwa ile faida yangu na nikaigawa sasa kwa sawa kati yao. Wakaanza biashara tena na hawakukoma baada ya muda wakaamua kusafiri tena kibiashara. Hali ilikuwa mbaya zaidi wakati huu. Walipata ajali tena majini na wakktupiwa nchi kavu wakuiwa hata mavazi hawana.Niwalipfika nyumbani sikuwatambuwa kwa kuwa walikuwa uchi na wakiwa wamechafuka ngozi zao. Wakajitambulisha na niliilia kwa huruma. Machozi yangu nhayakufaha kitu kwa kuwa tayari jambo lilisha tokea. Kama mara ya kwanza nikawapa mtaji na wakaanza upya biashara zaoi. Baada ya muda biashara zao zikakaa vizuri, na wakaamuwa kutoka tena kibiashara. Ila mara hii walitaka niende pamoja nao. Nilipinga zaidi safari hii lakini walinilazimisha na hata maandalizi pia wakanifanyia.Sikuwa na jinsi nikajiandaa na mimi kwa safari. Nikachukuwa mali zangu nikazigawa sehemu mbili na sehemu moja nikachukuwa na nyingine nikaificha. Safari ilianza vizuri na tulifika miji mbalimbali tukifanya biashara. Nilipata faida kubwa na nikanunuwa baadhi ya bidhaa ambazo ningeziuza pindi nitakapo rejea.Muda wa kurudi uliwadia tukawa tunaanda safari ya kurudi. Nilipokuwa matembezini nikitafuta bidhaa na zawadi za kwenda nazo nyumbani, nilipita ufukweni nikakutana na mwanamke aliyevaa mavazi yaliyo chakaa. Nilimsalimia na akarudisha salamu, nikamchukuwa na kumtafutia mavazi yaliyo mazuri. Kwa mavazi yale uzuri wake ulidhihiri mbele yangu. Kwakuwa sikuwa na mke ilibidi nifuate taratibi za kufunga nae ndoa na akakubali. Maandalizi yote yalipoisha nilimchukuwa mke wangu kurudi nae nyumbani.Tukiwa kwenye jahazi zikugunduwa kumbe ndugu zangu walikuwa wananionea wivu. Wakawa wananipangia njama ya kuniuwa. Ulipofika usiku walinichukuwa na kunitumbukiza majini. Baada ya pale sikujuwa kilichoendelea nikajikuta nipo nchi kavu. Mke wangu akanieleza khabari za yote yaliyotokea na akanieleza kuwa yeye si mtu wakawaida. Akaniambia pia hatoweza kuwasamehe ndugu zangu kwa walichonifanyia. Nilimuomba asiwaue ila nipo radhi kwa adhabu yeyote ile.Alinichukuwa mpaka nyumbani kwangu, kisha akalizamisha jahazi waliopanda ndugu zangu. Mali zangu zote akaziokoa. Siku iliyofata nikiwa nyumbani nikaona kuna mbwa wawili weusi wanakuja huku wakionesha majonzi na hali ya kuomba msamaha. Nilistaajabishwa na tukio hili. Haukupita muda mke wangu akatokea na akaniambia hawa ni nduguzangu amewapa adhabu hii. Watakuwa hivyo kwa muda wa miaka 10.Miaka 10 sasa imefika, na kwakuwa alinielekeza sehemu ya kukutana, ndio nimetoka kuelekea hapo sehemu. Nikaona niwachukuwe ndugu zangu kwa kuhofia kuwaacha kwa mtu asie akawadhuru.Hii ndio stori yangu na mbwa hawa ewe mkuu wa majini. “hii ya kwako inamakubwa zaidi” ni maneno ya jini. Baada ya hapo mzee wa tatu akazitupa miguuni kwa jini na kutaka ruhusa aruhusiwe kughadithia stori yake ili iwe ni kafara ya kuachiwa huru mfanya biashara. Lile jini likasema “hapana nimetosheka na hizi mbili, na nimekubali kumuacha huru mfanya biashara” jini lilizungumza maneno haya na kuondoka.Mfanya biashara akawashukuru wazee wale. Basi wakati wazee wale wapokaribu na kuondoka yule mfanya biashara akamuuliza mzee yule wa tatu mwenye mbwa mwekundu kuhusu habari ya mbwa yule. Mzee akamwambia ni stori ndefu ila kwa ufupi huyu ni mke wangu. Akaanza kusimulia hadithi yake kwa ufupi huku akiwa na haraka ya kutaka kuondoka eneo lileHADITHI YA MZEE WA TATU NA MBWA WAKE MWEKUNDU
Kama nilivyotangulia kusema , huyu ni mkewangu wa ndoa tulioishi pamoja kwa muda wa miaka zaidi ya kuni na tano sasa.mkewangu nilimpenda sana. Niliamini ananipenda sana pia. Bila ya kujua kinachoendelea kumbe alikuwa anajiiba na kuzini na moja ya watumwa wangu pale ndani. Ilichukuwa muda mrefu mpaka nilivyogundu tabia hii mabya ya mkewangu.Basi siku moja nikaaga safari ya dharura lakini lengo langu nilitaka nimtegee ili nimkamate. Niliondoka nyumbani vizuri lakini nikarejea nyumbanni usiku ule na kumkuta mke wangua na yule mtumwa wakiwa wanafanya madhambi. Hali ile iliniumiza sana. Lakini mkewangu hata bila ya aibu akachukuwa maji na kuyasemea maneno ya kichawi na kunimwagia usoni. Hapo nikaanza kuunguwa mwili mzina na hatimaye nikabadilika kuwa mbwa.Basi nilipojiona nimekuwa mbwa nikaondoka pale ndani na kuenda kwenye duka la mfanya biashara mmoja. Yule mfanya biashara akawa ananionea huruma kulikuwa na mbwa wengine wanataka kunipiga basi yule mfanya biashara akawa ananigombea. Ulipofika muda wa mchana binti yake mfanya bishara akaja kumletea chakula baba yake. Ghafla tu macho yangu na ya yule binti yalipo kutana nikahisi hali flani ya mabadiliko usoni kwa yule binti.Baada ya mfanya biashara kual akanipatia mabaki yale ya chakua na kunipatia. Yule binti akamuuliza baba yake “baba umepata wapi mbwa mzuri huyu?”. “hapana amekuja mwenyewe hapa”. Basi binti akamwambia baba yake “baba uanjuwa huyu sio mbwa wa awaida, huyu ni binadamu aliyegeuzwa mbwa” niliposikia maneno yale nikawa natingisha kichwa isara ya kuyaunga mkono maneno yale. “sasa unaweza kumrudisha katika hali ya kawaida?” aliuliza mfanya bishara. “ndio baba naweza” ni majibu ya binti.
Basi binti akachukuwa maji na akayasemea maneno yasiyo eelweka na kunimwagia usoni. Palel aple nikawa katika umbo la kawaida. Kisha akamwendea mke wangu na kumgeuza kuwa mbwa kama alivyonifanya mimi. Kisha akanielekeza sehemu ya kukutana nae itakapofika miaka 10. Hivyo miaka 10 sasa imefika ndio niko safarini kukutana nae ili amrudishie mke wangu umbo lake mwenyewe. Ndio nikakutana na nyinyi hapa. Basi waztu wote wanne wale wakaachana pale na kila mmoja akaenda na safari zake.Baada ya kumaliza hadithi hii Schehra-zade akamwambia mdogo wake “vip unaionaje hadithi hii” “mmmmhmmh … Ni nzuri sana dada, ila ni ipi hadithi ya yule mzee wa tatu”? Ni maneno ya Dinar-zade. “hata mimi sijui ila naamini ni nzuri zaid, lakini haiwezi kushinda hadithi ya mvuvi na jini” alisikika Schehra-zade akimweleza mdogowake. Sultani akadakia “ooh, kama hii nzuri hivi vp hiyo ya mvuvi na jini, natamani kuisikiliza,”
Schehra-zade akaongea “kama utanipa siku nyingine zaidi naamini utaflaiya hadithi hii”. Basi siku ile Schehra-zade hakuuliwa na siku ilofata mfalme akamuleza asimulie hadithi ya mvuvi na jini. Schehra-zade bila ya kuchelewa kaanza kusimulia kama ifuatavyoHADITHI YA MVUVI NA JINI
Hapao zamani kulikuwepo na mvuvi aliyekuwa masikini wenye watoto watatu na mke mmoja. Alikuwa anavuwa kwa kutumia nyavu ya kutupa. Alijiwekea sheria ya kutupa nyavu mara nne kwa siku.Alitoka sikumoja asubuhi, akatupa nyavu yake mara ya kwanza na asiambulie kitu. Akarudi nyumbani na kurudi baada ya muda, akatupa nyavu yake na akaambulia mauchavu. Akatupa mara ya tatau akaambulia mauchafu bila ya samaki. Na hapo nyavu yake alikuwa imeharibiwa hivyo akaishona na kuiweka tayari kutupa mara ya mwisho. Mara hii alipotupa aliambukia kuvua lichiupa la shaba lenye mfuniko wa silva.Kwa kutaka kujuwa kilichomo mule akaamua kuofunguwa chupa ile. Akaanza kuitowa kifuniko. Ghafta akaona moshi mkubwa unatoka kwenye ile chupa. Moshi ukajikusanya angani kama kiwingu na punde tu kukatokea jini kubwa sana. “chaguwa mwenyewe kifo cha kukuuwa” ni sauti ya kushangaza ya jini lile. Mvuvi akashngaa kusikia anaambiwa achaguwe kifo.“nimefanya nini mkuu? Na wewe ni nani? Na umetoka wapi?”. Ni fgurushi la maswali ya mvuvi kuliuliza lile jini.“Mimi ni jini nilikuwa nimefungiwa kwenye chupa hii na mkuu wangu, na wewe ndo umenifungulia”. Ni maneno ya jini
Mkuvu akamuuliza “sasa kama nimekufungulia ulipokuwa umefungu ina maana nimekutendea wema , haya mbona unataka kuniuwa”?“nilifanya kosa na mkuu wangu akanifungia humu, miaka mia moja kwa kwanza niliahidi atakaye nifungulia nitampa utajiri mkubwa. Mika ile ikapita na sikupata wa kunifungulia. Miaka nia ya pili nikaahidi atakaye nifungulia nitampa thamani kubwa ya duniani, pia hakutokea wa kunifungulia. Miaka mia ta tatun nikaahidi atakaye nifungulia nitamfanya mfalme na nimpa anachotaka kwa kila siku. Pia miaka hii ikapita bila ya kufunguliwa. Baada ya hapo nikaahidi kuwa atakaye nifungulia nitamuuwa ila nitampa nafasi ya kuchagywa kifo atakachotaka. Hivyo wewe ndo umekuja kunifungulia, chaguwa kifo gani unataka ufe”.Mvuvi akamwambia hule jini, “mimi siamini kama umetoka humu kwe nye chupa. Umeingiaje humu wewe mkubwa hivyo kwenye kichupa kidogo hiki?. Hebu ingia nikuone ndo nitaamini”.Yule jini akajirudisha kwenye jhali ya moshi na akaingia kwenye ile chupa. “umeona sasa nilivyoingia?, nipo kwenye chupa sasa, umeamini?” ni maneno ya jini kumwambia mvuvi. Mvuvi baada ya pale kwa haraka zaidi akachukuwa kifuniko na akaifunga chupa. “sasa nitakurudisha kulekule baharini ulikokuwa.” ni maneno ya mvuvi akimwambia jini.Jini akajitahidi atoke lakini akashindwa ikabidi amwambie mvuvi “ naomba nifungulie, nitakupa utajiri ukunifungulia” mvuvi kwa sauti kubwa akamjibu “hapana siwezi kukutowa usije ukawa umenidanganya. Nitakutupa baharini na nitaweka tangazo hapa ili atakaye ivua chupa ajuwe kuna jini airudishe”.Jini likaanza kujitetea kwa saiti ya kinyonge “nakuomba, nakuahidi pia unifungulie, nitakupa utajiri”. Mvuvi kwa sauti ya busara akamjibu “naogopa yasije yakanikuta yaliyompata tabibu wa mfalme.” “ni yapi hayo yaliyompata tabibu?” ni swali la jini kumuuliza mvuvu. Mvuvi akaanza kusimulia hadithi ya tabibu kama ifuatavyo;-HADITHI YA TABIBU WA MFALME
Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Mfalme huya alipenda kusoma na kucheza mpira wa farasi, alimwamini sana waziri wake. Mfalme huyu alikuwa na ugonjwa ambao matatibu wengi walijitahidi lakini walishindwa. Kila tabibu mzuri katika nchi yake alijaribu bila ya mafanikio. Mfalme alikata tamaa ya kupon augonjwa wake.Ilitokea katika nchi ile kuna tabibu ambaye ni mjuzi sana lakini hakutambuwa kama mfalme ana tatizo hilo. Tabibu huyu aliitwa Douban. Alipo[ata taarifa za ugnjwa wa mfalme alikusanya mavitabu yote na utabibu na kuanza kustadili kuhusu ugonjwa wa mfalme wake. Na hatimaye akafanikiwa kugunduwa dawa itakayomtibu mafalme. Dawa ambayo ingemtibu mfalme hata bila ya kumgusa.
Siku ilofata alivaa nguo zake safi za kitabibu na akaenda ikulu kuomba kumuona mfalme. Kwa kuwa alijitambulisha kama tabibuilikuwa ni rahisi kwake kumuona mfalme. Alipiga magoti na kumueleza mfalme kilicho mleta. “nina dawa ya kutibu maradhi yako hata bila ya kukugusa kwa uwezo wa Allah” ni tabibu akimwambia mfalme. “ukitibu maradhi nilonayo nitakufanya tajiri na utakuwa ni katika watu wangu wa karibu” kwa furaha mfalme akimwambia tabibu Douban. “Ndio mkuu tutaanza tiba yetu kesho IN shaa Allah” ni maneno aliyoyasema tabibu.Siku hiyo tabibu alivaa safi mavari yake na kuiweka dawa yake tayari kwa ajili ya kumtibu mfalme. Aliiweka dawa yake kwenye fimbo ya kuchezea mpira wa farasi. Kisha akamwambia mfalme atumie fimbo ile kuchezea mpira wa farasi na apige kwa nguvu mpaka jasho limtoke. Mambo yaka wa kama hivyo na mechi ikaanza. Mfalme alicheza kwa uwezo wake wote na akawa anapiga mpira kwa fimbo yenyedawa. Kila anapopiga ndio dawa inavyiongia kutoka kwenye fimbo kuingia mwilini mwake. Mechi ilipoisha akamwambia mfalme akifika nyumbani kwake aoge kisha alale. Mfalme alifanya vivyohivyo na alipoamka ailikuwa ni asubuhi. Alistaajabu kuona ampona kabisa maradhi yake.Aliagiza tabibu Douban aletwe mbele yake ili amlippe alichomwahidi. Mambo yakawa vivyo hivyo aliletwa tabibu na kutoa heshima kwa mfalme. Mfalme alifurahi na kumpa utajiri yeye na familia yake. Tabibu Douban akawa ni katika watu wa karibu na mfalme. Baadhi ya viongozi wa nchi walimonelea wivi tabibu. Waziri mkuu alikuwa ni muhanga wa jambo hili. Alikuwa akikasirika sana kumuona tabibu na mfalme. Hakupenda ukaribu wao na alitafura mbinu na njama mbalimbali kuweza kuwatenganisha.Sikumoja kaamuwa kutekeleza mpango wake, alimfata mfalme na akamweleza kuwa amegunduwa kuwa huyu tabibu anataka kukuuwa. “kama angetaka kuniuwa kwa nini amenitibu” ni swali la mfalme kwa waziri. “huenda ange kuuwa muda ule angejulikana, lakin sasa umemwamini muda si mrefu atatekeleza madhambi yake” waziri akimjibu mfalme. Mabishano haya yalichukuwa muda mfalme akimtetea tabibu na waziri akimkandamiza tabibu. Mwisho mfalme akamwambia tabibu “nakumbuka vizuri maneno ya waziri mfani alipomwambia mfalme Sinbad alipotaka kumkinga mwanae asiuliwe” . “ni maneno ganihayo ewe mfalme wangu” waziri akimuuliza mfalme kwa shauku. Mfalme akamjibu “alimwambia usiamini maneno ya mtu yeyote hata akiwa mkweo kisha akamsimulia hadithi hii”;-HADITHI YA MKE NA KASUKU.
Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara, ambaye alikuwa na familia yake na mkewe ambaye alimpenda san. Hakuamini kama atakuja kuachana naye. Kwakuwa yeye ni mfanya biashara alikuwa akisafiri mara kwa mara. Ijapokuwa kuanwatu walikuwa wakimpa maneno kuhusu mkewe alikuwa ahawaamini. Ilifikia wakati sasa aliingiwa na mawazo ya kutaka kuwaamini japo hakufanya hivyo,Sikumoja alipopata safasi alikwenda kwenye maduka yanayouzwa ndege wa kufuga. Alinunuwa kasuku mmoja laiye mzuri sana. Kasuku huyu pia alikuwa na uwezo wa kuzungumza habari zilizofanyika wakati bwana wake hayupo. Alimnun ua kasuku yule kwa gharama za juu na akamuweka kwenya kitundu chake. Alimpelekea mkewe na kumwambia “mtunze ndege wangu huyu, na umuweke ndandi na katu usimtowe”. Mke alitii ankumchukuwa kasuku yule na kumugifadhi ndani.Mfanya biashara huye alitoka na kuenda mbali ya mji. Huku nyuma mkewe akafanya ya kuyafanya pale ndani. Ulipofika wakati mfanya biashara alirejea nyumbani. Alimchukuwa kasuku wake na kutoka naye nyumbani ili kutafute mahala pa faragha kisha akamuuliza kasuku kilichofanyaka pale ndani wakati hayupo. Kasuku aliyasema yote aliyoyaona na hayakumpendeza yule mfanya biashara. Aliporejea nyumbani aligombana saa na mkewe. Mke alishangaa ni nani alomwambia. Aliwapa adhabu watumishi wake akidhani ndio walovunja siri. Ila baada ya muda akagunduwa kuwa ni kasuku ndiye muongo.Mfanyabiashara laipata safari nyingine ya kibiashara. Alipoondoka yule mkewe alipotaka mufanya anayoyafanyaga aliwaita wajakazi wake watatu. Mmoja akamwambia aweke beseni la maji chini ya tundu la kasuku, na mwengine akamwabia maji juu ya tundu la kasuku na mwinguni akamwambia achukuwe kioo na kwa kutumia mwanga wa mshumaa ammulike kasuku kwa mwanga uloakisiwa na kioo. Akamwambia afanya hivi kulia na kushoto. Wakati mambo yote haya yakifanyika yule mke nae alikuwa akifanya mambo yake anayoyafanyaga wakati mumewe akiondoka.Siku ilofata mfanyabiashara akarudi nyumbani. Akamuuliza kasuku kilichotokea kasuku akamwambia “mmh bwana wangu mvua ilikuwa kubwa pamoja na radi nilishindwa kujuwa kinachotokea.” yule mfanyabiashara alijuwa kuwa hakuna mvua ilonyesha usiku ule. Akaona kuwa kasuku ni muongo hivyo akaamua amchinye. Baada ya siku akaja kugunduwa kuwa kasuku alikuwa mkweli ila alichezewa mchezo, alijilaumu sana lakini lawama zisingemrudisha kasuku.Baada ya kumaliza kuzungumza hadithi hii (mvuvi akamwambia jini maneno aliyoyasema ) mfalme akamwambia waziri “sitakusikiliza kwa hili, nitamshughulikia tabibu na kama nisije nikajuta kama mfanya biashara alivyojuta baada ya kumuuwa kasuku asiye na hatia”. Waziri akajibu “mfalme tabibu anataka kukuuwa, siwezi kumuacha na kama itatokea nimefanya kosa nitakuwa tayari kuadhibiwa kama alivyoadhibia waziri wa mfalme flani” “alifanya nini huyo waziri” ni swali aliodakia mfalme. Waziri akasimulia hadithi ifuatayo;-HADITHI YA WAZIRI ALIYEADHIBIWA.
Kulikuwa na mfalme aliyekuwa na mtoto wake mmoja wa kiume. Alimpenda sana mtoto huyu, huenda ni kwa sababu alikuwa ni mmoja na ni wakipekee. Mtoto huyu alipenda sana kuwinda na alikuwa ni hodari wa kupanda farasi, hasa alikuwa na uwezo wa kumdandia farasi kwa haraka sana. Zaidi haayo aliweza kuelewa lugha nyingi. Alikuwa anapokwenda kuwinda akienda na waziri ambaye alipewa kazi ya kumlinda mtoto huyu.Walitoka sikumoja kwenda kuwinda, waliwinda kwa muda mrefu bila ya kupata kitu. Mtoto huyu akaona kibendera kimenyanyuliwa (isharaya kuonekana kiwindwa) alijuwa kuwa aliyonyanyuwa ni waziri. Basi akakifata kibendera na akakutana na swala mzuri mwenye afya. Alimfata na swala akikimbia, alichukuwa muda mwingi na hatimaye akaamuwa kurudi. Kwa bahati mabya alipotea nyia na asijuwe pa kurudia. Hakujuwa waziri yupo wapi, hivyo akazidi kutokomea mwituni.Ilipofika karibia na jioni alikutana na bint mmoja msituni, akamkaribia na kumsalimia. “unafanya nini hapa na na ninnani wewe?” ni maswali aliyomuuliza binti yule. “mimi ni mtoto wa mfalme wa hindi na hapa nimepote” yalikuwa majibu ya bint. Basi akamchukuwa kwenye farasi wake na wakawa wanatafuta njia. Wakapita sehemu kuna jumba lililohamwa siku nyingi. Yule bint akashuka na kijana akashuka pia. Bint akawa anaelekea mule ndani. Alipoingia ndani yule kijana akiwa nje akasikia sauti ya yule bint ndani kwa lugha ya kihindi (yule binti alidhani yule kijana hatelewa lugha ile) “wanangu nimekuleteeni nyama kubwa yenye afya leo” akasikia sauti nyingine zikijibu “iko wapi mama tuile tuna njaa sana mama”. Kijana akagunduwa yule bint si mtu wa kawid,Yule kijana kusikia vile kwa uhodari alio nao akaruka kweye farasi haraka na kuondoka. Baada ya mwendo wa dakika kadhaa akakutana na njia ya kuelekea kwao. Alipofika akamweleza baba yake kuhusu kilicho tokea. Mfalme alikasirika na akamwadhibu waziri kwa kutokuwa makini na kusababisha ajali kwa mwanae.Baada ya kusimulia hadithi hii waziri akamwambia mfalme “angalia sana mfalme, unaonekana umemwamini sana tabibu, lakini usijejuta kwa kumuamini kwako kama alivyojuta huyu mfalme aliyemwadhibu waziri wake baada ya kumwamini”. Maneno haya yalimpenye sana mfalme, hivyo akaamuwa kumuamini waziri wake. Hivyo akaamuwa kumuuwa yule tabibu wake.Siku iliyofuata akaamrisha askari wakamkamate tabibu na kumleta mbele yake. Tabibu akiwa hajui kinachoendelea, anashangaa kuambiwa amekamatwa kwa kosa la kupanga njama za kumuua mfalme. Tabibu akawa anajitetea “sasa kama ningetaka kumuuwa mfalme ina maana gani nikamponya?”. Ijapokuwa alizidi kujitetea lakini mfalme alishaamuwa ubaya hivyo hakusikiliza maelezo yake.Katika hali ngumu kama hii, yule tabibu akataka apewe ruhusa ya mwisho kuzungumza. “zungumza bila shaka, hata uzungumze vip leo utauliwa tu rafiki yangu tabibu.”. Ni maneno yaliyojaa kejeli kutoka kwa mfalme. Tabibu akazungumza “mimi sina kosa mfalme, ninaapa kwa jina la Allah, mimi sina kosa kabisa, lakini kama haina budi mimi kuuliwa, kuna kitabu changu kipo nyumbani, kitazungumza ukweli wote, juu yangu mimi. Kitabu hiki kitazungumza pindi utakapo niua”.Baada ya mazungumzo haya mfalme akapatwa na mshangao na kuzungumza kimoyomoyo “yaani ili hicho kitabu kizungumze ukweli wa mambo mpaka wewe nikuuwe ndo kizungumze? Hii kweli ni khabarikubwa. Basi sina budu kukuuwa ili nione maajabu ya kitabu kinachozungumza”. Mfalme akamuuliza tabibu tukupe muda gani ukakilete hicho kitabu? “miachieni leo ili niweze kukiandaa kisha kesho nitakuja nacho hapa, na hukumu yangu itatekelezwa.” ni maneno ya tabibu kumwambia mfalme.Basi mfalme akaamrisha askari wake wamlinde tabibu. Tabubu alipotoka pale akaenda nyumbani kwake na kuiaga familia yeke kwa uchungu na machozi ya hali ya juu. Baada ya pale akachukuwa hicho kitabu akakipaka dawa iliyo na rangi ya kijibu. Dawa hii ipo kama ungaunga, na haina harufu kali. Akakipaka kitabu kurasa zote. Ilipofika asubuhi akachukuwa beseni la maji lakini halikuwa na kitu ndani na akatoka kwake akiongozwa na askari wa mfalme. Alipofika sehemu ya hukumu akaanza kutoa maelekezo yake.“nitakapokuwa nimeuliwa chukueni kichwa changu kisha kiwekeni juu ya kitabu kilichopo kwenye beseni hili. Pindi damu itakapoanza kutotesha gamba la nje la kitabu hiki mfalme atakichukuwa na kufungua mpaka ukurasa wa 6 wa kitabu hiki.” haya yalikuwa ni maelekezo ya tabibu kwa mfalme kuonesha maandalizi ya kitabu kitakachozubgumza. Basi haukupita muda dabibu akauawa kwa upanga.Kwa shauku mfalme akafuata maelekezo kama alivyoambiwa. Damu ilipoanza kutotesha kitabu akakichukuwa kwa shauku kubwa. Akawa analamba kidole chake kutia mate ili afunguwe kurasa kwa urahisi, kichwa kikasema “funguwa mpaka ukurasa wa sita”. Akaanza kufunguwa huku anatia mate kidole na kisha nafungua, alifanya hivi mpaka akafika kurasa wa sita na hakukuta maandishi yoyote. Kichwa kikasema “fungua mpaka mwisho” akaendelea kufungua huku analamba kidole kutia mate, mpaka akafika mwisho na asione chochote.Ghafla macho yake yakaanza kulegea na mwili ukaanza kupoteza nguvu, damu zikaanza kutoka puani, kisha kichwa kikaseme “na ukatili wako, haukujuwa kama ulikuwa ukilamba sumu iliyopo kwenye kurasa. Umebakiwa na muda mchache kufa. Hivi ndivyo watu waovu wanavyolipwa uovu.” baada ya maneno haya kichwa kikapoteza maisha na haukuchukuwa muda mfalme akafa huku anajuta kwa kumuua tabibu na kuamini maneno ya waziri wake.Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mvuvi akamwambia jini “kama mfalme angemwamini tabibu na kupotezea maneno ya waziri wake, haya yole yasingetokea. Hivi pia ndivyo itakavyokuwa kati ya mimi na wewe, nikikuamini nitajuta. Hivyo mimi nakutupa baharini sasa hivi na nitaweka alama na tangazo hapa ili kula mvuvi ajuwe kilichopo hapa nin nini. Na nitajenga na nyumba pia nitakaa hapa kuwaonya wavuvi.Jini kusikia maneno haya akamwambia usinifanyie kama imma alivyomfanyia ateka. Mvuvi kwa shauku akauliza “kwani imma alinfanyia nini ateka?”. Jini likamjibu “unadhani nitakwambia wakati umenifungia humu?, nifungulie na nakuahidi nitakufanya tajiri maisha yako yote, nakuahidi”. Mvuvi kwa kupenda mali akakubali ahadi ya jini na akamfungulia, jini lilipotoka likapiga teke chupa ile na likacheka kwa sauti ya juu. Hali hii ilimuogopesha sana mvuvi. “usiogope rafiki yangu, nimefanya hivi kukutisha tuu, mimi naamini sana ahadi”. Ni maneno ya jini kumwambia mvuvi. Kisha akamwambia amfate na achuuwe na nyavu zake.Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini. Walikwnda kwa muda usiopunguwa masaa saba. Kisha wakakutana na milima minne. Wakaipanda milima ile juu ya milima wakakuta kuna kijibwawa cha maji yaliyo meupe sana. Kisha jini akamwambia mvuvi atupe nyavu yake. Alipotupa akavuwa samaki wanne wa rangi tofauti. Mvuvi alishangaa hajawahi ona samaki wenye umbo na rangi kama hizi maishani kwakwe. Kisha jini likamwambia “chukuwa samaki hawa na ukawauze kwa mfalme, utapata utajiri bila shaka. Ila kumbuka utavua hapa kwa siku mara moja tu?” kisha jini likapiga miguu yake chini na kupotea.Mvuvi akatoka na samaki wake wale na akakutana na mpishi wa mfalme, mpishi akawachukuwa samaki wale mpka kwa mfalme. Mfalme alishangaa uzuri ulioje wa samaki wale. Akawanunua kwa pesa nyingi sana iliyomfanya mvuvi asahau maisha ya kimasiki jitena. Mpishi akatoka kwendapika samaki wale. Akaanza kuwakaanga , pindi walipoanza kuiva, upande mmoja akawageuza ghafla akashangaa ukuta wa jiko umepasuka na kukatokea mwanamke mzuuri. Mwanamke yule akaaambia samaki “je mnafanye kazi niliyo watuma?” samaki wakamjibu “ndio tunafanya kaz” kisha mwanamke yule akapiga teke karai lile na samaki wakaanguka na kugeuka mkaa. Baada ya hapo akapoka na ukuta ukarudi ukawa kama vile ulivyokuwa.Matukio yote haya yakifanyika mpishi aliyaona, na alikuwa akishangaa. Zaidi ni pale alipoona samaki wa mfalme wamegeuka mkaa, aliogopa sana na akatoka kumtafuta mvuvi ili amwambie amletee wengine. Kwa kuwa mvuvi aliwauza wawili akampatia wale wawili walobakia kwa pesa nyingi sana. Kisha mpishi akaenda jikoni. Tukio lielile likatokea tena na samaki wakageuka mkaa. Mara hii aliamua kumweleza mfalme mfalme alishangaa sana na kaamrisha aletwe mvuvi. Mvuvi alipofika akampewa amri ya kuleta samaki kama wale siku itakayofata.Mambo yakawa kama hivi siku ilofata mvuvi akawaleta samaki wale na akapewa pesa kama ile ya jana mara mbili yake maana amempa wote wanne. Mfalme akaingia jikoni mwenyewe na akaanza kuwakaanga. Tukio kama la jana likatokea tena na samaki wakageuka mkaa. Sasa mfalme akaona hawa sio samaki wa kawaida. Akaagiza mvuvi aletwe. Alipokuja mvuvi akamweleza nataka unipeleke nikapaone hapo unapovua samaki hawa. Mvuvu akawaeleza ni bali lamda kwa kesho. Mvuvi alijitetea hivi akiogopa ahadi aliyoekeana na jiniBasi siku iliyofata mfalme akatoka na msafara wake kuelekea kule kwenye bwawa. Wakafika mida ya mchana, kwenye bwawa lililozungukwa na milima minne. Watu wote walistaajabu kuona bwawa likiwa milimani na lina maji masafi sana kiasi kile. Kila mmoja alitamani luyaonja maji yale. Ilipofika jioni mfalme akamwagiza mlinda mlango kuwa anatoka lakini asimwambie mtu yeyote. Na atakaemuuliza mwambie amesema hataki kusumbuliwa. Basi mambo yakawa kama hivi.Usiku ule mfalme alitoka na upanga wake akiwa anazunguruka katika eneo lile, alikuwa akisaidiwa na mwanga wa mwezi ulioonekana unawaka sana. Katika kuzunguruka akaona kinjia kidogo kinaelekea upande wa ashariki kutokea kwenye ziwa. Akafata njia ile akakutana na bostani nzuri, yenye maua na matuta mazuri sana. Alistaajabishwa na bostani ile yenye vitu vizuri ambavyo kwenye ufalme wake havipo. Kwa sahuku aliendelea kuchunguza ndani mule kuona maajabu zaidi.Kwa muda mrefu katika kuzunguka kwake alikutana na geti kubwa la rangi ya dhahabu, akaingia kupitia geti hili. Akakutana na njia iliyowekwa taizi za almasi. Alishangazwa na ururi ulioje wa njia hiyo. Mbele yake akakutana na kitu kizuri, kiti hiki kimenakshiwa dhahabu na fedha. Kuangalia vizuri akaona kwenye kiti kiel kuna mtu amekaa. Mtu huyu ni wa ajabu sana, alikuwa ni jiwe kwa chini mapaka kiunono. Kuanzia kiunini mpaka juu ni mtu aliye sawa.Kwa shauku mfalme akataka kujuwa nini kunaendelea eneo lile. Akawa anamuuliza kuhusu yeye ni nani na anafanya nini pale. Na ni kipi kimetokea eneo lile. Maswali yote aliuliza bila ya kujibiwa. Kijana yule alikuwa anatokwa na machozi muda wote ule. Kisha kijana akaanza kuzungumza “hayo maji unayoyaona sio maji, na hao samaki unaowaona ni watu. Hiyo milima ni visiwa na mimi ndiye mfalme wa eneo hili” ni maneno ya kijana aliye jiwe nusu. Mfalme akauliza nini kilitokea sasa. Kijana akaanza kusimulia hadithi ya eneo hili kama ifuatavyo;-HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE.
Baba yangu alikuwa ni mfalme wa eneo hili kwa muda usiopungua miaka hamsini. Alifariki akiwa na umri wa miaka 66, na baada ya kufariki kwake mimi nilichukuwa madaraka hayo. Nchi hii i;likuwa nzuri sana ilozungukwa na visiwa vinne ambavyo ndio milima unayoiona. Nilikuwa na mke wangu ambaye ni binamu yangu. Nilimpenda sana mke wangu na niliamini kuwa naye ananipenda kama ninavyompenda. Tuliishi hivyo kwa muda wa miaka kadhaa bila ya kuona mabadiliko yoyote katika mapenzi yetu.Ilitokea siku moja nilipokuwa nipo kati ya kulala ama kusinzia (mang’amung’amu ya usingizi), vijakazi wawili wa mkewangu wakawa wananipepea. Nikawasikia wanazungumza “namuonea huruma mfalme, anampenda sana mkewe lakini mkewe hampendi, anampenda mtumwa wake.” ni maneno ya mmoja wa wale wajakazi. Mwingine akadakia “yaani anatamani hata amuuwe, na vile anajuwa ucha wipo siku atamuuwa tu”. Wajakazi hawa wakati wanazungumza walidhani nimelala, kumbe nimeyasikia vizuri maneno yao.Siku ilofuata nikaanza kufanya uchunguzi wa maneno yale. Niligunduwa kuwa ni ya ukweli kama walivyosema wale wajakazi. Hivyo nikamchukuwa yule mtumwa na kuanza kumwadhibu. Kwa bahati mbaya wakati wa kumwadhibu alipigwa vibaya na akapoteza fahamu. Yule mke wangu alikasirika sana na akamtibu lakini bia ya mafanikio. Alifanikiwa kumueka hai, yaani anafahamu lakini haweza kufanya chochote. Mwanamke yule kwa hasira alizonzo wakati ule aliondoka kwa muda na nisijuwe wapi alipokwenda.Baada ya muda akarudi, na akachukuwa kifuu cha nazi na akaweka maji, kisha akazungumza naneno ya ajabu akamwaga juu. Visiwa vilivyouzunguka mji huu vikawa milima hiyo unayoiona na mji yakiwemo maduka na vinginevyo ukawa bwawa la maji hayo unayoyaona na watu wakageuzwa kuwa samaki hao wa rangi nne unaowaona yaani hizo rangi za samaki ni aina za watu walokuwepo eneo hili. Baada ya kufanya hayo na mimi akanimwagia maji nikawa kama hivi unavyoniona. Haikuishia hapo kila siku anakuja kunitandika mijeledi ya ngozi ya kifaru. Hunitandia kadri anavyotaka kisha huondoka. Hii ndiyo historia yangu na mji huu.Kijana alimaliza kusimulia hadithi ya nchi yake, mfalme alipatwa na uchungu sana wakati akisikiliza maneno yale. Chozi lilikuwa likimtoka kwa huruma na majonzi. Kish akauliza mahala alipo huyo mwanamke. Kijana akamjibu kwa kumwambia kuwa yeye hajui alipo isipokuwa kila siku jioni baada ya kuniadhibu huenda upande ule (akaelekeza kwa kidole upande wa kusini). Mfalme alikwenda kule alikoelekezwa na kumkuta mtumwa ambaye ni mgonjwa. Akarudi kwa kijana na wakapanga mbinu yako, kisha wakakubaliana watekeleze kesho mpango wao.Basi mambo yakawa kama walivyokubaliana, siku ilofata mfalme akachukuwa upanga wake na akaunoa safi. Akaenda kwenye lile jumba lenye yule mtumwa mgonjwa. Alipofika akamkata upanga na kummalizia uhai wake, kisha akamuingiza kwenye kisima cha maji. Baada ya hapo akajilaza pale kwenye kitanda kama vile yeye ndiye mgonjwa. Yule mwanamke kama kawaida yake alipokuja siku ile akamuadhibu yule kijana kisha akaelekea kule kwenye mgonjwa wake. Alipofika akamwuliza “u hali gani wangu? Vip tafadhali naomba zungumza nami japo neno moja tuu”. Mfalme alojilaza pale kama yeye ndo mgonjwa akamjibu “sina raha kwakweli” “mmmh utamu ulioje leo kusikia sauti yako. Hebu niambie kipi kinachokukosesharaha jama”. Ni maneno ya yule mwanamke. Mfalme alojifanya ndo mgonjwa akajibu “hiyo sauti ya mumeo inanipa taabu, hebu mrudishe katika hali yake ya kawaida na aondoke hapa”. Basi kusikia hivyo yule mwanamke akatoka na kwenda kuchukuwa maji akayasemea maneno flani kisha akamwagia yule kijana na hapohapo akarudi katika umbo lake. Kisha akamwambia uondoke na nisikuone tena eneo hili, sihivyo nitakuuwa.Yule kijana alijifanya anaondoka na akajificha ili ashuhudie kinachoendelea. Basi huku yule mwanamke akaelekea kule moyo wake ulipozama, alipofika akamuliza mtumwa wake “nimesha fanya utakavyo, vipi unajisikia amani sasa ?” yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia hapana, hizo sauti za watu ulowageuza samaki zinanipa shida usiku. Hebu warudishe katika hali yao ya kawaida pamoja na mali zao”. Yule mwanamke akatii an kutoka akazungumza maneno yake ya kichwawi na mji ukabadilika kama ulivyo zamani. Wale watu wa mfalme walokuja kuchunguza samaki walishangaa kujikuta wapo katikati ya mji.Yule mwanamke mchawi akaenda kwa mtumwa wake. Akamuuliza haya sasa bilashaka umeridhika. Yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia “sogea hapa karibu” mwanamke akasogea zaidi yule mfalme akachukua upanga na kumkata vipande viwili. Hna huo ukawa ndo mwisho wa mchawi huyu. Mfalme akatoka na kukutana na kijana. Waliflai sana na kuzungunza mengi zaidi kuhusu eneo lile lenye mali mengi na utajiri wa kutosha.Yule mfalme akamwambia kijana “nimeflai sana, na kwakuwa tupo majirani zaidi tutakuwa ndugu”. Kijana alicheka sana kwa fyraha na mshangao. Kisha akamwambia yule mafalme “kutoka hapa mpaka kufika kwenye utawala wako ni mwendo wa mwaka mmoja. Uliweza kutumia masaa machache kwa sababu eneo hili lilifanyiwa uchawi kama ulivyoona. Basi kijana akamwahidi atamsindikiza wakati wa kurudi mpaka kwake. Mfalme aliflai sana na akamwahidi kumfanya mrithi wa utawala wake kwani yeye hakuwa na mtoto wa kumrithisha.Basi mambo yakawa hivyo, na safari ilikuwa ni nzuri ya ya furaha zaidi. Wafalme hawa walizungumza mengi na kucheka utadhani mtu na mwanae. Walibeba zawadi nyingi na mali nyingi kutoka ufalme ule tajiri. Walipofika walizigawa mali zile kwa viongozi kulingana na vyeo vyao. Mfalme aliitisha mkutano mkubwa sana siku ilofata na akatangaza nia yake ya kutaka kumrithisha ufalme kijana yule na kumfanya kuwa ni mtoto wake. Basi mambo yakawa kama hivyo,Nchi ilikuwa katika hali ya furaha sana kwa muda mrefu. mfalme alikuwa katika furaha kubwa zaidi kwa kupata mtoto na mrithi wa utawala wake. Yule mvuvi ambae ndio chanzo cha yote haya alipewa mali nyingi sana za kuweza kutumia yeye na vizazi vyake vingi vijavyo na akamfanya katika watu wake wa karibu. Kufikia hapa Dinar-zade akamaliza hadithi ya mvuvi. Hadithi hii mpaka kwisha ilichukuwa siku nyingi kwa mfale mpaka akalowea na hadithi. Dinar-zade aliponyeka kuuliwa kama hivi ikawa ikiisha hadithi analeta nyingine. Hivyo akaendelea kusimulia hadithi iliyonzuri kuliko hii ya mvuvi nayo i hii;-HATITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME NA WANAWAKE WA BAGHDADHapo zamani katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na mbeba mizigo maarufu sana. Alikuwa ni kijana asiyepunguwa miaka 40, na alisifika kwa nguvu na akili sana na uwezo wa kufikiri alio nao. Alipendwa sana na watu na aliheshimika pia. Siku moja laikuwa amekaa eneo lake la kila siku kusubiri wateja, ghafla akatokea binti mmoja mrefu wa kiarabu. Binti huyu alimfanya mbeba mizigo amtazame sana kwa muda mrefu kwa uzuri alonao binti huyu. Binti akamwambia yule kijana nifate. Kwa haraka zaidi kijana akanyanyuka na kuanza kufata.Wakafika kwenye nyumba moja yule binti akagonga mlango kwa madaha, mzee mmoja akatoka, binti akatia mkono kwenye mkoba wake na kutoa pesa nyingi na akampa yule mzee. Bila ya kuzungumza mzee alijiwa kinachotakiwa aliingia ndani na akaja na chupa kubwa lililojaa pombe. Kijana akabeba mzigo ule na kuuweka kwenye kapu lake kubwa la kubebea mizigo. Wakaelekea kwenye duka la matunda, hapa wakanunua matunda ya aina nyingi sana. Kisha wakafika duka lingine wakanunua vitu vingi sana vya harufu nzuri. Kwa urembo alonao huyu binti unaweza kufikiri ni vitu gani vya harufu nzuri angechukuwa. Kijana akamwambia “binti bora ungenambia toka mapema kama una mizigo mingi ili nichukuwe punda ama ngamia”. Binti akaheka sana na akamwambia “sijamaliza bado”.Mambo yakawa hivyo waliendelea kununua vitu vingi katika matunda na vyakula na vinywaji. Vitu vya kunukia maua, mafuta pafyumu nna vinginevyo viingi. Wakafika kwenye nyumba mija mzuri sana, yule binti akaenda kuginja kwa madaha na upole zaidi kwenye malngo wa geti la nyumba hivyo. Muda wote kijana alikuwa akifurahia uwepo wa binti huyu na kila analofanya. Basi akatoka binti mwingine wa makamo aliyeonekana mzuri zaidi kuliko huyu na akafungua mlango.Muda wote kijana alikuwa akishangaa na macho yake yaliganda kwa hutu mfungua mlango. Baada ya muda yule binti akamwambia “tafadhali ingia ndani”. Hapa kijana fahamu zikamrejea kwa shauku akaingia ndani. Alishangaa sana uzuri ulioje wa ndani pale. Nyumba yenye kila kizuri anachokijuwa na ambavyo ndo alianza kuviona. Kuna vinyago vya dhahabu na chemchem za maji. Meza yz almasi na sakafu yenye marumaru za kuvutia zaidi.Kila kilichopo ndani hapa kilimflaisha kijana, ila zaidi ya hapo kilichomshangaza zaidi pale ndani kuna kiti kikubwa na zizuri. Aliyekaa kwenye kiti kile alikuwa ni dada mmoja mzuri sana huenda aliwashinda wote pale ndani. Kijana alifikiri yule ndo mkubwa wao, na huu ndo ukweli. Yule aliitwa Zubeida na yule alokuja nae kutoka kwenye bidhaa ni Sadie na yule alofungua mlango aliitwa Amina. Basi amina aliingiza mizigo ndani na sadie alitowa kiasi chapesa na kumpatia kijana.Kijana aliendelea kushangaa pale ndani kwa muda mpaka zubeida akauliza “vipi kaka mbona hauondoki? Au unataka pesa zaidi?”. Kijana akaanza kujitetea kuwa angependa kukaa kidogo na akaleta hadithi nyingi na baadae wakamruhusu aendelee kukaa kidogo. Zubeida akamwabia “basi nitakuruhusu kukaa kwa sharti uwe mpole na usitowe siri ya maisha yetu hapa”. Kiana akakubaliana na sharti na akawajibu “nitatunza siri za humu ndani kuliko alivyotunza siri kinyozi wa mfalme”. Kwa shauku Amina akauliza “alifanya nini kinyozi wa mfalme?”. Kijana akamjibu amina “ni hadithi ndefu kidogo”. Akadakia Sadie “tusimulie basi hiyo hadithi ya kinyozi”. Kijana akamuangalia Zubeida aliyekuwa akimuashiria awaridhishe ndugu yake. Basi kijana akaanza kusimulia hadithi kama ifuatavyo;-HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME.
Hapo zamani za kale katika nchi moja kulikuwepo na mfalme aliyependa kufuga nywele. Mfalme huyu alikuwa akinyowa nywele zake mara nne kwa mwaka. Mfalme huyu alipenda kuvaa kilemba kichwani kama ilivyo kawaida katika tamaduni za kiislamu. Watu wengi walipenda uvaaji wa mfalme wao na yeye alilijuwa hili kwa muda mrefu. Kumbe mfalme alikuwa anasiri kubwa katika uvaaji ule. Mfalme alikuwa akinyolewa na kinyozi maalumu.
Ilipita masiku na miaka mingi hata yule kinyozi wa mfalme akafariki. Ilibidi mfalme atangaze kumtafuta kinyozi mwingine. Uchunguzi ulifanyika kumtafuta kinyozi muadilifu na mwenye maadili. Zaidi ya sifa hizi mfalme alitaka kinyozi mwenye sifa ya kutunza siri. Sifa hii aliitaka mfalme kwa kuwa kuna siri kubwa kwenye kichwa chake. Basi alipatikana kinyozi mmoja kijana mwenye familia ya watoto wanne. Alikuwa ana maadili mazuri na ni muadilifu pia.Ilitokea siku moja mfalme akataka kunyolewa. Akamuita kinyozi wake na kumwambia “kwa mara ya kwanza ndo unakiona kichwa changu, utakachokiona kwenye kichwa changu iwe siri yako mpaka utakapoingia kaburini”. Kinyozi akaapa mbele ya mfalme kuwa katu hataizungumza siri ile kwa yeyote. Kinyozi kufunguwa kilemba cha mfalme alishikwa na mshangao kkubwa baada kuona siri kubwa katika kichwa cha mfalme. Kinyozi akajuwa kumbe hii ndio sababu ya mfalme kuvaa kilemba na kufuga nywele.Basi kinyozi yule alikaa na siri ile kwa siku nyingi sana. Alithubutu hata kukimbia nchi kwa kuogopa kutoa siri ya mfalme. Hali iliendelea kama hivyo anamnyoa kinyozi na anaenelea kutunza siri ya mfalme. Kama ujuavyo siri ikikaa sana kwenye moyo utadhani moyo unataka kutumbuka. Kinyozi akawaza hii siri ya mfalme siwezi kuotoa nitafanya nini sana. “ningejua kama mfalme ana pembe katu nisingekubali kukifunua kichwa cha mfalme”. Ni maneno ya kinyozi.Basi siku moja akatoka na chepe lake na jembe kwenda porini. Kufika kule akachimba shimo kubwa mpaka kiunoni. Baada ya hapo akainama na kuanza kuimba “mfalme anapembe, mfalme anapembe”. Aliimba hivi kwa muda mpaka alipoona moyo wake umetulia na umepoa kwa kuiweka siri ya mfalme kwa muda. Basi baada ya hapo akafukia shimo lake na akaondoka kurudi nyumbani. Haukupita muda mrefu shimo like likaota majani na pakaota mti mkubwa sana.Ni miaka 15 sasa imepita toka mti ule uote sasa mti ule ukabakia na siri ile aloiacha kinyozi miaka 15 iliyopita. Mti ule ulipofikia kutoa maua ukawa upepo ukaja unarudia ule mwimbo wa alouacha kinyozi miaka 15 ilopita. Hivyo ukaja upepo mti unaimba “mfalme ana peembe mfalme anapembe, waaa waaa waaa”. Ikatokea siku moja wawindaji wakapita karibu na mti ule wakastaajabu kusikia wimbo wa ajabu unaozungumza kuwa mfalme ana pembe.Basi habari zikaanza kusambaa kwa kasi sana mpaka ikamfikia kinyozi. Watu wakawa wanafunga safari kwenda kuuangalia mti uanoimba kuwa mfalme ana pembe. Habari zilisambaa mpaka zikamfikia mfalme. Mafalme akatoka na msafara wake nae akashuhudie mti unaotoa siri yake ya pembe kichwani. Alishangaa sana, ilibidi siku ilofata aitishe mkutano mkubwa kwa kila atakaetaka kuhudhuria kwenye eneo lile lenye mti ule.Basi watu walikusanyika sana eneo lile, watoto, wazee na vijana walimwaika eneo lile la tukio. Baada ya muda watu walipokusanyika akasimama na kuanza kuhutubia, kisha akavua kilembe chake watu wote wakashuhudia pembe kichwani mwake. Kisha akasema “nimeamini hakuna siri”. Na huu ndio mwisho wa hadithi ya kinyozi msiri wa mfalme. Basi Amina na Sadie walifurahi sana na wakamruhusu kijana aenelee kubakia pale.Basi pale ndani chakula kikapikwa na watu wakawa wanakula na kunya na kufurahi. Mashairi yaliimbwa na furaha zaidi. Wakatowa pombe wakanywa na wakaendelea kufurahi pale ndani. Nyakati za swala pia ziliwapita palelpale walipokaa. Mapaka wanakuja kutambua ni jioni na kigiza kinakaribia kuingia. Zubeida akamwambia kijana “amka uende zako, muda wa kutengana na wewe umekaribia”. Kijana akaanza kujitetea tena kuwa amelewa sana hivyo hataweza kufika kwake. Kama watamruhusu alale pale mpaka kesho ataondoka na kurudi kwake.KUINGIA KWA WAGENI
Amina na Sadie walimuonea huruma wakamuomba Zubeid amruhusu abakie. Basi Zubeida akamwambia “naongeza sharti lingine kuwa usiulize chochote kwa utakayoyaona yanafanyika hapa ndani”. Kijana kwa mara nyingine anakubaliana na sharti hili. Basi pale ndani furaha iliendelea mpaka waliposikia mlango unagongwa. Sadie akaenda kufungua akakuta kuna watu watatu kwa mavazi yao wanaonekaa ni wageni katika mji ule. Walikuwa wote wanachogo jicho la kulia, na wamenyoa nyusi zao na vichwa vyao ni kipara. Wageni hawa wa kushangaza walikuwa wanamuomba Sadie hifadhi ya kuwaruhusu walale pale kwa leo.Sadie akarudi kwa dada zake kuwaambia kilichopo mlangoni, Zubeida alionekana kutokukubaliana na ugeni huo Sadie akadakia “dada waruhusu walale bila shaka mtawafurahia, maana wanapendeza kweli” kwa shauku Amaina alitaka kujuwa wakoje wageni hao, “wote ni vipara na hawana nyusi upande wa kulia na waote ni chongo jicho la kulia, na wanaonekana ni wageni wa huu mji, bila shaka ni wasafiri” alisema Sadie. Basi Zubeida alijubali kuwaruhusu ila akamsisitiza Sadie awape shari la kukubaliana na kilichoandikwa mlangoni.Wageni wakaingia ndani na bila kusahau Sadie akawaashiria wasome maandishi yaliyopo malangoni “USIULIZE CHOCHOTE KATIKA MAMBO UTAKAYOYAONA HUMU NDANI” wageni walionesha ishara ya kukubaliana na sharti hili. Basi nyumba iliendelea kufurahia, mmoja ya wale wageni akaomba apewe filimbi, na akaanza kupiga na mwenzake mwengine akawa anaimba na mwenzao mwengine akawa anacheza. Wimbi uluwafurahisha sana wakina Amina na Sadie. Zubeida alionekana kupenda zaidi namna ya yule aliyekuwa akicheza.Basi mabo yakawa kama hivyo, furaha ilienea sana ndani mule. Siku hiyo mfalme wa nchi hiyo alikuwa anafanya uchunguzi wake akiwa amefaa nguo za kiraia zinazofanana na wafanyabiashara. Basi walipofika jirani na nyumba ya wakina dada hawa walisikia vifijo na furaha iliyoenea nyumbani pale. Basi kwa shauku kubwa mfalme alitaka kujuwa ni wakinanani hao. Na kwakuwa alifaa mavazi ya wafanya biashara haikuwa rahisi kumtambua. Basi akamuamuru waziri wake akagonge mlango. Waziri akafanya kama alivyoambiwa, na akagonga mlango akatoka Sadie kuja kufungua mlango. Akakuta wafanya biashara watatu waliovaa mavazi mazuri ya kupendeza.Sadie akaingia kwenda kutoa taarifa ndani kwa dada zake, “dada ni wageni watatu wanataka hifadhi, wamekuja nchi hii hawana wanaemfahamu hivyo wanaomba hifadhi ya kulala kwa leo tu” ni maneno ya Sadie akiwaeleza dada zake. Baada ya mashauriano Zubeida akaruhusu wapate hifadhi lakini kwa shart lilelile liloandikwa kwenye mlango wao. Basi Sadie akawakaribisha na kuwapa sharti lile waliopewa wale wageni kwa kwanza. Basi furaha ikarejea pale ndani na vinywaji na vyakula vililiwa na wachezaji na waimbaji wakaendelea. Waziri alikuwa muda wote anadukuduku la kutaka kujuwa kwa nini pale kuna chongo watatu, wote upande wa kulia wamenyoa nyusi na ni vipara. Wakati anataka kuuliza Sadie akadakia “jua mambo yako usiulize kitu usije ukajuta”.Haliiliendelea hivyo mapa Zubeida aliposimama na kuwaambia ndugu zake “HAYA MUDA UMEFIKA TUANZA SASA”. Basi pale Sadie akaanza kusafisha pale ndani na kupangilia kila kitu kwenye sehemu yake. Kisha akawataka wageni wote wakae kwenye viti na pale ndani pabakie pakiwa safi. Kisha sadie akamuomba kijana mbeba mizigo aje amsaidie. Wakaingia ndani na kuja na mbwa wawili wakiwa wamefungwa nyororo katika shingo zao. Zubeida akiwa amekaa kwenye kiti kile kirefu akaagiza aletewe moja kati ya wale mbwa. Basi Sadie bila kuchelewa akampelekea mbwa yule. Zubeida akambusu mbwa yule kisha akasema “je tuanze?”. Hakuhitaji kujibiwa swali lile.
Basi akachukuwa mjeledi akaanza kumchapa mbwa yule kwa muda mrefu mpaka akachoka. Akapunzika kidogo na kuendelea. Alipomaliza akamshika yule mbwa miguu ya mbele na kuanza kumfuta machozi. Akajifuta na yeye pia kisha akambusu kwa mara nyingine. Kisha akaagiza aletewe mbwa mwingine na yule arudishwa, Sadie akatii maagizo. Mbwa wa pili alifanyiwa kama alivyofanyiwa yule wa kwanza.Wakati mambo yote haya yanafanyika, wageni walikuwa wakigusana gusana kwa shauku ya kutaka kujua hasa ni nini kinaendelea. Mfalme aliyejifanya mfanyabiashara akawa anampa maagizo waziri wake kuuliza lakii waziri akajifanya hakusikia. Wakati mambo yanaendelea pale ndaubaida akamuita Amina na kumwambia “njoo Amina ufanye kazi yako”. Muda uleule Amina akaja na vifaa vyake vikaletwa pale na Sadie.kukaletwa filimbi, nguo, kioo na vitu vingine.Basi Amina akawa anaimba mashairi kwa filimbi ile mpaka akapoteza fahamu. Walati huo watu wote wakawa wanashangaa kinachoendelea pale ndani. Basi Sadie akaja na kumpepea dada yake na kumpunguzia mavazi, basi mfalme na wenzie wakaona akovu mengi ya kutisha yaliyopo kwenye mwili wa Amini. Mara hii mfalme alishindwa kujizuia kwa shauku akataka kujuwa ni vitu gani vinafanywa pale ndani, kwa nini mbwa wamepigwa vile na ni kwa nini huyu dada ana makovu makubwa na ya kutisha kwenye mwili wake?. Basi waziri kumridhisha mfalme akamuuliza moja kati ya chongo “hebu tuambieni nyinyi wenzetu mlikuwa hapa ni mambo gani haya tunayo yashuhudia?”. Chongo akawajibu “mmh hata sisi hatuna ujuzi wa kujua mabo haya, sisi pia tumekuja muda si mrefu kabla ya kuja kwenu, lamda tumuulize kijana mbeba mizigo huyu maana tumemkuta. Huenda akawa na habari ya mabo haya”. Majibu ya kijana yakawa yaleyale hatambui kinachofanyika hapa.Basi wakiwa katika hali ya kunong’ona pale ndani ghafla Zubeida akanyanyuka na kuwaambia “mnanini hapo? au mmesahau sharti tuliowapa kabla ya kuingia ndani hapa?”. Kijana akajibu “heti wananiuliza wanataka kujuwa maana ya mabo haya mmnayoyafany ahapa.”. Watu wote pale walikuwa tayari hata kufa lakini wajue maana ya mambo yale. Zubeida akauliza tena “ni kweli anayosema mwenzenu?”. Wote wakaitikia “naam, hasa ni kweli kabisa”. Zubeida akaoka pale kwenye kiti chake akiwa maekasirika sana na kuanza kusema “tumewafadhili hapa na tukawapa sharti moja tu lakini limewashinda. Sasa mnataka kujuwa mabo msiyopasa kuyajuwa.”. Kisha akaita “njooni”Muda uleule wakaja walinzi wa ndani pale na kuwaekea kisu shingoni kwa kila mmoja pale ndani.“sasa wote mtakufa kwenye mikono ya walinzi wangu hawa au kula mmoja anieleze habari yake hata bila ya kudanganya” kusikia maneno haya mfalme akafurahi kwa sababu wakisikia kuwa yeye ni mfalme wasinge muua. Basi Zubeida akamwenea kijana mmemba mizigo na kumwambia “tueleze habari yako bila ya kudanganya na umefika vipi hapa?” kwa sauti ya woga kijana akaanza kuzungumza kuanzi apale asubuhi alipokutana na Sadie maka alipofika pale ndani.Baada ya kwisha kutaja hadithi yake kijana akaruhusiwa aondoe ke muda uleule. Akapiga magoti mbele ya Zubeida na kumwambia “dada naomba ufanye haki kati yetu, wao wamesikiliza hadithi yangu na mimi nataka Kimoyoni alikuwa akiwaza kusikiliza hadithi za hawa vichongo watatu. Basi Zubeida akamwendea moja ya chongo wale na kumwambia ahadithie hadithi yake. Kichonho yule akanza kusema “kwanza jua ewe dada mkubwa wa nyumba hii kuwa sisi unaotuona ni chongo wote ni watoto wa wafalme katika tawala mbalimbali. Kila mmoja anastori yake ya kustaajabisha kuhusu chongo yake. Basi wakaanza kuhadithi stori zao kama ifuatavyo;-HADITHI YA CHONGO WA KWANZA MTOTO WA MFALME
kwanza utambue mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa. Hivyo kwa upekee wangu nilipokea mapenzzi makubwa kutoka kwa baba na mama. Mama yangu alifariki nikiwa mdogo. Hivyo kwa muda mrefu nilibaki na baba yangu. Nilikuwa napenda kuwinda ndege kwa kutumia mishale. Nilikuwa nikitembea na waziri mkuu ninapokwenda kuwinda.Sikumoja tulipokuwa mawindoni nilikuwa nikilenga shabaha shingo ya ndege aliyejificha kwenye kitundu chake. Bila ya kujuwa hili wala lile kumbe waziri alikuwa nyuma ya kile kitundu nae akimvizia yule ndege. Nikarusha mshale wangu na kumpata waziri kwenye jicho. Waziri aligugumia sana kwa maumivu makali yaliopelekea kupata chongo. Nilimuomba msamaha lakini alionesha kutokuridhia na kuamini kuwa nilifanya kwa makusudi.Tulivofika nyumbani nikamueleza baba stori mzima hapo baba akamuita waziri na kutaka kumfariji. Waziri hakutaka chochote na mwisho aliahidi kuwa lazima alipe kisasi kwa yaliyompata. Tulikaa kwa muda mrefu hata nikasahau tukio lile. Nilipata safari ya kwenda kumuona mjomba wangu ambae pia ni mfalme aliyekuwa ni jirani na utawala wa baba. Mjomba huyu nae alinipenda sana. Wakati mwingiune hunambia anaponiona eti namkumbusha marehemu dada yake.Mjomba alikuwa na kijana wake mmoja ambaye ni binamu yangu. Mimi na kaka huyu tulukuwa marafiki sana tulipokuwa wadogo. Hata hivyo urafiki wetu uliendelea hata nilivyokuwa mkubwa. Nilikwenda kwake kumsalimia. Kwakweli alifurahi sana uwepo wangu. Tulizungumza mengi sana na kufurahi pia. Tulipokula chakula cha usiku akanambia “kuna kitu nataka nikuoneshe, nilikuwa ninakiandaa toka ulipoondoka wakati ule”. Basi akachukuwa taa na kuniambia nimfate.Tulikwenda kwa muda wa usiopungua dakika 20 na tukakuta nguzo mbili zilizokaa mfano wa mlango. Tulipofika pale akanambia nifukue pale chini. Bila kuchelewa nikatafuta mijiti na kuanza kuchimba pale. Urefu wa shibri moja nikakuta zege, akanambia “fungua huo ni mlango”. Nikafungua na kukuta ngazi. Tukachuka kwenye ngazi ile na kukutana chini kuna mfano wa mlango ndani ya handaki. Akfungua mlango ule na tukaona nyumba nzauri sana. Akanambia “turudi sasa hiki ndio kitu nilichokuwa naandaa, nakuomba usimwambie mtu jambo hili”.Basi tuliporudi siku ile sikuweza kulala usiku nilikuwa nikiwaza ni la nini jumba lile na ni kwa nini anafanya siri. Niliwaza mengi mpaka nikapitiwa na usingizi. Siku ilofata tuliendelea kufanya mabo ya kawaida mpaka. Baada ya wiki tatu binamu yangu aliniita na kunambia niende nyumbani kwake muda wa usiku. Basi nikaenda na kunambia kuwa “kuna mwanamke atakuja hapa umchukuwe wende nae pale kwa siku ile na mimi nitakuja baadae.Mambo yakawa kama vile haikupita muda yule mwanamke akaja na nikaenda nae mpaka pale. Hatukukaa sana binamu yangu akaja akiwa amebeba mfuko wa sementi na nyumdo na chepe. Bila ya kuzungumza na mtu alipofika pale akaanza kufukuwa mpaka akaikuta ile zege. Akafungua mlangomule na kushuka yeye na yule mwanamke kisha akanambia “ahasante sana nakushukuru wewe rudi na usimueleze yeyote jambo hili”. Basi akaziba ule mlango na mimi nikarejea nyumbani.Nilikaa siku tatu kisha nikarejea kwa baba. Nilipofika kule nilishangaa sana mambo yamebadilika sana. Nilipouliza wakaniambia kuwa baba yangu amepinduliwa na mfalme wa sasa ni waziri mkuu yule niliyemtoboaga jicho lake. Nilishangaa sana na haukupita muda nikakamatwa na kuingizwa mahabusu. Waziri akaja na kunambia sasa umefika muda wake wa kilipiza kisasi. Nilimuomba sana msamaha lakini alikataa.akaamrisha askari wake anichukuwe na akaniuwe na kunitowa jicho moja la kulia.Basi askari yule akanichukuwa mpaka mbali na kunambia “ nikifikiria wema alotufanyia baba yako siwezi kukuuwa lakini naomba uniridhie nikutoe jicho ili kumridhisha mfalme wa sasa na nitamwambia nimesha kuuwa”. Nilikubali nikamuomba niingie porini na kutafuta dawa ya kunifanya nipoteze fahamu. Dawa hii nilifundishwaga na binamu yangu. Yeye alikuwa akiitumia dawa hii anapokuwa na mawazo mengi hivyo hujipoteza fahamu kwa muda.Nilitafuta dawa hivyo kwa muda na nikaipata nikayafikicha majani yake na yalipotowa mai nikayanywa na nikapoteza fahamu muda ulelule na sikujuwa kinacho endelea. Nakuja kuamka nikiwa na maumivu makali sana kichwani na jichoni nikiwa chongo asiye na jicho moja la kulia. Askari akanambia niondoke aneo lile na nisirudi tena nchi ile. Nilirudi kule kwenye utawala wa mjomba wangu.Kufika kwamjomba nae alikuwa katika hali nzito ya kumtafuta mtoto wake. Alifurahi pindi aliponiona maana aliamini nitakuwa na taarifa kuhusu mtoto wake. Aliponambia ni mwezi sasa hajaonekana nilipatwa na hofu, hivyo nikamueleza mjomba kuhusu stori nzima. Usiku ulipoingia nilitoka na mjomba kwa siri na kuelekea kule kwenye ule mjumba wa ardhini. Basi tukaingia palele baada ya kuvunja mlango. Tulipofika kwenye jumba ile tukaingia na tukakuta kuna moshi pale ndani. Tulipopita moshi ule tukamkuta binamu yangu amelala chini akiwa amekauka kama amebanikwa nyama.Kuona hali ile mjomba alilia sana na akanambia tutoke na tumuache palelpale. Tulipofika pale nje akanambia “nilijuwa tu nilipomuaona anakaana mwanamke yule nikajua kuwa atakufa tuu, yule mwanamke ni jini”. Basi akanambia nisimwambie yeyote habari ile. Niliishi na mjomba kwa muda ila alifariki na nikachukuwa madaraka yake.Siku moja nilishangaa kuona ufalme wangu umezungukwa na askari wa ile nchi ya mjomba. Kumbe yule waziri aliyempindua baba amekuja kupindua na utawala wa mjomba wangu. Kwakuwa nchi yangu haijajiandaa kwa vita niliamua kukimbia ilikuepusha vifo vya watu. Niliondoka pale nikawa nalanda mpaka nikafika nchi hii ya baghdad nikanyoa nyusi zangu na nikakutana na wenzangu wawili hawa maka tukafika hapa. Hii ndio stori yangu. Zubeida kusikia maneno yale alifurahi sana kwa stori ile na kumwambia umeokoka. Akamfata chongo wa pili na kumwambia tuambia na wewe stoti yako. Naye akaanza kama ifuatavyo:-HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME.
Kwanza utambuwe kuwa mimi nimekuwa chongo si kwa sababu ya ajali ama bahatimbaya kama iliyompata mwenzangu huyu. Mimi ni kwa sababu ya ujeuri wangu wa kutaka kujuwa mambo yasiyo nihusu. Hadithi yangu ni hii:-Kama nilivyotangulia kusema mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa na baba yangu akanichagulia jina la Agib. Baba yangu alinipa taaluma nyingi sana. Ila kwa upand wangu nilipenda kuwa mfanya biashara. Hivyo nilikuwa nikisafiri kwa kufanya biashara maeneo mengi ya dinia. Tulikuwa tukiuza vitu mabalimbali. Kwa ufupi nilikuwa nimejaaliwa kwa kuwa na nuru ya biashara. Nilikuwa nikiuza sana na kupata faida nzuri.Siku moja tulikuwa tumetoka kibiashara kwa njia ya majini. Nahodha alikuwa mjuzi sana wa safari hizi na safari yetu ilikuwa nzuri sana. Tulifanya biahsra katika visiwa kadhaa na kuelekea upande wa kusini kutoka kisiwa tulichotoka. Upepo ulikuwa mzuri kwa muda wa siku nzima. Hali ilibadilika pale ilipofika asubuhi. Upepo ulikuwa mbaya sana na chombo kilikuwa ninakwenda uelekeo usiojulikana. Nahodha na wenzie walijitahidi kutuwa nanga lakini kamba ilikuwa fupi. Basi wakakiachia chombo kiende tu.Ilipofika asubuhi nyingine tupepo ulitulia na tukaona mbele kuna mlima uliotanda kiza kinene sana. Nahodha alipoulizwa alisema hana ujuzi na eneo hilo lakini anachoweza kusema ni kuwa mlima uliopo mbele yetu ni mlaima wa sumaku hivyo misumari yote iliyopo kwenye chombo chetu itatoka na kuvutwa kwenye mlima. Hivyo nahodha akatutaka kila mmoja ajiandae na ajali hiyo.Mambo yalikuwa hivyo hivyo baada ya muda kadhaa misukari ikaanza kung’oka na kwenda kunata kwenye mlima. Jabir tukaanza kung’ang’ania mbao. Kwa upande wangu mbao nilioipata ilikuwa ni madhubuti hivyo niliogelea naye kwa muda wa siku kadhaa. Mapaka siku ya 5 nikaona kuna kisiwa kidogo. Nikajitahidi nai kufika pale nikaona kuna mti wa mpera nikafika hini pale na kuanza kula mapera.Nilikaa pale kwenye mti ule kwa muda mpaka nikapitiwa na usingizi. Nilipoamka nikaona kuna msafara mkubwa sana unakuja kuelekea pale nilipo. Nikapanda juu ya mpera ule na kujificha pale. Msafara ule ukaja mpaka pembeni kidogo ya mpera ule kwa futi 50 wakachimba chini na kufungua mlango pale chini na msafara wote ukaingia pale. Baada ya muda wa masaa kama matatu walitoka wote kasoro mtu mmoja tu ndiye aliyebaki mule ndani.Walipoondoka nilisubiri kama masaa 2 nikafungua pale na kuingia ndani. Nilipofika nikamkuta kijana wa umri wa miaka 10 ivi. Nikamsalimu na kumuuliza kilichomsibu hata wenzake wakamuacha mulendani. Akaanza kunieleza stori yake kama ifuatavyo;-
HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI
Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii. Kwa sasa nina umri w miaka 15 na baba yangu aliponizaa alinichagulia jina la Agib. Nimewekwa hapa kwenye handaki si kama nimetelekezwa hapana. Hii ni njia pekee iliyoonekana kuwa nitakuwa salama. Bla shaka unataka kujuwa hasa nini kilinitokea, mambo yalikuwa hivi;-Baba yangu kabla hajanizaa kwa muda wa mwaka mmoja alipata ndoto ya ajabu sana. Aliwatafuta watu maarufu na wenye elimu ya kutambuwa maana za ndoto na wakamwambia kuwa mke wake yaani mama yangu atapata ujauzito wa mtoto wa kiume. Na mtoto huyo ataishi kwa furaha na amani kwa muda wa miaka 15. na kama akifika miaka 15 bila ya kitu chochote kumpata Jabir mwana wa mfalme katika mlima wa sumaku, mtoto huy ataishi salama mpaka uzeeni. Vinginevyo kama akifika miaka 15 na mwana wa mfalme Jabir akipatwa na ajali katika mlima wa sumaku basi uhesabu siku 40 tu za umri wa mtto wako zitakazokuwa zimebaki toka utakapopata hiz habari.Hivyo mambo yakawa kama hivyo mimi nikazaliwa na mpaka sasa nina miak 15 sijawahi kuumwa wala kupata majonzi makubwa. Lakini ni siku 5 zilizopita baba alipata habari kuwa Mlima wa sumaku umesababisha ajali ya watu na huenda huyo Jabir mwana wa malme akawemo humo. Hivyo baba akaamuwa kunificha huku ili nisiweze kukutana na jabir. Kwa sasa nina matumaini kidogo lakini huwezijua hatima ya mwanadamu. Hii ndio stori yangu ewe ndugu yangu.Basi niliposikia stori ya kijana yule nilipatwa na majnzi kuona kumbe ni mimi nitakayemuuwa. Sikuamini mawazo haya na kikaapa kuakaa pale ili nimlinde huenda akawa ni mtu mwingine atakayekuja kumuuwa. Basi niliaua kumdanganya jina langu na kumwambia naitwa Habir ni mvuvi niliyepatwa na ajali majini. Nikampatia mapera niliyochuma kule nje na aliyependa sana. Basi nikamwambia nitaishi na wewe hapa na nitakulinda na huyo anayetarajiwa Jabir kama akija.Kijana alikubali na alifurahi pia, kwani alitaka hata apate mtu wa kuweza kuzungumza naye pale ndani, maana wazazi wake walimuahidi kuwa watakuja siku ya 40. basi mimi nikawa ndiye mfanyaji kazi pale ndani, napika na kufanya mambo kmengine kama kutandika kitanda na kufagia. Kwakweli tuliishi kwa furaha sana wawili sisi pale ndani. Nilikuwa nikijaribu kumfurahisha kila wakati kwa namna yoyote ile.Basi mabo yakawa kama hivyo, tuliishi kwa upendo na furaha kubwa kwa muda wa siku 39 zote pale handakini. Siku ya 40 hatimaye ikafika na kila mmoja katika sisi alifikiri mambo yale yamekwisha hivyo kijana yupo salama. Siku hii kijana alivaa nguo zake nzuri na niliandaa chakula kizuri sana. Ilifika muda wa wa kukaribia mchana kijana akaend kualala. Basi mimi nikaendelea kuandaa chakula na vinywaji. Lakini nilipotaka kumenya matunda sikukiona kisu.Nikaenda kukitafuta kisu nimenye matunda bila ya mafanikio. Ghafla nikakumbuka kuwa kijana alikuwa akimenyea embe jana kitandani kwake. Basi nikaelekea kwenda kukichukua kisu. Nikakikuta amekitundika kwenye mjiti wa kitanda kunapochomekewa pazia la kitanda. Basi kwa utaratibu nikapanda pale kwenye kitanda bila ya kumuamsha na nikawa nakichomoa. Kwakuwa mikono yangu ilikuwa ikiteleza kisu kiliniponyoka na kufikia kwenye kifua cha kijana na kuumaliza uhai wake kupitia moyo.Nilipatwa na woga sana, sikiamini9 kama mimi niliyetaka kumlinda ndiye nimemuua. Nililia sana, ila ghafla nikakumbuka leo wazazi wake watakuja hivyo nikatoka pale ndani kwa haraka. Nilipomaliza tu kutoka nje na kuukaribia mpera nikaona kundila watu linakuja. Basi kwa woga wangu nikaificha pale kwenye mpera.Wale watu wakaingia ndani mule na kwa muda usiopungua masaa 3 wakatoka na mwili wa kijana huku wengine wanalia sana. Wakauzika mwili ule pale pembeni na kisha wakaondoka. Nilikaa pale kwa muda mrefu hata ilipokaribia jioni nikatoka pale na kutembea tembea katika eneo lile. Nikakuta kanhia kanakoelekea milimani nikakafuata. Huko nikakutana na watu 10 wote ni machongo wa jicho la kulia.Watu wale nikawaelezea kuwa mimi nimepata ajali baharini na sina ninaemjua eneo hili hivyo nikawaomba wanihifadhi. Ijapokuwa kati yao baadhi walikuwa wakikataa lakini mkubwa wao akazungumza “tutakukubalia kukaa nasi ila kwa sharti moja naloni KUTOKUULIZA CHOCHOTE KATIKA MAMBO YATAKAYOFANYIKA USIKU”. kuna mwengine akaongezea kwa kusema “na sharti hili ni kwa ajili ya usalama wako tu” basi nikatoa ishara ya kukubaliana na sharti lile.Kwahakika niliishi bila ya shaka nyumbani kwao wale machongo. Lakini jambo moja tu lilikuwa likinisumbua ni kuwa kila ifikapo usiku wanachukuwa mijeledi na kuanza kujitandika mgongoni viboko 100. nilikaa hivi bila ya kuuliza kwa muda wa siku kadhaa. Siku moja nikaamuwa kuwauliza na lolote litakalotokea na litokee ila lazima nijuwe ni kwa nini wanajitandika mikwaju ile na ni kwa nini wote ni machongo wa jicho la kulia?.Basi mambo yakawa kama hivi, siku ile mchana nikawauliza maswali yale mawili. Basi walishangaa sana kuona ninakiuka masharti ya kuishi ndani pale. Mkubwa wao akanieleza “kijana sharti hili tuliweka kwa ajili ya usalama wako, lakini sasa inaonekana hata haujali nini kitakupata”. kaka mimi naomba kupata majibu ya maswali haya na sijali kwa lolote litakalonipata. Akanijibu “sisi hatutakueleza chochote katika hayo ila utajionea mwenyewe, kama ukotayari tutafanya maandalizi kesho” nikamjibu kuwa nipo tayari.Basi siku ile ilofata asubuhi wakamchinja kondoo nakuniambia “tutakushonea kwenye ngozi ya kondoo huyu na tutakupa kisu. Tuatkuweka juu ya mlima na hapo atakuja roki (ndege) atakubeba akidhani ni kondoo. Pindi akikutuwa tumia kisu na uchane ngozi yeye atakimbia. Utakapotoka upande wa mashariki ya mlima kwa chini utaona njia ndogo. Ifate njia hiyo na utakuba nymba. Humo usimuulize mtu yeyote juu ya mambo haya. Ukifanikiwa kurudi hapa ndani ya sikua 100 na ukawa haukupata majibu ya maswali yako nitakujibu mwenyewe”.SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI.
Basi mambo yaka wa hivyohivyo, siku ile wakaniweka kwenye ngozi ya kondoo na kubebwa na roki. Alikwenda kunituwa juu ya mlima na nikatumia kisu na kutoka yule ndege akakimbia. Nikafata ile njia niloambiwa mpaka nikakuta nyumba kubwa sana. Kwa hakika nyumba ilikuwa ni nzuri sana na ni kubwa. Ilikuwa ina vyumba zaidi ya 100. ilikuwa ina vitu vingi vya kuvutia na mabostani ya matunda na miti.Nyumba hii ilikuwa imetulia sana yaani utadahani haina hata mtu mmoja japo utashangazwa kwa usafi wa nyumba hii. Nilianza kuhesabu vymba mpaka nikafika chumba cha 35, na humo nikasikia sauti za wanawake. Nilibisha hodi na kukaribishwa kwa furaha. Nilipewa chakula na malazi, vinywaji na furaha nyingine.Nilikaa pale kwa muda wa siku 5 nikiwa ninabadilishiwa furaha mpa ya mambo mapya kila siku. Huenda hata ningeishi siku 1000 ningepata mabo mapya kila siku. Kwa hakika nyumba hii ilikuwa na kila kitu nilichokisikia na kila uzuri. Niliendelea kukaa pale hata ilipofika mwezi 3 kambla ya kumalizika kwa mwaka kwa siku 10.Siku ile wale wanawake wakaniita na mkubwa wao akaanza kuongea “mgeni wetu, tunapenda sana kuishi na wewe hapa kuwa muda zaidi lakini hatunabudi ya kutengana kwa muda wa sili 100. sisi ni watoto wa wafalme na huwa kila mwisho wa mwaka tunarudi makwetu kwa ajili ya mabo ya kifamilia. Hivyo hatunabudi kutengana nawe ila tutakuacha hapa. Tunakuachia funguo hizi za vyumba 100 humo utafutahia vitu ambavyo hujapata kuviona kwa muda wote uloishi hapa. Ila vyumba vyote fungua isipokuwa cha 100. kama tutakutana baada ya siki hizo tutafurahi sana na tusipokutana usisahau kutuombea dua.”Kwa majonzi niliagana nao sikuile na wakaondoka. Basi nikaanza kufurahia mambo mazuri yaliyomo pale ndani. Nikawa kwa kialsiku Snafunguwa chumba kimoja. Ikawa kila chumba nikuta mambo mazuri ambayo chumba nilichofungua jana hakina. Kwahakika nilifurahia sana harufu nzuri ya mawaidi mule ndani. Sauti nzuri za kupendeza za ndege, chemchem za maji na asali iliyohifadhiwa. Vyakula vya kila namna na vikalio vya kuvutia.Nilifanya hivyo mapaka pale nilipomaliza vyote vyumba 99 kwa siku 99 na kubakia chumba kimoja na siki moja mpaka kurudi wale wenyeji wangu. Sikuile ya 100 ilipofika nikawa sina hamu ya kurudia vyumba vya nyuma hivyo nikataka kufungua kile cha 100. nikaenda kwenye mlango na kuanza kupiga mahesabu ya kufungua. Nilianza kuoiga ramli ya vigole kwa kufumba macho lakni matokea yakawa nisifungue, basi nikaamua niondoke pale mlangoni.Nilizunguruka mule ndani na nikajikuta narudi tena chumba cha 100. mara hii nilikuja na jani nikawa napiga ramli ya majani lakini matokeo yaka wa nisifungue. Dukuduku lilianza kuniumiza kwa nini chumba cha 100. mna nini hasa humu mpaka nisifungue. Basi nikaichukua ile funguo na kufungua kidogo ili nichingulie. Nilipofungua ghafla ilikuja harufu nzuri ya ajabu na hapohapo nikapoteza fahamu.Nilipokuja kuzindukka nikafungua ili nijue kuna nini na ni wapi harupu ile ya kuvutia ilipotokea. Basi nilipofungua tu nikajikuta nipo nje, kumbe kile hakikuwa ni chumbaila ni mlango wa kutokea kwenye bostani. Nilipofika mule nikaona kuna ndege wanaoimba nyinyo nzuri, matunda ambayo sijayaona na mauwa yanayotoa harufu njema ya kuvutia. Maji ya chemchem yenye rangi ya dhahabu na ni ya moto. Halikadhalika vivuli vyenye mumboKwa hakika katika bostani lile kulikuwa na mabo mengi na ya kuvutia sana. Cha ajabu zaidi niliona kuna farasi mwenye mabawa na mkia mrefu wa kuvutia wenye mashapupo yanayofanana na miba ya nungunungu. Nilitamani sana kumpanda farasi yule. Nilimsogelea na kutafuta fimbo ya kumuendeshea na nikaiona. Polepoe nikampanda na kuanza kumuendesa mrembo farasi.Farasi yule ghafla akaanza kupaa hata kabla sijakua namna ya kumpaisha, alipofika umbali kadhaa akaanza kunifiga na mashaputo ya mkia wake ulio mrefu. Mashaputo yale yakanipata kwenye jicho langu la kulia na kunitoboa. Nilianguka chini ghafla na kupoteza fahamu. Nilipokuja kushitua nikajikuta nipo karibu na mlima na lile jumba sikuliona tena na hata ile njia sikuiona tena.Basi nikarudi kwa wale wenzangu machongo tukawa tupo chongo11. wale wakanambia siwezi tena kukaa na wao maana wamesha enea. Hivyo yule mkubwa wao akanimalizia majibua ya maswali yangu kuwa sababu ya wao kujitandika na mikwaju ni adhabu ya kuvunja amri ya kutoufungua mlango wa 100. hivyo wakaniambia niende baghadi huko nitakutana nae ali anipangie adhabu yangu.Baada ya hapo nikanyoa nyusi zangu na nywele zangu na kuelekea baghdad na nilipofika hapa nikakutana na wenzangu hawa watatu na usiku ulipotufikia tuakaamua kuomba hifadha hapa kwenu. Hivyo hii ndio stori yangu ewe dada Zubeida.Zubeida alipomaliza kusikiliza stori ya chongo huyu akamuelekea chongowa tatu na kumwambia aeleze stori yake bila ya kuficha kitu na vinginevyo atakufa. Chongo wa tatu akaanza kuelezea kuwa na yeye ni mtotowa mfalme na amepata chongo si kwa sababu ya ubishi wake bali ni qadar tu na hivi ndibyo mambo yalivyokuwa;-HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME
Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama. Nilipewa taaluma nyingi na wazazi wangu na nilifahamu vizuri. Nilifundishwa sayansi, maarifa ya mazingira, simulizi na biashara. Kwa upande wangu nilipenda sana uandishi na nilikuwa na muandiko mzuri sana hata niliwashinda waandishi wote nilowahi kukutana nao. Uzuri wa muandiko wangu ulifika mbali sana hata nikawa ninaa ndika barua zote za mfalme kwenye nchi za majirani.Ilitokea sikumoja nikaandika barua iliyotakiwa kuenda nchi za hindi kwa mfalme wa wahindi. Niliandika barua ile kwa ufndi wa hali ya juu na ikatumwa kwa mfalme wa hindi. Taarifa zikatujia baada ya miezi kadhaa kuwa mfalme wa wahidi amestaajabishwa sana na uzuri wa mwandiko wa barua ile hivyo akataka amuone mwandishi huyo na alitowa zawadi nyingi kwa mfalme wa nchi yetu yaani baba yangu ili aniruhusu niende uhindini akanione.Baba alifurahihwa sana n barua ile na mimi pia nilifurahi japo nilisita kuenda hindi. Kwa zawadi alizopokea baba aliniomba niende na kuniambia huenda nikajifunza mambo mengi ambayo pale nchini kwetu hakuna. Baba alichagua walinzi wazur kwa ajili ya kuulinda msafara wetu kwani safari ilikuwa ni ndefu na yenye ugumu pia.Basi ilibidi nikubaliane na mawazo ya baba ya kwenda nchi ya wahindi chini ya ombila mfalme wa watu nwa hindi. Baada ya siku 10 safari ilianza kuelekea uhindini. Safari ilikuwa nchema na yenye amani. Tuliweza kupita kwenye majangwa na misitu. Tulivuka mito na mabwawa ya kuvutia na kupendeza. Nilifurahishwa na safari na kujiahidi mwenyewe kuwa kwa hakika nitajifunza mengi huku niendko.Tulitembea bila ya dharuba kwa siku 15 na tulilala siku hiyo katika eneo la jangwa lenye mlima wa michana na vichuguu vya hap na pale. Bila ya kujua lolte kumbe kulikuwa na wavamizi wanatuchunguza. Asubuhi ya siku ilofata tuliondoka pale na tukapita kwenye ponde lililochimbika. Wale wavamizi walikaa juu ya bonde na kutuacha sisis tunapita chini yake. Ghafla wakaanza kutushambulia na wengi katika sisi wakapoteza maisha. Kila mtu akaanza kukimbia upande wake kuokoa maisha yake.Kwa upande wangu sikuona hata askari aliyekuwa akinikinga. Basi nikavua yale mavazi ya watoto wa wafalme na kuwatupia wavamizi na nikaanza kukimbia. Hii ilikuwa ni salama yangu kwani mavazi yale yana thamani kubwa hivyo wasingethubutu kuniachia. Nilikimbia bila ya kujua ninakoelekea mpaka niliposilkia sauti ya jogoo akiwika. Kwa mbali nikasikia sauti ya pungu hapo nikajuwa kumbe ilikuwa ni saa saba sasa.Nilielekea kule niliposikia sauti zile na kukutana na mzee mmoja na kumuelezea tukio lote. Mzee huyu akakybali kunipa msaada wa kuishi pale kkwake. Nikaishi pale kwa muda wa siku tatu kwa yule mzee nikila na kuoga bila ya tatizo lolote. Siku ya nne yule mzee akaniuliza. “mwanangu, unaishi hapa ila inabidi ujifundishe kuishi mwenyewe bila ya kunitegemea. Vip kwani mwanangu una ujuzi gani wewe?”. nikamjibu “mimi nimeishi maisha ya kifalme kama nilivyokwambia baba yangu ni mfalme hivyo maisha niloishi ni ya kisomi. Taaluma nilonayo ni masimulizi na uandishi”.Yule mzee aliposikia maneno yangu akaguna kidogo kisha akasema “mwanangu, kwa ujuzi ulonao hapa ni vigumu kuweza kujitgemea. Hivyo nakushauri uanze biashara ya kukata kuni. Nitakuandalia zana na nitakufundisha pia. Kwa hakika ni kazi njema na ni ya rahisi katika eneo hili”. Basi siku ilofata yule mzee akanikabidhi shoka na panga pamoja na kata ya kubebea mizigo ya kuni.Basi mzee alinichukuwa kuelekea msituni ambapo akanifundisha kazi ile na unielekeza mambo yahusuyo. Tulikata kuni siku ile na tukarudi na mizigo kila mtu na wa kwake. Mzee akanipeleka sokoni na kunelekeza matajiri wa kununua kuni zile. Siku ilofata nikaenda peke yangu, kwa kweli mwanzo kazi niliiona ngumu sana ila baada ya siku kadhaa nikaanza kuzoea.Nilianza kuishi bila a kumtegemea mzee wangu yule, kwa hakika alinizoea sana na alinifanya kama mwanae. Alikuwa nabinti yake aliye mdogo alikuwa kila siku akiniambia pindi akikuwa ataniozesha. Ingawa sikua na matumaini hayo lakini nilikubwa kwa kuataka kumridhisha mzee yule. Hivyo nikawa ninatoka asubuhi kuelekea kazina na mida ya mchana ninarudi kwa ajili ya kutegea soko la mchana na wale anaotaka kupika usiku.Sasa nimesha zoea kazi hata mzee aliweza kuniachia familia yake niweze kihudumia pindi alipopata safari za dharura. Ni mieze miwili na siku nane sasa toka nikutane na mzee huyu. Nilimuheshimu sana na alinipenda pia. Kwakweli heshima inapelekea kupendwa na watu. Mambo yalikuwa kama hivyo, ila siku moja kila kitu kiliharibika. Kwa hakika sikuweza kuisahau siku hii hata mara moja.Ilitokea siku moja nilikwenda kukatakuni asubuhi sana na mapema. Siku hii nilikwenda mbali sana tofauti na sikuzote. Nilipokuwa ninachanja kuni ghafla nikasikia sauti kama vile shoka imepiga chini ambapo kuna shimo. Nikaacha kuchanja kuni na kuanza kufukua pale chini na nilishangaa kuona kuna mfunikowa zege. Pale nikaanza kuchimba ule mfunika hata nikaufungua na kukuta kuna ngazi ya kushuka chini. Kwa umakini nikaikamata ngazi ile na kuanzakushuka nayo kule chini na kukuta kuna jumba moja kubwa sana.Nilistaajabu kuona jumba kule chini. Kwa udadisi zaidi nikataka kujua kuna nini hasa. Ikaelekea mlango mkuu wa jumba lile na kugonga mlango na kufunguliwa na wafanyakazi wa kike. Wakanipeleka mpaka kwa mkubwa wao. Kumbe jumba lile lina wananwake watupu na mkubwa wao ni mwananoke ambaye ni mtoto wa mfalme. Nilipomuona tu nilistaajabu kwa ururi ambao ameumbiwa. Kwa hakika ni mzuri na anaonekana katika mavazi ya heshima zaidi.Nikamsalimia kwa upole na kurudisha salamu. Baada ya salamu nikajitambulisha kwa jna la Hamid mchanja kuni wa kijiji, binti alitabasamu na kuniacha mdomo wazi kwa mshangao.nilimuuliza kipi kimemsibu na yeye ni nani hasa. Akaanza kunielezea habari yake kama ifuatavyo;-HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME.
Juwa ewe mwenye kuja kwa jina la Habili kwa cheo cha mchanja kuni kuwa mimi ni mtoto wa mfalme niliyetambulika kwa uzuri na hta mawaziri na watoto wa wafalme wakawa wanagombana kwa kutaka kunipata kuwa mke wao. Ugovi huu ulikuwa mkali hata ukaingiliwa na viumbe visivyo onekana navyo vikataka kunioa nao ni maini waliombali na rehema za Mwenyezi mungu.Nyumbani kwetu kulikuwana kisima kilichoaminika kuwa ni cha muda mrefu kisichopungua umri wa miaka 150. katika kisima hiki kijana wa kijini alichikuwa madaraka ya kutawala majini waliopo kwenye kisima kile. Siku ile nilikwenda kuchota maji kisimani pale nikiwa kichwa changu kipo wazi kinyume na maamrisho ya dini yetu. Bila ya kutambua unywele wangu mmoja uliangukia kwenyekisima kile na kumganda kiongozi mpya a majini alipokuwa akipewa majukumu.Nilirudi nikiwa na mabadiliko katika kichwa changu hata ndoo ya maji niliiona n nzito sana kuibeba hivyo nikatumia mikono yangu kubeba maji yale. Siku ile sikupata usingizi kwa maumivu ya kichwa na nilipopata usingizi nilshituka kwa ndoto za kutisha nilizokuwa ninazipata. Sikujuwa chanzo cha matatizo haya yote. Ilipofika asubuhi nilimueleza baba yangu ju ya maumivu ya kichwa changu. Baba alimwita daktari wetu na kuanza kunitibia. Kwa muda wa siku 5 sikupata nafuu zaidi ya maradhi yaliyokuwa yakinizidia.Kwa muda wa miezi waganga na madaktari wote walishindwa kutibu ugonjwa wangu. Ilifikia hali kuwa mbaya hata nikawa sinafahamu juu ya niayofanya, unaweza kusema nilikuwa mkichaa ambaye akili zinaingia na kutoka. Hali hii ilimpa baba yangu wakati mgumu hata akafikiri ni maradhi yaliyosababishwa na wale wachumba wliokuwa wakinigombania. Habari za ugonjwa wangu zilienea nchi nzima na kila mtaalamu wa tiba alikuja kujaribu bahati yake kwani donge nono liliahidiwa kwa atakayenitibu.Miezi sita ilifika na habari za ugonjwa wangu zikaenea nchi za majirani. Baba alifikia hatua akatangaza kwa yeyote aatakayenitibu ataniozesha nae. Jambo hili lilisababisha hata wataalamu wa ta kutoka nchi za jirani wa lengo la kunioa pindi wakifanikiwa kunitibu. Bila ya mafanikio yeyote juu ya ugonjwa wangu ijapokuwa wapo walofaniukiwa kunipa nafuu lakini haichukui muda kabla ya ugonjwa kunizidia.Siku niliota ndoto ya kushangaza. Ndoto hii nilipomwambia baba alijaribu kuwauliza wataalamu wenye kujuwa tafsiri za ndoto. Basi akaja mtaalamu na akaniambia nimueleze ndoto ile bila hata ya kuacha hata sehemu ndogo. Basi nilikaa kimya kwa muda kisha nikakusanya mawazo yangu na kuanza kumuelezea ndoto yangu kama ifuatavyo;-NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME.
Nilipokuwa nimelala nilioa kana kwamba nipo katikati ya kundi kubwa la watu na wote ni wanume. Wote walikuwa wanagombania kuushika mkono wangu. Ila walishindwa kuupata kwa sababu nilipokuwa nipo nilizungukiwa na miba hivyo walishindwa kupita. Watu hawa walionekan kuminyana na miba ile bila mafanikio hata wakaanza kugombana na kulaumiana juu ya nani ameweka miba ile.Wakiwa katika hali hiyo ghafla upepo mkubwa ulivuma ukiambatana na vumbi kubwa. Miti iliinama kwa upepo ule na wale watu wote wakatulia kwanza. Katika hali hiyo alitokea kijana mmoja mzuri aliyevaa mavazi meupe yenye kuvyovywa kwenye dahabu nyekundwu. Kwa hakika alinivutia sana. Kisha akawaambia wale watu kuwa wasigombane yeye ndiye aliyeweka ile miba, na hivyo hakuna hata mmoja ataweza kuivuka miba ile ila mpaka aitoe.Mmoja kati ya wale watu akamuuliza ni kwa sababu gani ameamua kuweka miba ile. Akawajibu kuwa “kwa muda mrefu pacha wangu amekuwa akiulinda mkono wa huyu binti dhidi ya wabaya na mabaya. Lakini si muda mrefu amepoteza maisha kwa sababu ya huyu binti. Wale watu wakaanza kupiga makelele na kumwambia kuwa yeye ni muongo. Vipi itawezekana huyu binti asiyejuwa hata kushika silaha akamuuwa pacha wako. Kwakweli hatujasikia jambo kama hili.Akawajibu kuwa huyu binti siku moja alipokuwa anachota maji kisimani sehemu ya mwili wake ilidondokea kisimani na kumkuta pacha wangu akiwa katika hali ya kupewa majikumu hivyo muda ule hakuwa na nguvu yoyote ya kujikinga. Hivyo aliungua mwili wake kwa sababu hiyo akapoteza maisha baada ya siku 9 toka tukio lile. Hivyo nikaweka miba hii na kuapa kuwa hakuna yeyote atakayeipita miba hii na kukuta mkono wa binti huyu muuaji wa pacha wangu.Mtu mwingine kati ya wale watu akauliza “vipi sasa miba hii utaitowa lini, au ni lini utaweza kuushika mkono wake na kumtoa kizuizini”. akajibu kuwa mpaka sasa huyu binti alikuwa kwenye adhabu ya kumuua pacha wangu lakini kwa sasa adhabu imekwisha hivyo nitamtowa kwenye kizuizi hiki mbele ya macho yenu. Basi pale pale akazungumza maneno fulani kisha miba yote ikaondoka. Nilipokuwa nikitoka yule kijana akanishika mkono na kunitowa pale. Ila kabla ya kuondoka eneo lile ghafla akachomwa na mkuki na kufariki palepale.Jambo hili liliwashangaza wale watu wengine na wakaanza kujiuliza nani amemuuwa. Mtu mmoja mwenye sura mbaya akatokea akiwa amepanda punda mweusi. Akazungumza kumwambia yul kijana “nilikuwa nakusubiri tu umtoe ili nimchukue mimi, wewe ni kijana mdogo lakini ulinishinda wa miba yako hii kwa hakika nilishindwa kupita ila sasa hakina wa kunizuia” basi palepale akanichukuwa na kunipeleka chini ya ardhi iliyopo nchi nisiyoijua. Ghafla nikasikia maumivu kwenye mgongo wangu na nikashituka kuoka usingizini. Hii ndiyo ndoto niliyoiota ewe mjuzi na muelewa wa hadithi za usiku.Katika kuitafasiri ndoto ile akasema kuwa “umekuwa ukiposwa na watu wengi lakini hakuna alokubaliwa mpaka sasa, hii ni kutokana na jini aliyekuwa amekfunga usiolewe akisubiri apewe madaraka kwenye utawala wao ili akuchukuwe na akufanye mke wake. Jini huyu alikuwekea ulinzi mkubwa dhidi ya maradhi na wachawi katu usingeweza kudhuriwa hata. Alikuwekea kinga iliyofanana na kunga yake. Bila shaka ulipokwenda kuchota maji sehemu ya mwili wako iliyomdondokea ni nywele zako. Na kwa kuwa alikuwa akipokea amri hakuweza kudhibiti usito w nywele yako iliyojaa nguvu iliyotokana na kinga zake. Hivyo alipatwa na matatizo kama ndoto inavyo elezwa.Utawala huu wa majini upo chini ya kisima hicho ulichokwenda kuchotea maji. Majini hawa walikuwa mapacha hivyo moacha wake kama ndoto zinavyoonesha kwa hasira na majonzi akakupa haya maradhi kama adhabu. Na bila shaka atakuja mwenyewe kukutibu kama ndoto inavyosema. Halikadalika pacha huyu unamfahamu na ulishawahi kukutana nae na anakupenda pia hivyo hataweza kukuua.Ila pindi atakapo kutibu tukio kubwa litampata litakalopelekea mauti yake na kwa upande wako pia hautakuwa salama kama ulivyoona kwenye ndoto. Alivyomaliza kusema hayo akamwambia baba kuwa hii ni tafasiri ya ndoto ya binti yako ewe mtukufu mafalme. Basi baba aliingiwa na majonzi kwa tafasiri ile ila hakuwa na jinsi. Kwa hakika nilikumbuka kuwa nilipokuwa mdogo sura ile niloiona kwenye ndoto niliiona. Niliona mtoto anazunguruka kwenye kisima na nili[omfuata akasema amepotea.Basi siku ya ilofuata asubuhi akaja mganga mmoja na akasema anaweza kunitibu, lakini akataka mfalme aweke ahadi juu ya kumuozesha pindi atakaponitibu. Baba alikubali, basi nilipomuona tu nilimjuwa kuwa ni yule nilomuona kwenye ndoto. Kwa hakika alikuwa ni kijana mtanashati na ni mzuri pia, nilikubaliana na wazo la baba la kuniozesha kama ataitibu. Ila sikuweza kumueleza baba kuwa huyu mdiye yule nilomuona wenye ndoto kwa kuhofia kuvunja ahadi ya kuniozesha kuokana na tafsiri ya ile ndoto.Basi ilichukua nywele kumbe ni ile nywele yangu na kuichoma na kuniambia nijifunike shuka ili mosho wote wa ile nywele unipate mimi. Basi haukupita muda nilipiga ukelele mkali sana hata baba alishangaa, kisima kiliporomoka madongo na maji yalijaa kwenye kisima, kuku walitawanyuka na punda wakawa wanapiga kelele ovyoovyo. Nilipoteza fahamu na nisijue kilichofata baada ya hapo. Nilipokuja kuzinduka mikajikuta nimepona kabisa. Basi ahadi ikaendelea na nikaolewa na yule kijana.Tuliishi pale nyumbani kwa raha kwa muda wa siku tatu. Siku ya nne asubuhi nyoka mkubwa alitoka kisimani mchana na watu walimshuhudia a kuja ndani akamuua mume wangu na kunimeza mimi. Sikujua nini kiliendelea kuhusu mwili wa mume wangu au nini kiliendelea baada ya pale. Nilikujakushituka siku tatu baadae na kujikuta nipo humu ndani. Huyu jini ameniweka humu na amenifanya mkewe na anakuja kila baada ya siku 40. ila nikiwa na shida nae au nikipata matatizi huwa nabonyeza hii pete ya mkufu na hapohapo atakuja. Hii ndio stori yangu ewe Habil makata kuni.Basi niliposikia habari hii nilistajabu sana na kuona kumbe kuna watu wamepta makubwa kuliko hata mimi. Basi na mimi nikamueleza stori yangu hata nikafika pale. Basi tulikunywa na kufurahia pae ndani. Nilikunywa pombe na nilipokuwa nimelewa nikaivuta ile pete ya mkufu na kuanguka chin. Yule binti alipiga kelele na kusema umeniua na maisha yako yapo hatarini pia. Toka nje na ukimbie.Basi muda uleule pale ndani pakawa na kiza kinene nikajitahidi kutoka nje na kiakumbuka kuwa nimesahau kiatu kimoja ndani. Sikujuwa kilichoendelea huko ndani ila nilipofika nyumbani niliishia kitandani. Haikupita muda ilifika mchana na akaja mtu mmoja kutaka kuni. Nilipotka moyo wangu ulitetemeka kwani sikupata kumjua mtu yule akaniuliza “asubuhi ya leo ulikuwa wapi” nikamjibu nilikuwa hapahapa leo sijatoka. Akanionesha kiatu changu akasema “hiki sio chakwako?” nilionekana kubabaika basi akapiga guu lake chini na hapo hapo upepo mkali ukanibeba.Alinituwa ufukweni mbele ya yule binti na kumuuliza kama ananijua. Yule binti akakana na kusema kuwa hanijui na mimi pia nikakana kusema kuwa namjua. Basi jini yule akamchinja ule mwanamke na kunuiambia “sasa ni zamu yako”. nikaanza uomba msamaha lakini hakuonekana ni mwenye kusamehe. Nika mwambi “naomba unihurumie kama khalid alivyomuhurumia Jlid”. basi jini akauliza “kwani jalid alimfanya ni ni Khalid”. nikaanza kumsimulia kisa cha Khalid na Jalid kwa upole kma ifuatavyo;-HADITHI YA KHALIDI MWENYE KUNEEMESHWA NA JALID.
Khalid na jalidi waliishi eneo moja huko kijijii kwao. Walikuwa na chuki zao za muda mrefu na hivyo ilipelekea uadui kati yao.Khalidi hakupendezwa na ile hali ya kuwa na uadui na watu. Khalidi alifahamika kwa ucha mungu pale kijijini na ukarimu alio nao. Wat walikuwa wakimpenda sana khalidina kumchukia Jalidi kwa tabia zake mbaya. Ijapokuwa Khalid alikuwa akimtendea wema Jalidi lakini hili halikumfanya jalidi kupunguza chuku zake kwa Khalidi.Hapo zamani khalidi na Jalidi walikuwa ni marafiki wapenzi sana wa tangu utotoni. Ijapokuwa tabia ya Jalidi haikuwa njema sana hata wazazi wa Khalidi wakawa wanamkataza kucheza na jalidi. Mambo hayakuwa hivyo urafiki wao haukuweza kuvunjika kwa maneno haya. Marafiki hawa wawili walippenda sana kuwinda kwa kutumia manati, mikuki na mishali. Walifahamika kwa uhodari wao pale kijijini walipokuwa wanaishi.
Sikumoja walipokuwa wanawinda karibu na mto ghafla nyoka aina ya chatu alimkamata Jalidi na kuanza kumbingirisha ili amuingize kwenye maji. Jalidi alipiga kelele na hiku akijikwamua kwenye mbavu za joka hili lakini juhudi zake zilikwama. Khalidi alikuja akiwa na mkuki wake na kuanza kumsaidia rafiki yake. Khalidi hakuwa na nguvu sana ukilinganisha na Jalidi lakini alikuwa akitumia akili ya ke hasa.Khalidi alikumbuka kauli ya babu yake alipomwambiaga kuwa ukipambana na chatu lenga macho yake, ukiyakosa kamata mkia wake na ukiukosa mtie jeraha sehemu ypyote lakini bora umjetuhi kwa kuuvunja mgongo wake. Mawazo haya yakapelekea mapambano makali kati ya Khalidi na nyoka yule ili kumsaidia Khalidi. Wakati huo Jalidi alikuwa ameshaanzwa kuviringishwa na lijoka hilo tayari kuanza kuvunja mbavu laini za Jalidi.Kwa upande wa Khalidi alikitafuta kichwa kwa hali na mali lakini hakukiona akakumbuka kauli ya baba yake alipomwambiaga “chatu mara nyingi anapokamata huficha kichwa chake ili kisijedhuriwa wakati wa mapambano”. basi akahamia kwenye mkia lakini mkia wa chatu ulikuwa ni vigumu kuumiliki alipoukamata alirushwa na mkia ule na alipata maumivu makali. Katika hali hiyo akakumbuka kuwa aliwahi kusikia kuwa chatu huulinda mkia wake kwa hali na mali.Katika hali hiyo Khalidi akahamia kwenye mgongo na kuamza kumjerui nyoka yule, juhudi za Khalidi hazikutoka patupu alifanikiwa kumtia majeraha kadha na hapo chtu akaanza kupoteza nguvu. Wakati anataka kuvunj mgongo wa chatu mkuki ulidunda pale ngonjo ni na ukamtoka mkononi. Mkuki ule ulikwenda mchoma Jalidi kwenye jicho na kumtoboa. Kwa pigo lile chatu alipata maumivu na kukimbia mbalia sana na kumuacha Jalidi akiugumia maumivu.Kuja kupata ahueni Jalidi alijikuta akiwa na chongo la upande wa kulia. Hali hii ilipelekea kutengeneza uadui na kuvunja urafiki. Jalidi aliamini Khalidi alifanya kususi kwani angeweza kumnusuru bila hata kumjeruhi lakini uzembe wake wa kutokukamata vizuri mkuki umepelekea maumivu kwa jalidi. Hivyo uadui huu ukajengeka kwenye nafsi ya Jalidi na kuanza kumfanyia vituki vipy kila siku. Hali hii iliendelea kwa muda mrefu sana hata Khalidi akachoshwa na vituko vya Jalidi.Hali hii haikumpendeza khalidi hivyo akaamua kuhama kwenda mjini kwa kumkimbia jalidi na kwa kuepusha shari zaidi. Kule mjini Khalidi alifahamika sana wa uchamungu hata ikafikia watu wanampenda sana kwa uchamungu wake. Watu wakawa wanakuja kwake ili awaombee dua kwa Allah Muumba wa mbingu na ardhi. Basi Khali alihamia mjini na kwa pesa alizotoka nazo kijijini alinunua nyumba na kuanza kufanya biashara ndogondogo pale mjini.Watu walimpenda sana Khalidi pale mjini kwa ukarimu, ucheshi na uchamungu wake. Watu kutoka mjini pale walikuwa wakienda kwa Khalidi na kumuomba awaombee dua. Watu wa mjini waliamini dua ukiombewa na Khalidi itkuwa ni yenye kukubaliwa na Mwenyezi Mungu. Basi pale mjini Khalidi aliishi maisha mazuri sana akiwa na upendo kwa watu hata akasahau vttuko vya jalidi. Biashara zake zilipata nuru na kipato chake kikawa kinaongezeka siku hadi siku.Licha ya kuwa nyumba ya khalidi ilikuwa eneo zuri la kibiashara lakini nyumba yake ilikuwa ina kisima ambachoo katu hakikuwahi kukaukwa wala kuchimbwa upya kwa muda wa miaka 50. khalidi alitumia maji haya kwa matumizi ya nyumbani na akawa anatowa sadaka ya maji kwa wapita njia na watu wanaokujwa kununua biashara zake. Khalidi sasa amefika umri wa miaka 30 bila ya kuwa na mke. Sasa khalidi alikuwa akifikiria kupata jiko.Siku moja bila ya kutarajia aliuona uso wa Jlidi pale mjini akija kumsalimia. Khalidi alimpokea Jalidi kwa tabasamu na bashaha akidhani ugomvi wao umekwisha. Jalidi alikaa pale kwa muda wa siku mbili na akawa anachukiwa sana na mafanikio ya Khalidi pale mjini. Basi siku ya tatu walipokuwa wanazungumza huku wanatembea wakati wa jioni wakapita karibu na kisima kile. Jalidi akajifanya anataka aelezwe mengi kuhusu kile kisima ila haukuchukuwa muda akamsukumiza khalidi kwenye kisima. Bila ya kujuwa kinachoendelea kwenye kisima alirudi nyumbani kijijini akiamini ameshammaliza Khalidi.KUTOKA KWENYE KISIMA MPAKA KUWA MFALME.
Pale kisimani khalidi aliokolewa na majini waliokuwa wakiishi pale kwa muda wa miaka mingi iliyopita. Hata kabla ya kufika chini walimzi,isha na kumbebe na kumtua kidogokidogo na hakupatwa na madhara. Majini hawa walimpenda Khalidi kwa tabia zake njema na ukarimu uliopambwa na uchamungu wake. Hivyo hawakupenda damu ya mtu mkarimu iumwagike mule kisimani walipokuwa wakiishi.Basi alipokuwa kati ya kupoteza fahamu na kurudi fahamu yaani akiwa kwenye mang’amung’amu akawasikia majini wakizungumza. “unajuwa mtoto wa mfalme wa nchi hii anaumwa sana na inapata miezi sita sasa bila ya kupona” wengine wakawa wanajibu “mimi sijapata kusikia hilo kabisa” kukatokea mmoja akasema “mimi nafahamu dawa ya ugonjwa wake” basi pale yule aliye anzisha mada akamuuliza “ni ipi dawa yake?” akamjibu “nyumbani kwa Khalidi kuna paka mwenye rangi nne na adimu sana paka hawa. Magoya saba ya mkia wa paka huyu ukiyachoma na ubani na harufu ikimpata vilivyo huyo mtoto wa mfalme kwa hakika atapona.Wale majini hawakujuwa kama Khalidi amewasikia. Basi baa da ya muda wakamtoa pale ndani ya kisima. Khalidi alipitiwa na usingizi na aliposhituka akajikuta kitandani kwake. Alipoamka asubuhi akachukuwa magoya saba ya mkia wa ule paka akisubii kuona kama aliuwa anaota au ilikuwani kweli. Siku ile ilienda salama sana na hakukuwa na tatizo lolote, na huku Jalidi akaamini amemuuwa Khalidi,Siku ilofata akaona ugeni unaingia kwake ni mfalme na msafra wake wakija kwakwe ili amuombee dua binti yake aliyekuwa anaumwa kwa miezi sita hata bila ya kupoona. Hapo khalidi akajuwa kumbe haikuwa ndoto ila ni ukweli. Pale akamchukuwa mgonjwa yule na akachukuwa udi na kachanganya na mgoya yale na akaomba dua. Hata kabla ya kumaliza alisikia kishindo. Mgonjwa alianguka chini na kupoteza fahamu.Watu wakaanza kumpepea na mflme alijuwa lamda binti yake amepatwa na jambo. Baada ya masaa kadha akazinduka na hakuhisi maumivu yeyote. Hii inamaanisha alipona kabisa ugonjwa wake. Basi mfalme kwa furaha akamwambia “kijana kwa furaha nilizo nazo sina kikubwa cha kukulipa lakini naomba umuoe binti yangu” Khalidi alikubaliana na mawazo hayo na akamuowa binti mfalme. Kwakuwa mfalme hakuwa na mtoto wa kiume basi alopofariki Khalidi akapewa ufalme na akawa anaongoza nchi.Miaka 15 sasa imepita toka aonane na Jalidi. Siku moja aliiona tena sura ya Jalidi ikiwa getini kuja kuomba msaada kwani maisha yamemuwia magumu. Jalidi alishangazwa kumuona Khalidi kuwa ndiye mfalme wao. Bila ya kinyongo Khalidi akamaidia Halidi n kumpati a vyakula na nguo kwa wingi sana na kumpatia na usafiri wa kubebea mizigo kwenda na yayo kijiji ni.Kijana alipomaliza kusimulia hadithi hii akmwambia jini “nii ndio ilivyokuwa kati ya wagomvi wawili hawa, hivyo nakuomba unifanyie huruma kama Khalidi alivyomuhurumia Jalidi pindi alipomtumbukiza shimoni. Lile jini likasema “kwa hakika khabari hii inasikitisha lakini haiewzi kulinganisha hasira nilizo nazo . kwa hakika binti niliyemuuwa nilitoka nae mabli sana. Basi pale pale jini likapiga mguu chini na upepo mkali ukanibeba. Niliachwa kuleleni cha mlima uliopo pembenu ya ufukwe. Jini lile likanambia “nitakuonea huruma, sitakuuwa lakini nitakigeuza nyani” basi akanimwagia maji yamoto na palepale nikaanza kutowa magoya na kuota mkia. Kucha na hatimaye nikawa nyani kamili.KUTOKA NYANI MPAKA KUWA CHONGO.
Katika hali ya unyani nikajiambia “kama nikiishi msituni kwa hakika italiwa na chui bora niende kwa binadamu huenda nikapata muokoaji”. mwazo yangu yakawahivyo nikashuka pale na kuelekea ufukweni. Nikakuta kunajahazi linakaribia kuondoka. Basi niktafuta mti na kuutumia kama mtumbwi na kielekea kwenye jahazi.Watu walishangaa sana kuona nyani anaweza kutumia nyenzo kuweza kuvuka. Wakaanza kukusanyika ili kuona akina ya nyani walioendelea kiasi hiki. Walikuwepo wengine wananipigia makofi na wengine wakawa wananicheka na wengine wananozonea. Mimi sikujali mpaka nikakamata jahazi na kukaa pembeni. Walikuwepo watu walotaka kunirudisha majini na wengune hata wakadiriki kunipiga mawae. Kwa bahati njewa nahodha wa jahazi akawakataza ni kuahidi kunilinda kwa maajabu niloonesha.Haukupita muda ghafla jahazi letu likavamiwa na kundi kubwa la watu walooneka na ni waheshimiwa wenye madaraka ya juu serikalini. Mkubwa wao akajitambulisha “sisi ni watu wa baraza la mtukufu muheshimiwa mfalme. Karani muandishi wa mfalme amefariki mwezi ulopita hivyo tunatafuta mtu mwenye muandiko mzuri ili achukuwe nafasi” basi wakagawa makaratasi kwa kila mtu aandike chochote kwenye karatsi.Basi walipomaliza na mimi nikaashiria nipewe karatasi ya kuandika. Basi nahodha akanipatia karatasi na kaamu na nikakaa mkao wa 4 na kushika kalamu vizuri kisomi. Watu wote walishangaa sana kuona nyani mwenye ujuzi wa hali yajuu hii. Basi niliandika mashairi machache ya kumsifu mfalme na kumjazia sifa kemkem. Kisha nikawapatia karatasi. Kwa hakika walishangaa sana kuona nyani ana ujusi wa namna hii.Basi walichukuwa makaratasi yao na kuondoka, huko mfalme aliziangalia karatasi na kuupenda mwandiko wangu. Palepale aliamuru uletwe usafiri uje kunibeba. Nilibebwa kiheshimiwa zaidi na kuekwa mbele ya mfalme. Nilitowa heshima kinyaninyani na mfalme akaelewa. Alimipa karatasi niandike nikaandika tena mashairi ya kumpamba zaidi ya yale ya mwanzo. Kwakweli alistaajabu na kufurahi pia. Mfalme alikuwa anapenda sana kucheza bao. Hivyo aliashiria liletwe bao.Basi nikacheza mechi na mfalme. Kwa mara ya kwanza nilimfunga nikaona amekasirika. Hivyo nikamwachia kanifunga goli tatu na kulipisha zote. Mwisho mfalme akaamrisha kiletwe chakula asi kikaletwa na sikula kinyaninyani nilinawa mikono na kula kwa kutumia mikono yangu. Yote nilokuwa nikiyafanya yalikuwa yakimstaajabisha mfalme na watu wa baraza lake.Ilipofika jioni mfalme akaagiza aletwe binti yake wa kipekee ili astaajabu uwepo wa nyani mbele ya macho ya mfalme. Kama zilivyo tamaduni za waislamu mtoto wa kike hujifunika mwili wake ila kwa ndugu zake wa karibu na wazazi wake. Kwakuwa aliitwa na baba yake alukuja kawaida hat bila ya kujifunika. Ila maratu alipoingia kwa baba yake alihaza na kurudi nyuma na kwenye kujifunika kisha akarudi. Mfalme alishangaa kilichomsibu hata mwamnae akarudi.Binti akaeleza “baba unaniita mbele ya mwanaume mwingine nikiwa sijajifunika” pale mfalme alishangaa na kumwambia “nipo mimi tu hapa na huyu nyani, ametoka wapi huyo mwanaume mwingie?”. akajibu “baba huyo sionyani ni mtu na amegeuzwa kuwa nyani kiuchawi. Ni aina za uchawi wanaotumia majini” basi mimi kusikia maneno yale nilitingisha kichwa kuashiria kukubaliana na maneno ya binti. Mafalme akamwambia “umeyajuwa vipi haya mwanangu?” binti akajibu “yule bib I aliyekuwa akinilea alinifundisha aina nyingi za uchawi na kuopoa”.Basi mfalme akamtaka binti yake aniopoe na binti akakubali. Siku ilofata asubuhi sisi watatu tulielekea kwenye jumba bovu lililohamwa zamani am,bapo binti amelelewa na huyo bibi. Binti akatuambua mimi na mfalme kukaa pale na tusiondoke kwa loote lile litalotokea. Hivyo binti akaanza kuzungumza maneno yasiyojulukana. Ghafla akatokea nge na binti akageuka kenge akawa anamkimbiza nge amle. Yule nge akageuka tandu na binti akageuka nyoka.Basi ikawa hivyo kila mmoja akigeuka flani mwinzie anageuka kitu kingine. Hali ilikuwa hivyo mpaka yule nge akageuka kunguru basi binti akageuka kipanga wakapaa wakikimbizaa na tusiwaone walipokwenda. Tulikaa pale kwa muda mrefu na tusiwaone. Ghafla tukaona punda aliyefundia kitu anakuja na akatema punje za komamanga. Kisha akageuka kuwa kuku mtembe na uanza kula punje za komamanga. Alizila zote alizoziona akawa anaashiria kama kuna ingine.Kumbe kulikuwa na punje moja imebaki iliyokuwa ikibingiria kulekea kwenye mfereji wa maji. Aliiwahi aikamate lakini akachelewa na ikaangukia kwenye maji, na palepale ikageuka kuwa samaki. Binti akageuka kuwa samaki mkubwa zaidi na wakakimbizana mpaka yule samamki akageuka kuwa dragon na kuanza kumwaga moto. Binti akageuka kuwa dragoni na kutukinga sisi na motoule. Kwa bahati mbaya moto uke ulumchoma binti kwenye miyo na chehe ikajanipata kwenye jicho na kulipasua na hiyo ikawa ndio sababu ya chongo yangu ya jicho la kulia.Baada ya mapamabno makali binti alifanikiwa kulichoma jini lile na kuliuwa. Alianguka chini na kuanza kuhe,a kwa uchovu. Alipopata nguvu akachukuwa majivu ya lieldragoni la kijini na kuchanganya na maji. Akatamka maneno na kunumwagia na palepale nikageuka kuwa mtu kamili. Furaha ilitanda kwa mfalme ila ghafla binti aliikata furaha hii kwa kumwambia “baba nimefanikiwa kumuuwa jini na kumtibu kijana, ila na mimi umri wangu umebakia siku tatau tu. Ule moto uliniunguza kweye moyo”.Siku tatu binti alifariki dunia na majonzi yalienea kwa mfalme kwani alikuwa na mtoto mmoja tu. Baa da ya situ saba mfalme aliniita na kunambia “upo huru kwa sasa maana sio nyani tena. Nimefanikiwa kukuokoa lakini nimepoteza maisha ya binti yangu. Hivyo siwezi kukuangalia. Ninakuomba uondoke nchini hapa na usirudi tena, kwani uwepo wako utaendelea kunikumbusha binti yangu.Basi nikaamua kuondoka nchini pale na nisijuwe pa kwenda. Nikaeekea baghdadi na nikanyoa kichwa cahngu na nyusi zangu. Nilipofika hapa nikakutana na wenzangu hawa na hatukupata kujuwa hadithi ya kila mmoja kati yetu. Hivyo hii ndio hadithi yangu. Zubeidah akamfuata waziri na kumwambia ataje stori yake yeye na wenzie basi akaeleza kuwa wao ni wafanya biashara wameomba hifadha pale baada ya kuingiliwa na usiku.Basi mpaka wanamaliza kusimulia hadithi zao ilikuwa ni majogoo hivyo Zubeydah akwaaruhusu watu wote watoke mule ndani. Bila hata kuomba waruhusiwe kukaa mule mpaka asubuhi walitoka mbiombio. Mfalme aliyejifanya mfanya biashara akamwambia waziri “wachukuwe chongo hawa watatu na ukalale nao nyubani kwako na ifikapo asubuhi niitie wale wanawake watatu wote waje kwenye baraza letu nao wataje hadithi zao. Inaonekana kuna makubwa yamewafika.
Basi mambo yakawa kama alivyotaka mfalme, kesho asubuhi wale wadada wakaletwa mbele ya mfalme na mfale akawaambia “hatukuwaita kwa kuwaadhibu kwa mlichotufanyia jana ila tunataka mtueleze na nyinyi haithi zenu hata mkayafanya yale mlikuwa mkiyafanya. Zubeydah aliposikia sauti ile akajua niwale watu wa jana kumbe ni mfalme na watu wake. Basi akapiga magoti na wenzake wakafata na akaanza kuomba msamaha “tusamehe ewe mtukufu mfalme, kwa hakika hatukujuwa kuwa ni wewe mfalme, tumekukosea sana hata tukaweza panga kwenye shingo yako” mfalme akamjibu “nimekwisha samehe tafadhali aeni bila wasi na mueleze hadithi zenu.Mfalme akawa anawashawishi kwa maneno mazuri na kuwaambia “nioneni kama mpo na rafiki zenu hapa na kuwa huru kusema chochote kile”. basi mabinti wakaanza kuangaliana wakitafakari ni nani aanze kusimulia hadithi yake. Kabla hawajaanza na wale machongo watatu wakaletwa ili wapate kusikiliza hadithi za wadada hawa. Basi wakaanza kusimulia hadithi zao kama ifuatavyo;-HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA.
Kwanza jua ewe mtukufu mfalme kuwa wale mbwa wawili uliowaona ninawapiga ni ndugu zangu wa baba na mama mmoja. Tuliishi pamoja kwa zaidi ya miaka 10 toka kufariki kwa baba kabla ya kutokea yale ambayo umeyashuhudia usiku wa jana. Basi tambua ewe mtukufu mfalme kuwa dada zangu hawa walinifanyia ubaya ambao ndio chanzo cha haya yote. Basi wakati Zubeida anazungumza maneno haya mbwa walikuwa wakitingisha vichwa na kutowa machozi.Tambua ewe mtukufu mfalme kuwa yote niliyokuwa nikiyafanya ni kwa ajili ya uhai wa mbwa hawa yaani dada zangu. Laiti kama sitawachapa fimbo zili wangelikufa papo hapo. Juwa ewe mfalme wa nchi hii kuwa yote niliyokuwa nikiyafanya sikuyafanya kwa hiari yangu ila nimeshinikizwa. Nini kulitutokea na nini ninachotakiwa kufanya. Nitaomba ushauri wako ewe mfalme baada ya kusikiliza hadithi yetu.Basi pale kwenye ukumbi wa mfalme kukaingiwa na utulivu wa hali ya juu. Machongo watatu walikuwepo wakitaka kujua zaidi kilichowakuta wenzao. Wakati mfalme na waziri wake wananshauku ya kutaka kujuwa hasa nini kilimtokea Zubeida. Basi mfalme akaagiza hadithi hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye nyaraka maalumu. Basi Zubeida akaanza kuhadithia zaidi kama ifuatavyo;-Tuliishi na baba yetu kwa furaha zaidi kwa muda wa miaka mingi. Mama yetu alifariki tukiwa wadogo, hivyo baba yetu akalazimika kuwa na majukumu ya umama. Baba yetu alikuwa ni mfanya biashara maarufu na alikuwa amefaniukiwa kwa kiasi kikubwa sana. Baba yetu alifariki kwa ghafla hata bila ya kuumwa. Baada ya mazishi tuligawana mirathi kwa mujibu wa sheria ya kuuslamu. Na kwa kuwa hatukuwa na ndugu wa kiume sote tulipewa mali ya mirathi kwa usawa kila moja.Mimi na dada zangu wote tukawa tunafanya biashara. Wote tulinunua nyumba na kuendelea na biashara zetu. Kwa upande wangu nilifanikiwa sana na biashara zangu zilikuwa kwa haraka zaidi. kwa muda mfupi niliweza kurudisha mtaji wangu na kuanza kukusanya faida. Halikadhalika na dada zangu nao waliweza kutengeneza faida kwa muda mchache. Unaweza kusema lkuwa tulibarikiwa kibiashara.Dada zangu waliolewa lakini mimi sikubahatika kupata mchumba. Siku szote nilikuwa namuomba Mwenyezi Mungu anipatie mchumba aliyekuwa ni mwema. Dada wa kwanza alipoolewa alihamishwa na mumu wake na kwenda mji wa jirani. Huko aliendelea na biashara zake pia, lakini kwa vituko vya mume wake hakuchukuwa muda akafilisika. Bila ya kuelewa chochote kumbe dada yangu aliposwa na mume yule si kwa sababu alimpenda ila ni kwa sababu ya mali zake.Dada alipofiliskisa hakuweza kumuona mumewe tena kwake. Na alipokuja humpiga na kumtukana sana. Hakuwa hata anamletea cha kukila wala cha kuvaa. Nikiwa sina habari ya hili wala lile kwa yanayompata dada yangu. Hali iliendelea kuwa ngumu kwa dada yangu hata mambo yakamshinda. Kwa mujibu wa sheria za kadhi aliweza kudai talaka na kuachwa. Siku ile aloachwa yule mume wake alimvizia na kumpiga na kumchania nguo zake na kumnyang’anya kila alichokibeba.Dada yangu alijikongoja hata akafika nyumbani kwangu. Kwa hakika sikumtambua kwa hali alonayo maana alikuwa ni nusu uchi. “Ashakumu si matusi” dada yangu akaniambia nisitiri ndugu yangu kwa hakika nimekumbwa na msiba ambao sitausahau. Basi nilimpatia pesa ambayo nimeiweka akiba na kumpatia aanze na biashara. Dada aliweza kuanza biashara tena na kuanza kukuza mtaji. Alipotaka kunirudishia pesa nilompa nilikataa na kumwambia kuwa ilikuwa ni sadaka.Kwa upande wa dada yangu wa pili yeye alipotaka kuolewa katu sikumilia kipingamizi. Na aliolewa na mfanyabiashara mwenzie wa nchi ya jirani.. Hawa walikuwa wakifanya biashara za majini kutoka kisiwa mpaka kisiwa. Basi dada na mume wake walifanya hivyo kwa juda wa miezi 6. kwa muonekano walionesha kupendana sana na kuishi kwa amani na furaha katika ndoa yao. Kwa ndani mambo hayakuwa hivyo.
Kwa kuwa dada alibarikiwa kibiashara pia alikuwa na mali nyingi hata akamzidi mume wake zaidi ya mara tatu. Sasa bila ya yeye kutambua kumbe mume wake aliuwa napanga njama ya kumuibia mali zake na kumtelekeza. Siku moja walipokuwa kwenye dau mume wake alipanga njama na nahodha ili alizamishe dau kimaksudi. Kwa kuwa dada hakujuwa kuogelea waliamini atakufa tu. Basi walifanya kama hivyo na jahazi lilipozama dada alitumbukia majini.Kwa kuwa ilikuwa ni njama nahodha na wenzake waliweza kuokoa mali na watu wengine na kumuacha dada yangu kuangamia majini. Mume wa dada waliendelea na safari zao wakiamini kwa kuwa dada ameshakufa kinachofata ni kugawana mali. Na mambo yakawa kama hivyo walivyopanga. Lakini kitu kimoja hakikuwa kama walivyotaka, ni kuwa dada yangu katu hakufia majini na aliokoka kwenye ajali hii. Kwa kweli Mwenyezi Mungu ni mkubwa.Wakati dada alipotumbukizwa kwenye maji wanyama wa majini walikuwa wakicheza na samaki mkubwa alimbeba na kuja kumtupia ufukweni. Na kwa hali hii dada yangu aliweza kuokoka. Kwa bahati nzuri dada alipookolewa alitupwa kwenye ufukwe wa nchi yetu hii na kutegemea nguo alizoziokota ufukweni aliweza kuja nyumbani. Kwa hakika nilishindwa kumtambua isingelikuwa kidani chake alichokuwa anakipenda.Sasa mimi na dada zangu tumekusanyika tena nyumbani baada ya utengano wa muda. Nilimpatia dada yangu huyu nae pesa kama nilompa dada yangu wa kwanza. Ana alianza kufanya biashara zake. Dada zangu hawa waliungana pamoja na kuanza kufanya biashara za majini. Hivyo wakawa wanatembea kwenye visiwa mbalimbali kufanya biashara. Kwakweli biashara zao zilikuwa vizuri sana na walipata umaarufu na mali nyingi pia. Walifanya hivi kwa muda mrefu takribani kwa miaka miwili. Sikujuwa kumbe waliweza kuwa na hisia za ubaya juu yangu.Wakati fulani wakaniomba niungane nao kwenye biashara zao lakini nilikataa. Walirudia kuniomba kwa zaidi ya mara 4 kwa nyakati tofauti. Basi mara ya tano nikakubali na kwa haraka wakaanza kuandaa safari na kuniandalia pia kwa upendo walionesha kunijali sana.basi nikagawa pes zangu mafungu mawili, fungu moja nikalifukia kama akiba na fungu la piali nikalitumia kuandaa bidhaa. Basi maandalisi yalipokamilika sote tulitoka na kuelekea ufukweni na kupanda jahazi letu lililojaa bidhaa. Safari ilikuwa njema sana, na nilifurahia pia maana ilikuwa ni mara yangu ya kwanza japo nilitapika sana.Tulikwenda kisiwa mpaka kisi tukifanya biashara. Kwa hakkika nilipata faida sana kuliko pale nyumbani. Kwa safri yote nilikuwa naomba tufike salama maana sikupenda mazingira ya majini. Basi tulipokuwa tukirudi nyumbani kwa ghafla upepo ulubadilika na mawimbi yakawa makubwa. Nahodha hakuweza kutia nanga hinyo akaliwachia jahazi lielekee kokote kule na hii ndio njia salama kwa manahodha. Basi jahazi lilikwenda mpaka upepo ulipotulia asubuhi ya siku ilofata.Tulishangaa tupo karibu na kisiwa ambacho kinaonekana ni mawe tu. Basi nahodha alipoulizwa hakuwa na ujuzi wa eneo hili, ila akashauri watu waingie kisiwani ili wakapate maji ya kunywa na kupata hewa safi. Kitu cha kushangaza ni kuwa kisiwa kizima kilikuwa ni mawe. Yaani majimba, miti, wanyama, watu na mikokoteni ni mawe matupu. Hata walinzi wa magetini walionekana kuwa mawe matupu. Kwa hakika huu mji ulikuwa ni wa ajabu sana. Kila mtu alitaka kujuwa habari za mji ule lakini ni nani wa kuwaambia.Jambo linhine la kushangaza ni kuwa pesa na dhahabu zilikuwa zikizagaa masokoni ambapo watu wake wamegeuka mawe. Watu wa kwenye jahazi walikuwa wakistaajabu na kuanza kukusanya pesa na dhahabu. Kwa upande wangu niliendelea ndani zaidiya mji ule kujuwa zaidi habari. Nilipokwenda nikaingia kwenye ukumbi wa mfalme na nikamkuta amekaa kwenye kiti chke akiwa ni jiwe. Dahabu alizovaa zilikuwa zikining’inia tuu. Nikasogea zaidi na kukuta baraza la malkia likiwa na wanawake wengi nao wakiwa ni jiwe na mapambo yao ya dhahabu yakining’inia tuu.Kwa hakika nilistaajabu sana na niliendelea pia. Niliona mambo mengi na ya kushangaza. Nilipokuwa kwenye eneo la kulia chakula watu nikuta wamegeuka mawe na vyakula vikiwa vizima hata kuharibika bado. Nikiwa katika hali ya mshangao nikasikia sauti ya mtu anasoma Qurani. Sikuamini hivyo nikasikiliza vizuri sauti ile na kupata uhakika wa kuwa nimesikia vyema. Hivyo nikaanza kuifata sauti ile hata nikaingia kwenye kijichumba kimoja na kumkuta kijana wa kiume mzuri sana. Nilibakia nikistaajabu kwa uzuri wake hata nikasahau yaliyonistaajabisha hapo mwanzo.Nilimsogelea kijana yule na kumsaalimia kwa salamu ya kiislamu na akaniitikia kwa upole zaidi. Sikuamini kama ni mtu au ni jini hivyo ikabidi nimuulize vizuri. Bila ya wasi akanijibu kuwa yeye ni mtu wa kawaida tu na ni mtu pekee aliyeokoka na janga liliowapata watu wa eneo lile. Kwa shauku nikamuuliza ni kipi basi kilichowapata watu wa eneo lile. Aliniangalia kwa huzuni kisha akaanza kufuta machozi yake na kunza kunisimulia hadithi ya yaliyotokea eneo lile kama ifuatavyo;-HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.
Mimi ni mtoto wa mfalme wa nchi hii ambayo umemuona amegeuzwa jiwe kama watu wengine. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikilelewa na bibi mmoja laiyekuwa ni muiislamu. Watu wa mji huu walikuwa wanaabudu masanamu hivyo bib i yule alifanya siri imani yake. Na kwa usiri huo akanifundisha imani ya uislamu juu ya mungu mmoja na akanifundisha kusoma Qurani. Katika muda wote niloishi nae yapata miaka 10 alikuwa akinisisitiza kufanya siri imani ile na mambo yakawa hivyo mpaka bibi yule alipofariki.Mwaka juzi alikuja mtu mmoja hapa nchini kwetu, mtu huyu ulikuwa ikilingania watu kuhusu kumuabudu mola mmoja tofauti na watu walivyozoea. Mfalme aliongea maneno ya ajabu na ya kipuuzi kuhusu sauti ile. Mtu yule aliondoka na akarudi tena mwaka jana na maneno yalikuwa ni yalelyale. Na mfalme yaani baba yangu alirudia maneno yaleyale. Na mara ya tatu mwaka huu alirudi tena Mtu yule na mambo yakawa vile vile.Wiki mbili baada ya kuondoka kwa Mtu yule ikatokea sauti ikionya na kulingania juu ya imani ya munngu mmoja. Hali ikawa kama mwanzo Mfalme wetu akatoa kejeli na maneno machafu sana. Kwa hakika niliumia na nikataka kwenda kumtia adabu baba yangu mwenyewe lakini nilishindwa kufanya hivyo. Machozi yalinitoka na nisijuwe jambo la kufanya na hakina wa kunishauri. Basi haikupita muda mrefu ile sauti ikatoweka na hapo anga ikafunga kuwa nyeusi kutokana na wingu lisilojuliukana kama la mvua au upepo mkali.Wingu lile liliendelea kusogea chini hata likakaribia kufunika nyumba. Ulikuwa ni wakati wa muda wa swala ya adhuhuri na watu wamechanganyika katika utaftaji. Wengine wapo masokoni na wengine mashambani na hali kadhalika. Wingu lile likaambatana na upepo mlaini ambao haukuweza kuharibu hata kipande cha nguo kilichokuwa kinaning’inia. Upepo ule uliingia masikion, puani na kila sehemu yenye tundu na kutokea upande mwingine.Haukupita muda wat wote wakawa katika hali uloiona kuwa mawe. Na kia mtu vile alivyo ndivyo alivyobaki. Hata walokuwa wamelalaq wamebakia mawe kwenye vitanda. Nilitoka kuchunguza zaidi sikuona hata mnyama ambaye aligeuzwa jiwe. Kwa hakika msiba huu uliwapata wanadamu tuu. Basi nikawa sina pa kwenda hiyo nikabakia kisiwani hapa peke yangu kama unavyonioa. Na hii ndiyo historia ya kisiwa hiki kilichogeuzwa mawe.Wakati kijana anamaliza kusimulia hadithi ile Zubeida akawa analia na machozi yanamtiririka kama chemchem iliyoanzia mlimani. Basi kijana kwa huruma akawa anamfuta machozzi Zubeida. Baada ya muda Zubeida akauliza “sasa wanyama walikwenda wapi?” kijana akamjibu baada ya kutokea yaliyokwisha tokea ilikuja tena ile sauti na kuniambia kuhusu hatima ya wanyama. “ama kuhusu wanyama amri yao ipo kwako, eidha utawatumia kama chakula chako mpaka Allah atakapoleta nusra , ama awahamishe awapeleke anakotaka ama wageuzwe kuwa vitu vya thamani na iwe kama zawadi ya Zubeida mwenye kupotea njia mwana wa tairi na msalitiwa na ndugu zake.Basi nikachaguwa jambo la tatu, na pindi ulivyokuja nilifahamu hakika ni wewe Zubeidah. Zubeida akamuuliza “ni kitu gani kilichokufahamisha” akaendelea ile sauti niliiulisa sasa ni kwa namna gani nitamfahamu Zubeidah ikajibu siku moja kabla ya kuja kwa Zubeiday bahari itakuwa chafu sana na upepo maini utaingia kisiwani hapa na kusafisha nyia ya Zubeida mwana wa tajiri, msalitiwa. Hivyo Zubeida atakuwa hana jinsi ila atakufikia tu popote utakapokuwepo muda huo. Basi nilipoziona ishara hizo nilifahamu ujio wako hivyo ili kukurahisishia kunipata nikawa nasoma Qurani kwa sauti ya juu ndivyo ukanisikia.Ama kuhusu kusalitiwa kwa Zubeida na ndugu zake nilishindwa kujuwa mengi zaidi maana sauti ile ikanambia hainipasi kujuwa siri za mambo yajayo. Halikadhalika ninachofahamu zaidi kuhusu huo usaliti ni kuwa maisha yangu ama yako yatakuwa hatarini. Basi Zubeida na yule kijana wakatoka pale na Zubeidah akashauri waoane na wakakubaliana kufunga ndoa punde watakapofika nyumbani.Basi kijana akampeleka Zubeidah kwenye zawadi yake na akakuta mali nyingi sana na tayari imeshafungwa vizuri kwenye mkokoteni. Basi wakaburuza mkokoteni wao mpaka kwenye chombo chao na kuuingiza ndani. Wakawa wanapunga upepo ufukweni na kubadilishana mawazo na kuchat. Wakiwa katika hali hiyo ghafla akatokea nge anakimbizwa na kunguru Zubeidah akachukuwa kijiwe na kumpiga kunguru na ukawa ndio mwisho wa maisha ya kunguru yule na nge akatokomea kwenye mawe. Na wawili hawa wakaendelea kuzungumza. Wakati yote haya yanafanyika dada zake na Zubeidah walikuwa wakiona wivu na kijicho kwa mafanikio ya ndugu yao.

USALITI UNANZA HAPA
Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Ndugu zake na Zubeidah kumbwe hawakupendezwa na mafanikio ya ndugu yao. Hali hii iliwafanya kuwa na wifu na kijicho. Basi zubeidah akaongea na ndugu zake na kuwapa mali zile zote na kuwambia mimi shida yangu ni kufika salama na huyu kijana ambaye kwa sasa ni mchumba wangu na tutaoana punde tu tufikapo nyumbani. Mali zile wakagawana ndugu wawili hawa.Hili pia halikutosha wakataka na wawaue kabisa, na kawafanya hivyo katika majira ya usiku. Waliwachukuwa wawili hawa na kuwatia baharini. Anakuja kushituka zubeida yupo baharini anakunywa maji ya chumvi na hatimaye kupoteza fahamu na asijue nini kiliendelea. Basi kwa furaha ndugu wale wakaanza kugawana tena mali zile.Kwa upande wa Zubeidah alopokuja kupata fahamu ilikuwa ni wakati wa jioni na akajikuta amezungukwa na kundi la wananwke wenye sura nzuri za kuvutia waliojipamba vizuri sana. Mbele yake kuna kiti kirefu sana kilichopamba na magodoro yaliyochovywa kwenye dhahabu nyekundu. Miguu ya kiti hicho ni meno ya tembo yaliyopambwa vizuri. Kwa hakika kiti hicho kilikuwa na kila aina ya mapambo mazuri. Aliponyanyua kichwa akaona amekaa juu ya kiti hicho mzee wa heshima mwenye ndevu ndefu zilizo kaa vyema.Zubeida kwa mshangao alionekana kufurahia mazingira yale na asijuwe nini kinaendelea. Alikuja msichana wa makamo hivi aliyependeza sana na akampaka maji ya marashi yaliyochanganywa na misk na kutiwa manukato mazuri sana. Zubeidah akarudisha kumbulkumnbu zake zote na akajuwa kwa mara ya mwisho alitumbukia kwenye maji sasa akawa anajiulia yupo wapi?. Yule mzee akamwambia “mwanangu furahia uwepo wako hapa kwa hakika hupo peponi wala kuzimu, hapa upo chini ya bahari na mbele yako ni mfalme mkuu wa majini yaendayo baharini na nchi kavu. Mzee yule akaagiza kuwa Zubeidah afanyiwe kila kinachostahiki kufanyiwa kisaha akatoweka.Kwa shauku Zubeida alikuwa na maswali mengi sana, wakaja mabinti watatu waliokuwa na sura nzuri sana hata Zubeidah akajiona yeye si lolote wala si chochote, wakamchukuwa na kwenda nae bafunu. Huko maji yaliyo na umoto kwa mbali yalikwisha andaliwa. Kwa mara ya kwanza Zubeidaha anakwenda kuoga maji yaliyotiwa marashi pamoja na misk nyekundu, manukato mablimbali yenye kuvutia. Zubeidah alijihisi yupo ulimwengu wa raha. Kwa maringo na madaha wakamvua ngu Zubeidah na kumtumbukiza kwenye bafu lile na kuanza kumsuguwa.Wakaendelea kumsuguwa kwa visugulio vyenye rangi ya silva vilivyochovywa kwenye marjani. Kwakweli utasema mwili wa Zubeidah umekuwa lulu iliyohifadhiwa vizuri. Uchafu wote mwilini mwa Zubeidah uliondoka hata akawa kama akawa kama aliyofanyiwa scrub na kumbakisha kama mtoto alozaliwa. Ngozi laini na nyusi za kupendeza. Hawakuishia hapo wakaendelea kumpmba na kumpaka manukato. Nguo safi za hariri zenye mapindo yalochovywa kwenye dhahabu, hakika siwezi kuelezea zaidi urembo walomchagulia.MALIPO YA WEMA NI WEMA
Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi. Hapa Zubeida akawa anajiulia kuwa ni nani huyu anakuja? Aua ni yule mchumba wake? Maswali haya hayakupata amjibu. Baada ya muda kupita akatokea binti mmoja mreembi kama mwezi uliokamilika umbo lake. Binti yule akamsogelea Zubeidah na kupiga goti mbele yake na kuukamata mkono wa Zubeidah na kuubusu kisha akamwambia “ NI YAPI MALIPO YA WEMA? KWA HAKIKA NI WEMA TU”.Lilikuwa ni swali ambalo halihitaji majibu kutoka kwa Zubeidah. Kwa malipo ya wema ni wema, Zubeida akamuuliza “ni nani wewe ni ni nani mimi na nimefuka vipi hapa?. Yule mrembo akaanza kutoa kisa chake. Kuwa yenye ni mtoto wa mkuu mfalme wa majini ambaye alionana naye hapo mwanzo. Alipokiuwa matembezima jana akiwa amejibadili katika umbo la nge alipokuwa nakimbizwa na adui wake aliyekuwa katika umbo la kunguru alimsaidia kwa kumuuwa adui wake kunguru. Hivyo yule nge alikuwa ni huyu mtoto wa mfalme. Kwa ufupo ni kuwa Zubeidah amemuokoa mtoto wa mfalme katika kizingiti za kifo kuuliwa na adui wake na huu ni wema mabao analipwa.Basi yule mrembo akamwambia Zubeida kuwa ndugu zako walipokutumbukiza baharini nilikuwepo kwenye jahazi lenu kwa nia ya kuku;inda mpaka ufikapo kwenu. Hivyo nilikuokoa kwenuye ajali ile na sikuweza kumuokoa mchumba wako, kwa hilo naomba unisamehe sana. Hata hivyo baba yangu anaweza kukupa chochote utakacho kiseme utapata, na hata ukitaka utaishi hapa na mimi. Ila kuhusu ndugu zako kwa hakika sitaweza kuwasamehe katu. Nitawapa adhabu kubwa sana nai ningewauwa ila kwa kuhofia chozi lako siwezi kufanya hivyo.Basi Zubeidah akaitwa na mfalem wa majini yule na kuulizwa nini ameamua kati ya yale aloelezwa na binti mafalme. Zubeidah akachagua kurudishwa nyumbani kwao na hakuhitajia chochote. Basi binti mafalme akampa unywele wake na kumwambia ukiwa na shida na mimi choma nywele hii kwa hakika nitakuja hapo kwa haraka zaidi. Basi kufumba na kufumbua Zubeidah akajikuta yupo nyumbani kwake na mlangoni wamekaa mbwa wawili na kuangalia pembeni akakuta bahasha ambayo imewekwa mlangoni. Kufungua bahasha ile akakuta ndani kuna barua iloandika\wa “Kutoka kwa Binti Mfalme wa majini ya majini na Nchi kavu kwenda kwa Zubeidah mwana wa tajiri mpotea njia mwenye kusalitiwa. Ama baada ya salamu napenda kukutaarifu kuwa hao mbwa unaowaona mlangoni kwako ni ndugu zako na hiyo ndio adhabu niloichagua. Watabaki hivyo kwa muda wa miaka 10 na utakuwa ukiwapiga fimbo za mijeledi 300 kwa kila mmoja na kila siku. Na kama hautafanya hivyo watakufa siku inayofata. Ama kuhusu mali zako zote nimeziokowa na zipo stoo. Hata hivyo baba yangu amekujengea nyumba karibu jirani na mji wa Mfalme mwadilifu Harun Rashidi mfalme wa Baghdah. Huko uende na ukakae na ndugu zako hao. Usisahau kufanya nilichokwambia Zubeidah.”Hivyo Zubeidah akachukuwa mali zake na kuhamia katika nyumba ile aloambiwa mjini Baghdad na ndugu zake. Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii mbwa wakawa wanatoa machozi mengi sana na hata mfalme akawa anatoa machozi. Hivyo hii ndi sababu ya mimi kuwaadhibu mbwa hawa kila siku yalikuwa ni maneno ya Zubeidah. Mfalme baada ya kusikiliza hadithi hii akamgeukia Amina aliyekuwa na alama na makovu kwenye mwili wake na mumwambia aeleze hadithi yake, nae akaanza kama ifuatavyo;-HADITHI YA BINTI WA PILI MWIMBA MASHAIRI MWENYE AKOVU.
basi juwa ewe mfalme wetu kuwa nilikuwa naishi na wazazi wangu na hatimaye wakanitoka na kuniwacha peke yangu. Niliachiwa mali za kunitosheleza kuishi kwa muda mrefu bila ya kuomba. Wate wengi walinisifi kwa uzuri nilio nao ijapokuwa nilihisi wananitania tuu siku nilipokuta na na Zubeidah kwa hakika alikuwa mzuri zaidi. Nili kaa pale nyumbani kwa muda mrefu niliwa peke yangu bila ya mume.Sikumoja alikuja bib mmoja na kuniambia kuwa mjukuu wake anashuhuli na hakuna mtu wa kumsimamia shuhuli yake hivyo akanitaka niwe kama msimamizi wa mambo ya wananwake kwenye shuhulu hiyo. Basi niliongozana na bibi yule hata tukafika mwenye shuhuili ile na mambo yakaenda salama. Ilikuwa ni shuhuli ya kuwakumbuka walotanguluia kufa kama kawaida ya waislamau wanavyoifanya mjini pale. Basi shuhuli ilipokwisha yule bibi akaniita katika chumba cha ndani na bila ya kuwa na wasiwasi nikaenda. Kufika kule ndani nikakutana na kijana mmoja aliyekuwa mtanashati na katika mazungumzo akaniposa na mimi nikakubali. Kumbe lile ndo lilikuwa lengo la yule bibi toka mwanzo.Basi maandalizi ya harusi yalifanyika na nikaolewa mwezi ulofata. Kwa hakika ndoa yetu ilikuwa ni njema na haina migigoro kwa muda wa miezi sita ya mwanzoi. Ama mimi sikuruhusiwa kutoka nje, hata sikuhiyo niikaomba ruhusa ya kuenda sikoni kununua mahitaji yangu binafsi na mume wangu akaniruhusu. Kule sokoni wakati narudi anilikutana na mlevi mmoja na tulipokuwa tunapishana akaning’ata kwenye shavu. Kumbe alikuwa ni mmtoto wa baba yangu mdogo ambaye nilimkatalia kunioa aliponiposa.Wakati haya yote yanafanyika mume wangu alikuwa amejibanza na alikuwa anaona. Na pia alitambua pika kuwa yule alikuwa nai mtoto wa baba yangu mdogo. Na alidhani kuwa ni mzinifu mwenzangu nilipokuwa naishi peke yangu kumbe sivyo. Basi niliporudi nyumbani akaniuliza sababu ya kidonda kwenye shavu langu nikamjibu nimegongana na mkokoteni, basi akasema nitamtafuta huyo mwenye mkokoteni na nitamua, nikamwambia usimuue mtu asiye na hatia kwani ni ajali tu.Basi akanikaba shingoni na kuniuliza kwa zaidi sababu ya kidonda kule na kunmbia anajua nimeng’atwa na mzuiinifu mwenzangu wa zamani basi akaamrisha nikakamatwa vizuri na na akaanza kinipiga fimbo za mijeledi mpkaka nikapoteza fahamu. Nilipozinduka akanifukuza na pale kwake na kufika nyumbani kikakuta nyumba yangu ameobomoa bomoa a nikakutana na Zubeidah kwa mara nyingine na kukubaliana kuishi pamoja. Niliendelea kuuguza vidonda vyangu hata nikapona na kubakia makovu ndio uloyaona. Hii ndia hadithi yangu ewe mfalme.Basi mfalme akamgeukia Sadie na kumwambia azungumze hadithi yake na kusema kuwa yeye alikuwa ni mtoto yatima ombaomba ambaye alikutana na Zubeidah na kumkirimu kama dada yake na nikamkuta min anaishi nae pia, hatukuwahi kuzungumza hadithizetu kama hivi. Hivyo hii ndio hadithi yangu ewe mtukufu muadilifu mfalme wa Baghdad; harun Rashid.Baada ya kusikiliza hadithi za mabinti hawa, Mfalme nae akaamua kufungua mdomo wake kwa kuwauliza maswali “hivi mnafikiri kuwa kila mtu ana hadithi za kusisimua katika yale yalowapata kwenye maisha?” Zubeidah akajibu “naam kwa hakika ana kila mmoja hadithi ya kusisimua katika maisha yake, aaanhaa nadiriki kusema hata wewe Mfalme unayo yako ijapo hatuwezi kukwambia utueleze”. Mfalme alimuangalia sana Zubeidah kisha akasema “naam hata mimi na waziri wangu tuna hadithi yetu, na leo nitaisimulia kwenu hadithi ambayo katu hatujawahi lkuisimulia.” basi Mfalme nae akaanza kufungua mdomo kwa kusimulia hadithi yake.HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE
Basi tambueni enyi rafikizangu kuwa mimi na waziri wangu huyu hatutokani na familia za kifalme wala mimi baba yangu hahusiani hata kidogo na ufalme. Tumepata vyeo vyetu hivi wakati tukiwa katika hali ngumu ya maisha. Mimi na waziri wangu tulipata vyeo vyetu tulipojifanya tunaswali baada ya kukimbizwa kuwa wezi tulipokuwa tunaiba msikitini. Bila shaka hamjaelewa nini ninamaanisha. Ila kwa ukweli zaidi mambo yalikuwa hiviTulikuwa ni watoto yatima tuliofiwa na wazazi wetu tungali wadogo. Sikuzote tuliitegemea chakula kwa kuokota ama kuomba. Tulianza tabia ya wizi, ingali tunajuwa kuwa wizi ni haramu, na ukikamatwa utakatwa mkono kwa mujibu wa sheria za dini. Tukiwa hatuna jinsi ya kutupatia rizki tulikuwa tukiiba vitu kwa watu na kuuza kujipatika pesa.i mwingine tunanakosa hata cha kuiba hivyo tunalala bila kula. Wakati mwengine tulikuwa tukipigwa pindi tunapokwenda kuiba.Tulianza kujishughulisha na shuhuli za kufanya biashara ndogondogo ijapokuwa hali haikuwa nzuri pia. Tuliamua pia kujikita katika kibeba taka majumbani hali ambayo pia haukuwa na uwezo wa kutufanya tupate riziki kwa unafuu. Kwa hakika maisha yetu yalikuwa ni magumu sana. Hatukujuwa kusoma wala kuandika. Na kwa bahati mbaya tulisomaga dini tukiwa watoto na kukimbia masomo hivyo tulifanikiwa kujuwa kuswali na mambo machache tuu.Wakati mwingine tulijiingiza katika misafara ya walinganiaji dini na kujifanya na sisi tukilingania, ila lengo ni kupata unafuu wa maisha lakini tulipogundulika tulikuwa tukifukuzwa. Maisha yaliendelea kuwa ni magumu. Unapoingia mwezi wa ramadhani sisi kwetu ilikuwa ni kama sikukuu maana tuliweza kushiba kwa kufuturishwa na mabaki ya ftari kwa matajiri na wenye uwezo tuliweza kuyatumia. Ila mwezi unapoisha hali ilirudi vilevile.Basi mambo yalikuwa hivyo na masiku yakawa yanaendelea. Ilitokea sikumoja tulikosa cha kukila na tukakosa hata nafasi ya kuiba kiti chochote cha kutuingizia kipato au kutunisha matumbo yetu. Basi siku ile tuliamua kuingia msikitini na kuanza kufungua vibubu na masanduku ya sadaka pale msikitini ili kuiba sadaka. Haikupita muda tukasikia miguu ya watu wanakuja hivyo tulishindwa kuwahi kujificha na tukaamua kujifanya tunaswali. Mimi nikiwa imamu na waziri wangu huyu alikuwa ni maamuma katika swala yetu feki.Basi kundi lile likaja mpaka msikitini na walip[otuona tunaswali wakawa wanatunyooshea vidole na wengine wakawa wanasema hawa ndo wenyewe, hawa ndo wanafaa. Basi nikiwa imamu wa swala feki nilijitahidi kurefusha swala lakini wale watu hawakukata tamaa na wakaendelea kusubiri. Hatimaye nikakata tamaa na kumaliza swala ile. Basi tulipotoa salamu tu wale watu wakatuita na kutuchukuwa kwenda kwa mfalme na kutuambia kuwa mfalme anatuita.Kwakweli hatujawahi kuiba kwa mfalme hata siku moja hivyo tulipata woga sana na kuhisi leo ndo mikono yetu inakwenda kukatwa. Tulipofika kwa mfalme wale watu mmoja wao akasema “muheshimiwa mfalme tumetafuta sehemu zote kwa siku nyingi lakini tumewapata hawa, na huyu alikuwa ndo imamu na mwenzie maamuma. Bale nilitamani kumwambia sisi sio wezi lakini nikasubiri kuona hatima yetu. Mfalme alifurahi kusikia vile na akaniambia ninakuozesha mwanangu. Nilishangaa kuona mfalme anasema maneno yale mbele ya wezi. Nikamuuliza sababu ya kufanya hivyo. Mafalme akanijibu kuwa yeye hana mtu wa kumrithi na ana mtoto wa kike tu, hivyo alikuwa akitafuta mtu wa kumuoa binti yake kwa sharti kuwa mtu hiyo awe anaswali hasa awe anaswali sunnah za usiku. Hivyo watu wake hawakupata mwenye sifa hiyo ila ameniona mimi,Hapo nikamwambia mflme naomba muda kidogo, basi nikatoka nje na kuchukuwa udhu kisha nikasujudi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema alonipa. Yaani kwa swala feki ile amenipa neema ya kuwa mfalme je ingelikuwa ni swala ya kiukweli ni neema kiasi gani angenipa? Basi nikarudi kwa mfalme na kumwambia nimekubali. Na hapo ndoa ikapita na nikamuoa binti mfalme.Kuanzia pale mimi na mwenzangu tukasahau wizi na haukupita muda mfalme alifariki na mimi nikawa mfalme wa nchi hii na rafiki yangu huyu nikamfanya kuwa waziri mkuu. Hivyo kwa kuwa tunatambua machungu ya maisha tumekuwa tukijitahidi kusaidia raia na tulikuwa tukitembea usiku kuona hali halisi ya maisha na kuwatambua wezi. Huwa tukiwapata wezi tunawapa kazi ili kuwasaidi. Hivyo imetokea jana tulipokuwa tukifanya uchunguzi wetu tukapita nyumbani kwenu. Hii ndio hadithi yangu na waziri wangu.

USULUHISHAJI WA WALODHULUMIWA.
Basi baada ya kusikiliza hadithi hizi mfalme akaanza usuluhishi na kumwambia Zubeidah achome huo unywele ili amuite jini binti mfalme. Basi Zubeidah akauchoma huo unywele na baada ya punde akaja jini yule na mfalme akataka msamaha kwa mabinti walogeuzwa mbwa, basi akawambwagia maji na wakageuka kuwa watu. Pia bint mfalme akazungumza kuwa alomfanyia unyama Amina ni mwanao mwenyewe ewe mfalme ni kuwa mtoto wako alimpenda Amina na kumposa na ndoa aliifanya kwa siri na hatimaye mambo yakawa hivyo. Basi jini akaondoka.Mfalme akamuita mwanae na kumuuliza yalotokea na akamjibu kama mambo yalivyo elezwa. Basi akatoa amri mrejee mkewe na kisha Zubeidah ana dada zake akawaozesha kwa wale machongo watatu na yeye mwenyewe mfalme akamuoa Sadie. Inasemekana ndoa zao zilikuwa ni za upendo wa hali ya juu na hakukutokea ugomvi mpaka Allah akapitisha amri yake.Baada ya Schehra-zade kumaliza kusimulia hadithi hii Dinar-zade alifurahi sana. Lakini furaha hii haikumzidi sultani. Hapo Schehra-zade akamwambia basi hadithi hii haifiki hadithi ya Sinbad mwenda baharini. Sultani akuliza ni kipi kilompata sinbad mwenda baharini hata hadithi yake ikawa nzuri hivyo? Hapo Schehra-zade akaanza kusimulia hadithi hii;-SAFARI SABA ZA SINBAD
Katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo. Kijana huyu alijaaliwa kuwa na uwezo mkubwa wa nguvu za kuweza kubeba mizgo. Pia alikuwa na uwezo mzuri wa kiakili. Sinbad aliipenda sana kazi yake pia watu walimpenda kwa kuwa alikuwa akifanya kazi zake kwa umakini.Ilitokea sikumoja alipokuwa katika kituo chake cha kufanyia kazi alikuwa mtu mmoja asiyemfahamu kabisa na kumpa kazi ya kupeleka mzigo wake sehemu husika. Mtu yule alitoweka baada ya kutoa maelekezo na kumpatia pesa yake. Sinbad baada ya kupewa maelekezo aliuchukuwa ule mzigo na kuanza kuukokota kwenye mkokoteni wake kuupeleka alikoelekezwa.Njiani Sinbad alikutana na geti liliozungukwa na mauwa mazuri yenye kuvutia ndege, wadudu na wanyama kwa harufu na utamu wake. Sinbad alisimama kidogo eneo hili ili apate kushangaa uzuri ulioje wa eneo hili. Akilini alijiambia kuwa bila shaka ndani ya eneo hili kuna nyumba kubwa yenye bosi mkubwa.Sinbad akiwa katika hali hiyo alituwa mzigo wake chini na kuanza kufuta jasho lake. Alisogea kidogo kwenye geti lile na kuona ndani kuna mambo ya kuvutia. Sinbad alikuwa ni kijana mwenye adabu na heshima lakini leo alisahau mambo yote hayo na akaanza kuchungulia ndani kwa watu. Alipokuwa hatoshelezi macho yake aliamua kuingia kwenye geti lile ili aone zaidi.Sinbad hakuamini macho yake kama yanamuonesha sahihi, aliona nyumba kubwa yenye kila akijuacho kuwa kinahitajika, na aliona pia ambavyo havijui. Aliona nyumba iliyozungushiwa malumalu na lulu zikiwa zinaningi’inia kama mauwa mazuri yaliyopambwa. Rangi za nyumba utadhani ni dhahabu iliyochovywa. Kawahakika Sinbad alistaajabu sana. Kisha akaanza kuzungumza maneno yaloonesha kumalaumu mwenyezi Mungu kwa kuwapa watu wengine mali nyingi kama anazoziona pale. Pa aliendelea kumlaumu mwenyezi mungu kwa kumfanya yeye apate rizki kwa jasho jingi lakini watu wengine wapo wamekaa na bila jasho wanapata rizk.Sinbad alilalamika sana hata akasikiwa na mwenye nyumba. Basi akaamrisha aletwe, akiwa natetemeka kwa woga Sinbad alipelekwa mbelel za Mkuu wa nyumba. Kisha akamwambia akae. Sinbad hakuamini kama meambiwa akae maana alifikiri atapewa adhabu kali. Basi mkuu wa nyumba akamuuliza “unaitwa nani kijana” “naitwa Sinbad “ au Sinbad mbeba mizigo. Yule mzee akamwambia jina zuri sana na inaonekana wewe ni wajina wangu. Mimi naitwa Sinbad au ukipenda niite Sinbad wa baharini.Baada ya kutambulishana majina Sinbad wa baharini akaanza kumwambia Sinbad mbeba mizigo. “kijana nimekusikia maneno yako, ila sio kosa lako kusema maneno yale na wewe pia si wa kwanza. Kwani wapo wengi wamesema kama wewe. Sasa leo nataka nikueleze kuwa mimi sikupata mali zote hizi kwa kukaa hapa bila ya jasho. Kabla sijapata mali hizi nilipata tabu kubwa sana na pengine hakuna anayeweza kunifikia jasho na taabu nilizopata wakati natafuta malihizi”Huu ni wakatii sasa wa mimi kula na kuulia kwani mchumia juani hula kivulini. Kabla ya hapo mimi nilikuwa ni mfanya biashara wa majini yaani nasafiri visiwa mbalimbali. Utajiri wote kuu umettoka na na taabu na mashaka yalonikuta. Nilisafiri safari SABA ambazo hizo nilipata taabu kubwa sana na sito sahau. Leo nitakueleza wewe na walokuwepo hapa yalonikuta kwenye safari hizo.”Basi kabla hajaanza kusimulia Sinbad mbeba mizigo akamwambia Mkuu mimi nina mzigo wangu natakiwa niupeleke sehemu hivyo niruhusu niondoke. Palepale Sinbad wa baharini akamwambia nitakupa mtu umuelekeze apeleke yeye hiyo mizigo na nitakulipa pato la siku yako yote ila ukae na mimi leo upate kusikia hadithi saba za safari zangu saba. Basi palepale akamuagiza mtu apeleke mzigo ule na vinywaji na vyakula vialetwa. Watu wakakusanyika na kukaa tayari kusikiliza hadithi za safari saba za sinbad. Badi bila ya kuchelewa akaanza kusimulia hadithi ya safari zake kama ifuatavyo:-SAFARI YA KWANZA YA SINBAD
Tambua kuwa baba yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana katika nchi ya baghdad wakati wa utawala wa sultan harun Rashid. Baba yangu alifariki miaka 21 iliyopita nilipokuwa kijana kama wewe. Wakati huo nilikuwa na marafiki wengi sana. Na nilianza kutumia mali aloniachia baba na hatimaye akakaribia kuisha na marafiki wakanikimbia. Na hapo ndipo nilipoamua kuanza biashara za majini, yaani kuuza bidhaa sehemu mbalimbali za visiwa.Nilijiandaa vizuri kwa ajili ya safari yangu ya kwanza. Na maandaliizi yalipokuwa tayari tulianza safari ya kubiashara. Safari ilikuwa salama kabisa kwa muda wa masiku. Tulipita visiwa kadhaa tukiuza na kununua. Kwa upande wangu biashara haikuwa mbaya ijapokuwa ugeni ulinisumbuwa sana. Kwa ujumla nilifurahia safari ile. Baada ya kutembea visiwa kadhaa tuliamua kumalizia katika viziwa vingine ili tuweze kurudi nyumbani. Ilitikea sikumoja ghafla upepo ulianza kubadilika na jahazi likashindika na kudhibitiwa na manahodha.Upepo ulizidi mpaka nahodha akaamua kukiachia chombo kiende kokote, hali iliendelea kuwa mbaya mpaka bidhaa zikaanza kutumbukizwa majini ilikuokoa ualama wa maisha. Haliiliendelea kuwa mbaya hata chombo kikaanza kunywa maji. Watu wakaanza kuania rohozao, na kuanza kushika mbao zilizovunjika kutoka kwenye jahazi. Mimi nilipata mbao moja na ilinipeleka mbali zaidi ambapo sikuweza kuona hali za wenzangu kilicho endelea.Kwa upande wangu mawimbi ya maji yalinipeleka mbali sana, nikiwa nimeshikilia tawi lile hata sikusubutu kuliachilia. Nilipofika hali ambapo sijielewi kwa kuchoka ghafla nikaona kunaweupe mbele yangu, kuangalia vizuri kilikuwa ni kijisiwa kidogo. Basi nikajitahidi kujizuia huku nikawa naiba maji ili yanipeleke kule. Kwa bahati njema kaupepo kakanipeleka kwenye kisiwa kile. Kwa msaada wa mizizi ya miti niliweza kutoka kwenye maji yale.KISIWA CHA UOKOZI
Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli. Na kwa kuwa miguu yangu haikuwa na nguvu nilibuluzika tu. Nililala bila ya kijitambua niliamshwa na maji yaliyokuwa yakinipiga miguuni kumbe maji yalikuwa yanajaa. Haukupita muda ghafla nikaona kuna kijahazi kinaingia kikiwa kina mifugo kadhaa. Walipofika pale kisiwani wakawafungulia mifugo yao na kuanza kuwaosha na kuwapaka dawa. Mmoja wao akaenda mbali kidogo akaja na majani mengi sana na kuanza kuchagua baadhi ya ng’ombe na kuanza kuwapa majani yale.Niliwafuata na kuwaomba msaada wa chakula. Wakanipa maziwa na mkate wa nyama. Nilipomaliza kula wakaniuliza habari yangu na eneo lile na nikawaeleza kila kitu. Basi wakaniambia kama ungekuja kesho usingetukuta na pengine ungefia hapa maana hakuna majahazi yanayokuja hapa ila ni sisi tu na huchukuwa miezi 3 ndo tunakuja tena. Na kisiwa hiki hakina chakula, hivyo pengine ungeishia kufariki hapa. Basi wakanipatia na nguo na nikawauliza pia sababa ya wao kuja hapa na ni kinanani wao.Mkubwa wao akanieleza kuwa wao ni watumishi wa mfalme aliyepo karibu na eneo hili. Mfalme huyo amekiteua kisiwa hiki kama eneo la kutibia mifugo yake na amepanda majani maalumu kama dawa ya mifugo yake. Hivyo eneo hili hawaruhusiwi watu wengine hapa. Basi walipomaliza shuhuli zao walifunganya mizigo yao na kuchukuwa majani mengi na nikaondoka pamoja nao.

Tulipofika kwenye utawala wao wakanipeleka kwa mfalme wao na nikamueleza mimi ni nani na nini kazi yangu na kumueleza kuwa natokea baghdada nchini kwa sultan Harun Rashid. Basi mfalme yule nikamueleza mengi kadir alivyouliza na mimi sikuwacha kuu;liza mambo kadhaa. Kwa haraka zaidi mfalme yule alionekana kunipenda sanan na kunikubali. Basi alinifanya katika watu wa karibu yake na ni kama mshauri pia. Niliishi pale nikawa nafanya biashara chini ya mfalme yaani nilikuwa naendeleza bishara za mtoto wake wa kike.Siku moja niligundua kuwa kuna kisiwa jirani ambapo kunasikika sauti za furaha kila siku. Nilipouliza nikajibiwa kuwa ni kisiwa jirani huwa wannafanya sherehe kila wanaporudi kutoka kutafuta lulu. Hicho ni kisiwa pekee kinachofahamika kwa kuwa ni wafanyabiashara wa lulu. Basi kwa kuwa sikuijua lulu ilibidi niumuombe ruhusa mfalme ili na mimi nikashuhudie sherehe zao na nipate kuijua lulu. Mfalme alikubali na akanipa msafara wa wafanyakazi wake waende pamoja nami.Tulipofika kule nilifurahi kuiona lulu kwa mara ya kwanza na nikafurahia pia sherehe zao. Basi katika hali kama zile nilishangaa kuona kuwa watu wanashusha mizigo kutoka bandarini lakini katika ile mizigo kuna ambayo imeandikwa Sinbad, nilipoangalia kwa uzuri nikagundua kuwa nahodha wa lile jahazi alikuwa ni yule nahodha wetu. Hivyo kumbe zile mali zilikuwa ni zakwangu na lile jahazi lilikuwa ni lile letu. Nikamuita kijana mmoja na nikamuuliza habari zao na akanieleza kuwa walibahatika kuliokoa jahazi lao na watu wote walipona isipokuwa Sinbad ndo hakuonekana. Kijana huyu alizungumza bila ya kunijuwa kama ndo mimiBasi nikamfuata nahonda na kumueleza kuwa mimi ndo Sinbad na zile mali ni za kwangu. Basi nahonda alliponiona akanikumbuka na kutoa machozi kwa furaha maana walifahamu kuwa nimekufa. Nahodha akanikabidhi mali zangu na nikaziuza, nikapata habari kuwa jahazi letu litarudi Baghdad wiki ijayo. Nilichukua bidhaa zangu na kuuza baadhi na kurudi kwa mfalme na baadhi ya bidhaa. Nikamuelezea kilichotokea na alifurahi sana kwa kupata bidhaa zangu. Na hivi ndo Mwenyezi Mungu anavyowafanyia watu wenye subira.Nikampatia mfalme bidhaa zilizobaki kama zawadi na nikamuomba ruhusa ya mimi kurudi nyumbani kwetu wiki ijayo. Kwa majonzi na kinyongo mfalme aliniruhusu na hata binti yake alikuwa na majonzi sana lakini haina budi “milima haikutani binadamu hukutana” ni maneno nilojisemea moyoni. Basi wiki ilipoisha mfalme alinipatia mali nyingi sana kama zawadi. Nilipata pia lulu kutoka kwenye kisiwa kile. Kwa hakika katika safari hii nilipata taabu na faida kubwasana.Tulipofuka Baghdadi niliwaelezea ndugu zangu habari ya yalonikuta, kwakweli waliniambia niwachanena habari za biashara hii. Hata mimi nikajiapiza kwa yalonikuta kwa hakika sitarudia tena bishara hii. Basi nikatoa sadaka kutoka katika faida yangu na nikatoa na zaka muda ulipo fika. Nilitumia faida ile kujiendeleza kibiashara hata miezi mingi ikapiata. Nilisahau kabisa yalonikuta kwenye safari ile. Baada ya muda nahodha wetu wa mwanzo nilikutana nae, na katika mazungumzo yetu alinieleza kuwa wanatarajia kuanza safari wiki ijayo.Kwa hakika nilivutiwa tena na biashara ile. Na kwa kuwa nilisahau machungu yalonikuta katika safari ya kwanza nikaazimia kuanza safari ya pili wiki ijayo. Mpaka kufikia hapa Sinbad kwa baharini akamaliza kusimulia hadithiya safari yake ya kwanza. Na kwa kuwa muda ulukuwa umekwenda hakuweza kuanza hadithi ya safari yake ya pili. Basi akampatia Sinbad mbeba mizigo zawadi nyingi na pesa kadhaa ya kutumia kama fidia ya kuvunja kazi zake. Na akamuahidi kesho awahi kuja maana safari ya pili ina mambo mengi na makubwa zaidi kuliko ya kwanza.SAFARI YA PILI YA SINBAD
Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi. Walipokusanyika watu wote vikaagizwa vinywaji na vileja na kuanza kula huku wakisikiliza hadithi. Sinbad wa baharini akaanza kusema “basi tambueni kuwa sfari hii ya pili nilikutwa na makubwa zaidi kuliko hii ya kwanza. Ha ilikuwa hivi:-Basi tulipozungumza na nahodha kuwa wiki ijayo wataanza safari nilirudi nyumbani na kujiandaa kwa safari. Ndugu zangu walijaribu kunizuia lakini sikuwasikia “sikio la kufa halisikii dawa” wengine wakanambia najipeleka nikafe ila sikuwasikiliza. Maandalizi yalikamilika kwa siku mbili na nikawa nasubiria safari tu. Wiki ilipofika tukaanza safari kwa amani lakini siku ya tatu kabla ya kuingia kisiwa cha kwanza kufanya biashara hali ya hewe ikabadiliki ghafla.Nikiwa na woga sana juu ya roho yangu nikabaki namuomba msamaha mwenyezi Mungu. Jahazi lilikwenda ovyo ovyo kwa muda wa masaa sita. Manahodha walifanya wawezapo hata wakaamua sasa kuachia hatima kwa Mwenyezi Mungu. Abiria tulianza kutapika na mimi nikiwa mmoja wapo. Kwamuda kadhaa nilipotelewa na kumbukumbu na sikufahamu zaidi. Nilikuja kupata fahamu chombo kilianza kutulia mbele yetu kukiwa na weupe kwa mbali. .Nilikaa vizuri nipate lujua kinachoendelea. Manahodha walituambia kuwa kwa sasa tunaingia kisiwa cha roc. Kisiwa hiki hakuna wakazi na wanyama pia hakuna au ni wachache. Kuna hadithi ya zamani sana walokuwa wakisimulia mababu kuwa kuna roc aliyekuwa akila mali za watu kama mifugo na kujeruhi wakazi. Hivyo watu wamehama kisiwa hiki. Ni miaka mingi sasa na ni mababu tu wanasimulia hadithi hii. Huenda ni ngano tuu au ni kweli. Hivyo tutaingia hapa kwa ajili ya kupumzika kidogo na kuangalia kama tutapata maji maana safari ni ndefu.
Basi tukaingia kisiwani pale na kuanza kuranda randa. Kwakuwa nilitapika sana sikuwa na nguvu za kutosha hivyo nikaelekea kwenye kivuli kikubwa na kujilaza. Nililala sana na nilipokuja kuamka sikuona watu wala jahazi. Kumbe nilisha kimbiwa, niliogopa sana na nisijue nitatokaje pale kisiwani ambapo hakuna watu wala chakula. Nilianza kujuta kwa kukubali kuja. Nilijua sasa hapa kisiwani nitakufa pekeangu kwa kukosa chakula.Nilianza kukizunguka kisiwa chote kujua nini nitafanya. Jua nalo lilikuwa likizama. Katika kuzunguka nikaona kuna kitu cheupe kwa mbali. Nikaanza kukifata taratibu na nikakuta kama limpira kubwa sana na laiiini. Kuangalia vizuri sikufahamu nini kitu kile. Ghafla nikaona anga inafunikwa na kuna kivuli kikubwa kinaingia nilikimbia kwenda kujificha. Kumbe alikuwa ni ndege roc mkubwa sana yaani mguu wake mmoja ni kama shina la mti. Kumbe lile dude kubwa jeupe ni yai lake.Basi kiza kilipoingia nilikwenda karibu na ndege yule nikavua kanzu yangu na kufifunga vizuri kwenye miguu ya yule ndege. Niliamini kuwa akiruka atanibeba na kunitoa kwenye kisiwa kile. Basi nilifanya hivyo na kuendelea na imani yangu hiyo. Mambo yakawa kama nilivyotaka asubhi ndege yule aliruka na kunibeba, kwa kuwa sikuwa mzito sana hakujua kama amebeba kitu lamda alijua ni guo tu.KUELEKEA BONDE LA UOKOZI
Alinibeba akapaa angani sana hata sikuona ardhi. Alikwenda kwa muda wa dakika 30-50 na akatua kwenye bonde lenye milima. Alipotua nikajifungua na kwawoga alishituka na kuniacha pale. Nikaondoka kwa haraka na kujificha asijeniona. Muda haukupita roc alikamata nyoka mkubwa sana na kumkata vipande. Alimla na kuondoka na kipande. Alipoondoka na mimi nikatoka mafichoni pale na kuanza kuchunguza eneo lile na kujua vipi nitatoka pale.Nilipochunguza zaidi eneo lile nikagungua ni bonde lililopochini sana na limezungukwa na milima mirefu yenye mawe. Ni bonde ambalo katu mtu asingeweza kutoka. Mchana mzima nilikuwa nikitafuta pa kutokea lakini bila mafanikio. Japo nilikuwa najishauri kuwa bora hapa kuliko kule kisiwani. Usiku ulipoingia nilijificha kwenye mapango na kulala. Usingizi haukuja kabisa kwa woga. Kwani uksiku nyoka walokuwa wakiogopa mchana kuliwa na roc walikuwa wakitoka kutafuta chakula.Muda wote nilikuwa nikimuomba Mungu dua aniokoe na wadudu wabaya usiku ule. Mwenyezi Mungu alinilinda na ulipofika asubuhi nikaendelea na uchunguzi wangu wa eneo lile. Kwa ghafla nilishituliwa na kishindo nyuma yangu. Nilipogeuka nikakuta ni kipande kikubwa cha nyama. Nyama. Hapa nikakumbuka hadithi ya zamani sana juu ya bonde la wawinda madini. Wazee wetu walikuwa wakitusimulia kuwa kuna watu wanawinda madini kwa kutumia nyama. Yaani wanatupa nyama kwenye bonde lenye madini, kisha nyama ile inaganda vipande vya madini na pindi ndege wanapokuja kuchukua nyama ile ambayo ina madini yaloganda kutoka bondeni huwakimbiza ndege wale na wanapoidondosha wanachukua madini.Pale nikawa nawaza huende hii ikawa ndio njia pekee ya mimi kutoka pale. Nikawa naangalia kama nitaona mtu lakini sikuweza kuona kwani juu ni mbali sana. Basi nikaamza kuokota madini mapande makubwa makubwa. Eneo lile lilikuwa na madini mengi na makubwa yalokuwa waziwazi. Niliokota almasi na dhahabu kwa wingi pamoja na madini mengine. Nilipomaliza nikayafunga kwa uzuri sana na kuanza kutengeneza mpango wa kutoroka pale nilipofungwa.Kwakuwa mapande ya nyama yalokuwa yakitupwa yalikuwa ni makiubwa sana, nikachagua lile kubwa zaisi na kujifunga nali na kujificha kwenye kanzu yangu. Baada ya muda ndege mkubwa sana alikuja ndege aina ya eagle. Ndege yule ana watoto hivyo alichagua pande kubawa na kuondoka nalo. Pande hili ndo lile ambalo nipo. Alinipeleka mpaka kwenye kitundu chake. Na haukupita muda watu wengi wakatokea na kuanza kumtisha ndege yule na kunidondosha mimi na nyama ile.Kumbe wale wawinda madini kila mmoja alikuwa na kitundu chake, hivyp walishangaa baada ya nyama anatoka na mtu. Niliwasimulia yote yalonopata. Walinipa pole lakini kwa kuwa nilikuwa na madini mengi sana yule mwenye kitundu chake nilimwambia achukue kiasi anachotaka na akachukua pande moja tu. Kisha akaniachia mengie, nikawagawia na wenzie. Tulikaa eneo lile kwa muda wa wiki tukiwinda madini na baada ya hapo tukaanza kurudi baghadadi, kwa kuwa na wale walikuwa wakiishi bafhdad ila hatukuwa tukijuana kwa kuwa ni wa mji mwingine.Njiani tulipita misitu mikubwa na yakutisha, tulipishana na manyoka wakubwa sana hata tukafika ufukweni na nikauza baadhi ya madini yangu kwenye kisiwa cha Balrora. Nikanunua pale bidhaa kadhaa na zawadi za kupeleka nyambani. Siku tatu baadae tulipanda jahazi la kuelekea baghadad na tulipofika kwanza nikaanza kutoa sadaka na zaka mali zangu na nikawasimulia ndugu zangu yote yaloniptata. Walinipongeza sanana na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunirudisha salama.
Nilikusanya watu na kufanya dua na kutoa sadaka zaidi kama ni shukrani yangu kwa msaada alonipa mwenyezi Mungu hata akanirudisha salama. Niliamua sasa kutofanya biashara nyingine za baharini na kuanza biashara ndogo ndogo. Nilifanya hivi kwa muda wa miezi sita, huku nikawa nafatilia habari za wasafiri. Muda wote huo sikusikia ajali yeyote na walikuwa wakinisifia faida walokuwa wakizipata. Nilivutiwa zaidi na nikasahau machungu yote yalonipata. Nikaamua kuanza safari ingine ya tatau.Baada ya kumaliza hadithi hii Sinbad wa baharini akampatia Sinbad mbeba mizigo kiasi cha pesa kama ni fidia ya kupoteza muda wake wa kazi na kusikiliza hadithi yake. Kisha akamuahidi kesho awahi ili ajepata yalomkuta safari ya tatu. Akawaambia watu wote walokuwa pale kuwa kesho wawahi maana safari hii amekutwa na mengi ya kustaajabu. Basi watu wote wakatawanyika pale na Sinbad wa baharini akaingia ndani kwake.SAFARI YA TATU YA SINBAD
Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao. Alipofika alikuta watu wote wamekusanyika tayari wanamdsubiri yeye. Alipofika vinywaji viliagizwa na vyakula laini. Watu wakaanza kuburudika, na baada ya muda mzee Sinbad akawasili na kuaza kusimulia safari yake ya tatu kama ifuatavyo:-Basi niliamua nisafiri tena kwa mara ya tatu, nikafuatilia taarifa za kuwa jahazi linaondoka lini na wapi. Nilikusanya bidhaa za kwenda kuanza nazo na maandalizi nilikamilisha kwa muda wa wiki nzima. Siku ya safari ilipofika ndugu zang walinisaidia kupeleka mizigo baharini. Walinisaidia na kupandisha pia huku wakinishawishi nisiende. Bila ya kujuwa kitakachonikuta nilikataa ushauri wao na kujitetea kuwa kwa miezi sita sijasikia ajali yoyote iwe leo kisa mimi nimo?.Tulisafiri salama katika visiwa kadhaa na safari ilikuwa ni njema kwakweli. Tulifanya biashara visiwa kadhaa na kuona faida na matunda ya biashara. Hapa nikawa najuta kwa nini sikufanya biashara kwa muda wote huo. Tulikubaliana tuendelee kidogo kufanya biashara kisha turudi nyumbani baada ya siku kadhaa. Ijapokuwa nilipenda tuendelee lakini mawazo ya wengi sikuyakatalia. Basi tukaendelea na visiwa kadhaa hata kukaelekea kwenye kisiwa cha mwisho ili tugeuze. Kwa jumla tulikuwa watu 48 wafanya biashara pamoja na manahodha na wasaidizi tulikuwa jumla ya watu 60.Tulipokuwa tupo kwenye bahari tukielekea kisiwa kile ghafla nahodha alipoteza uelekeo na kutuambia amepotea na yupo kwenye kisiwa cha maharamia vibushuti. Hatukuelewa nini anazungumzia lakini alifafanua zaidi ni watu wafupi wanaotembea kwa makundi. Kazi yao ni kupora majahazi. Basi haukupita muda tukawaona wanakuja, nahodha aliongeza kuwa kupambana nao kwenye maji hatuwezi ila tukienda nchi kavu hawatakuja.Nahodha alijitahidi awezavyo awahi kufika nchi kavu kwenye kisiwa kinachoonekana jirani. Hakuwahi kufanya hivyo tukavamiwa na jahazi letu likachanywa na kukatwa katwa na nanga ikakatwa. Walipora mali zetu zote na tukakimbilia kwenye kisiwa kile. Tukiwa tukihangaika nini tufanye kuondoka pale tukaona kuna jumba kubwa sana mbele yetu. Bila ya kujuwa kama ule ni mtego mwingine tukaingia kwenye jumba lile na kuanza kufanya mipango.Usiku ulipofika tukaamua kujisitiri mule. Kumbe jumba lile ni mtego wa majidude yanayokula watu. Wanavizia wasafiri wanapopata matatizo na kuporwa wakiingia mule wananafungua na kuwala. Basi usiku ule likaja jitu moja kubwa sana na refu pia. Kwa urefu alonao nilimfikia magotini na upana wake lamda tujipange saba kama mimi. Ukiangalia ukubwa wa jumba lile utaamini ukubwa wa alolijenga.Basi limtu lile lilipoingia likafunga mlango na kukoka moto. Tukiwa tumetulia sana hatujui tufanye nini, lile limtu likaamza kumshikamshika kila mmoja. Likamkamata nahodha mkuu na kuanza kumbanika. Kumbe lilikuwa likiangalia mtu alionenepa amle. Alimbanika nahdha wetu na kuanza kumla. Alimla wote kisha akalala fofofoi. Kila mmoja alikuwa akitetemeka na kuanza kulia na kuogopa.Lile limtu likalala pale mpaka ilipofika karibu na alfajiri likatoka na kuacha mlango wazi. Tulikaa pale ndani na baada ya muda tukatoka. Tulipofika nje tukaanza kupiga mipango ya kuondoka. Tulizunguka kisiwa kile kutafuta pa kulala lakini tulikosa. Tukiwa katika hali ilie nikapata wazo la kuwa tutengeneze mitumbwi midogomidogo. Tukaanza kufanya kazi ile hata usiku ukakaribia kuingia. Nikawashauri wenzangu kuwa tumuuwe yule mtu au tumtoboe jicho lake. Maana alikuwa najicho moja tu. Nikasisitiza kuwaambia kama tutamuuwa ndo tutaweza kuondoka hapa bila hivyo atatufuata na wenzie.Tukapanga mpango wa kumuuwa na mimi nikiongoza mtego. Usiku ule tukaingia mule ndani na tukajifanya tumelala. Lile limtu likaingia na kuanza kumpapasa kila mmoja ili achukuwe alonona amle. Alimchukua nahodha mwengine alokuwa amenenepa zaidi katika sisi. Basi akambanika pale tukiwa tunamuona. Uchungu ulinishika lakini niliendelea kusubiri alale. Alipolala tu nikaweka msumari wa moto kwenye mato na ukaiva vizuri hata ukawa mwekundu sana. Baada ya muda nikawdokoa wenzangu kuwa mambo tayariNilimfata yule limtu na kumchoma na msumari ule kwenye jicho lake. Alilia sana na kuguta makelele. Alikwenda kukaa mlangoni ili atukamate. Kwakuwa alikuwa ni mrefu sana tuliweza kupita kwenye magoti yake hata bila kutupata. Tukaenda kwneye mitumbwi yetu na kuanza kuimalizia kwa msaada wa mbalamwezi. Lile limtu likaelekea sehemu huku linalia. Muda le kwa haraka zaidi tukamaliza mitumbwi yetu na tukagawana waiwi wawili kila mtumbwi.Baada ya kugawana tukaanza kuingia maji kila mmoja anajitahidi kuenda kwa haraka kiasi awezavyo ili kuweza kuondoka kisiwa hiki. Basi baada ya jua kuchomoza tulikuwa mbali kidogo lakini tukashangaa tunaona weupe unakuja. Kumbe lile limtu lilikwenda kuwatafuta wenzie wengi wakiwa wamebeba mawe. Kwa urefu wao walianza kuyaingia maji na kuanza kuturushia mawe. Wenzetu walokuwa nyuma walizama kwa mawimbi ya maji baada ya kurushiwa majimawe makubwa. Mwshowe mitumbwi miwili tu iliokoka wakwetu na wawenzetu, hivyo tukawa wanne tulookoka.Tulikwenda bila ya kujua wapi tutaishia, kwa bahati tukaona kisiwa kwa mbele zaidi. Tukaingia kwenye kisiwa kile na kunanza kutafuta chakula. Tukapata matunda na maji. Tuliandalanda pale na ilipofika jioni tulilala chini ya mti. Kwa ghafla usiku alikuja nyoka mbubwa sana na akamchukuwa mwenzetu aliyekuwa pembeni amelala. Tukaogopa sana maana tumeokoka kule kwenye mawatu na sasa ni nyoka. Kwa hakika usingizi haukuja tena.Ilipofika asubuhi tulitafuta njia ya kurudi bila mafanikio basi nikawashauri wenzangu tutengeneze kitundu cha miiba tulale. Basi tukakusanya miiba mingi na kutengeneza kitundu.yule nyoka alipokuja usiku ule alizunguka kwenye miiba bila ya mafanikio. Baada ya muda alipata kaupenyo ka kuingia na akamchukuwa mwenetu mwingine. Pale tukabaki wawili tu. Asubuhi tukawatunajishauri la kufanya, bila mafanikio tukabahatisha kupata matunda machache ya kula tu.Tukaamua kutengeneza kitundu juu ya mti na chini tuzungushe miba ili ashindewe kupanda. Tukafanya vile na ulipofika usiku alizunguka sana nyoka yule na aipate pa kuingia. Aliruka na kuivunja miba ile na kupanda juu na kumchukiwa mwenzangu pale nikabaki peke angu. Asubuhi ilipofika nikazunguka sana kisiwani pale na nikakuta sehemu kuna kimfereji cha mguu mmoja. Nikakivuka na kukutana an kisiwa kingine. Yule nyoka alishindwa kuja kule kwa sababu ya maji ya chumvi ambayo yangemuuwa kama angejaribu kuyavuka. Nilitembea huku na kule na kufika sehemu kuna kijibostani kizuuri. Nikawa nakula matunda. Kwa mbali nikaona kuna kibibi kizee kinaniita kwa ishara.Nikaenda pale nikakikuta kibibi kinataka kuvushwa kwenye mfereji. Nikakibeba, ila mara tu baada ya kukibeba kikatia makucha yake kwenye mbavu zangu na kuganda. Kikawa kinaninyonya damu. Nikikaa pia habanduki, nilijitahidi kadiri niwezanyo lakini hakutoka. Nilichoka sana na nikaanza kupoteza nguvu na kukonda zaidi. Siku ya tatu nikatengeneza pombe kwa kutumia mizabibu na ilipokkuwa tayari nilimreburebu hata akakubali kunywa. Alipolewa aliachia na kuanguaka na hapo nikamkimbia.Nilizunguka sana na mida ya mchana nikaona jahazi kwa mbali, hapo nikavua shati langu na kuashiria wajeniokoa. Walipokuja nikawasimulia habari yangu. Wengi walinipa pole na wengine wakanambia bahati yangu ila ningekufilia mbali. Wakanichukuwa na kuenda nao na safari yao. Tukafika sehemu kuna kisiwa, yule nahodha akanambia shuka ukafanye kama watu wanavyofanya. Nikaendanao watu wa jahazi lile mpaka kwenye kisiwa kile. Basi wakaokota mawe mengi sana wakawa wanawapiga nyani waliopo kwenye minanzi.Nikaokota mawe na kupiga na mimi, basi kila nikimpiga nyani kwa jiwe ananirudishia kwa kunipiga na nazi. Basi nachukuwa nazi ile na kuiweka kwenye mizigo yangu. Niliweza kupata nazi mia sita. Mizigo ya watu ilipoenea tukaondoka na kwenda kisiwa kingine na kuuza bidhaa zile. Nilipata faida kubwa kuliko ile ilopotea kwenye maji. Baada ya hapo nikanunua bidhaa na tukaendelea kufanya biashara visiwa kadhaa na tulipofika karibia na baghadadi nikashuka na kurudi kwetu kwa majahazi yanayokwenda BaghadadiSafari hii nilipata faida kubwa lakini nilipatwa na makubwa zaidi. Nilikuta ndugu zangu wakilia pindi nilipowaelezea kilichonikuta. Nilitowa sadaka mali yangu na kuendeleza biashara zangu. Niliogopa tena kufanya biashara za majini. Ijapokuwa uwoga huu unanipata kwa muda ila huenda nikasahau. Na hivi ndivyo huwa sikio la kufa halisikii dawa. Miezi kadhaa ilipita na niliposikia msafaa wa biashara unatoka baada ya siku 12 nilijifunganya na mimi niweze kutoka safari ya nne.
Mpaka kufika hapa Sinbad wa baharini akamaliza msafara wake wa tatu na kumpatia Sinbad mbeba mizigo pesa kiasi kwa kufidia kazi zke. Akamuahidi awahi kesho maana safari ya nne alikutwa na hatari na mambo makubwa zaidi na alipata faida pia.SAFARI YA NNE YA SINBAD
Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Tulianza safari ile usiku hata ikafika asubuhi tukiwa katikati ya maji. Njia ya safari hii sikuwa na uzoefu nayo na niliona mambo mapy. Niliweza kuona majabali yalofanana na watu, wanyama na vitu mbalimbali. Pia tuliweza kuona mawe ya ajabu ambayo huwa hayapati maji sikuzote. Tukiwa karibu ya kuingia kwenye kisiwa chetu cha kwanza kwa ghafla tulivamiwa na majiwatu makubwa na yenye nguvu sana.Watu hawa walifanikiwa kututeka sote tuliokuwa mule ndani ya jahazi lile. Walitukamata wote na kutufunga kamba na kutuziba macho yetu kwa vitambaa hata tusione wapi tunakwenda. Walitupeleka tusikokujuwa na kwa kuelewa tu niliona kama tunarudinyuma. Waliturudisha nyuma kwa muda wa takribani masaa matatu kisha tukaelekea upande wa kushoto na kukiwacha kile kisiwa tulokuwa tukikiona kuliani. Tulikwenda kwamuda wa takribani masaa sita. Nikiwa nachukuwa hisia juu ya safari ili niligunduwa kumbe wanatuzungusha tuu lakini tunatupeleka pale kwenye kisiwa kile tulichokiona.Hatimaye tukawasili na wakatufungua machoyetu na hapo nikapata tena kuona ardhi nzuri yenye udongo mweupe wa kupendeza. Wale watu wakawa wanagawana kila mmoja kucukuwa watu kadhaa katika sisi. Waligombaniana watu wote na kubakia mimi. Walichelea kunichagua kwa sababu nilikuwa nimekonda sana. Basi akatokea mzee mmoja wa heshima katika wao akanichukuwa. Basi wote tuliingizwa kwenye jumba moja na kuletewa chakula kilichofanana na machicha ya nasi. Bila ya kuchelewa wenzangu wakaanza kula chakula kile ila mimi nikachelea kukila hata kikaisha.Baada ya muda tukaletewa majani mithili ya majani ya miwa lakini haya yana maji mengi na ni matamu sana. Mimi sikuyala kwa kuhofia usalama wangu. Niliweza kugunduwa ladha yake kwa kuhadithiwa na wenzangu. Nilikaa na njaa kwa muda wa siku mbili hata nikakosa nguvu. Yule mzee akamiletea samaki wa kuchoma pamoja na mayai ya kasa. Nilikula sana hata nikashiba. Nilipopata nduvu ziku ya tatu nikaona mabadiliko kwa wenzangu. Walikuwa wakinenepa sana kwa ghafla kila walipokula vyakula vile. Kitu cha kushangaza wakawa wanapoteza kumbukumbu na kuwa na akili ya kinyama kinyama.Hali iliendelea hivi kwa muda wa wiki tatu hata akawa mmoja kati ya wenzangu hawezi kupita kwenye mlago kwa unene. Basi wale watu wakawa wanamchukuwa mtu mmojammoja kila wiki na kuondoka nae na asirudi. Nikawa nafatilia nini kinaendelea hata nikagunduwa kuwa wanakwenda kumchinja na kumuuza nyama kwenye kisiwa kingine. Niolijaribu kuwaeleza wenzangu lakini wamekuwa wanyama hakuna walijualo zaidi ya kula tu. Mimi niliendelea kula vyakula kwa kuiba na hali yangu ikazidi kudhoofu.Yule mzee akaamuwa kunitoa bandani mule kwa kuamini nikiwa huru naweza kunenepa. Hali iliendelea hivyo hata nikapewa funguo ya kuwalinda wenzangu. Waliendelea kuchinjwa hata wakabakia watu kumi na mbili. Kuna siku kulikuwa na sherehe na watu wakaondoka na kuniacha mimi na yule mzee. Basi nilitoroka pale peke angu kwani ningemhukuwa yeyote asingekubali na kwa unene na uzito alonao asingeweza kukimbia hata kidogo. Basi nilitoroka kwenda mbali zaidi.KISIWA CHA UOKOZI
Nilikwenda mpaka nikakuta misitu minene na nisijuwe pa kuenda. Kwa ghafla nikasikia sauti za watu wanaowinda na kwa uchovu nilonao nilianguka chini na kwa njaa nilonayo nilipootelewa na fahamu. Hapo sikujuwa kilichoendelea hata nikashituka nipo kwenye kitanda safi na pembeni kuna binti mzuri ananiwekea chakula tayari kwa kuniamsha ili nipate kula chakula. Bila hata kujaribu kuniamsha niliamka kwa upole na kumuuliza swali “eti unaitwa nani, na nimefikaje hapa?”. “naitwa ‘Aisha ni mtoto wa mfalme, umeokotwa porini na baba alipokuwa akiwinda”. Ni maneno aliyoyasema bint Aisha mtoto mfalme.Nikanawa maji tayari kwa kuanza kula, baada ya muda wa dakika takriban 10 aliingia mfalme, na nilimtambua kwa mavazi yake. Baada ya utambulisho nikawaelezea kila kilichonikuta. Na akazungumza kuwa kwa uda wa miaka 10 wamekuwa wakikitafuta kijiji hiko bila mafanikio. Inadaiwa kuwa wakazi wa kijiji hiko sio watu wa kawaida hivyo walishangaa kuniona mimi nimeweza kutoroka kwenye kijiji kile kisichofikika. Basi mfalme aliniuliza mengi kuhusu Baghadad na bila kusita nikawa namjibu kwa uwazi kabisa. Kwa hakika alivutiwa sana na majibu yangu.Mfalme alinitambulisha kwenye baraza lake na kunifanya mimi mmoja ya washauri wake na watu wa karibu. Niliishi pale kwa muda wa wiki moja hata siku hiyo baada ya swala ya magharibi nikasikia mlango unagongwa. Nikaenda kufunguwa nikamkuta mfalme na mkewake. Kwa heshima kubwa nikawakaribisha na walionesha uso wa furaha hata nisiijue sababu ya ujio wao. Baada ya kuwapatia maji ya kunywa mfalme akaanza kuzungumza.“mwanangu, ujio wetu hapa mimi na mama yako ni kutaka ushauri wako. Kama ujuavyo sisi tuna mtoto mmoja tu naye ni wa kike. Pia binti yetu ameonesha kuvutiwa sana na wewe. Hivyo tumekuja kukuomba uwe mkwe wetu na mrithi wa utawala huu baada ya kufa kwangu”. Kimoyoni nilifurahi sana japo nikamwambia mfalme “nashukuru sana kwa maneno yako baba yangu mtukufu mfalme. Naomba muda nifikirie na nitakujibu baada ya mshuko wa swala ya ijumaa keshokutwa in shaa Allah” Basi mfalme akakubali kunipa muda ule na kuondoka.Nilitafakari sana nini nifanye na nikikubali kuoa pale nitaondoaje kwenda Baghadad. Nitakuwa mkwe na mtoto wa kiume wa mfalme, na nitatakiwa kuurithi ufalme ule, hivyo ndoto zangu za akurudi nyumbani zitakuwa zimekwisha. Siku ilofata asubuhi nikaenda kwa rafiki yangu ambaye mkewe alikuwa akiumwa na tumbo. Nikaenda kumuomba ushauri lakini nikamkuta analia sana. Sikuweza kumuomba tena ushauri badala yake nikamuuliza kinachomliza zaidi. “rafiki yangu, tambuwa kuwa katika nchi yetu hii, akifa mke mume atazikwa pamoja na mkewe akiwa hai, na akifa mume mke atazikwa na mkewe akiwa hai. Hivyo nalia kama mke wangu akifa na mimi ndo mwisho wangu.Niliposikia maneno yale pale moyo wnagu ulipasuka na kudunda haraka. Nikaanza kutetemeka miguu na meno. Jasho jingi lilinitoka japo kulikuwa na baridi wakati ule. Yote hayo yalitokea nilipokuwa nawaza nni nitamjibu mfalme. Maana nikikubali kuoa nikifa mimi wa kwanza sio taabu ana ila akitangulia kufa mtoto wa mfalme nitazikwa pamoja naye nikiwa hai. Mawazo haya yaliniumiza sana hata nikakosa hamu ya kula kabisa. Jioni ile mmnikapita nyumbani kwa mfalme na kumkuta binti yake akiumwa eti amekataa kula mpaka asikie jibu langu kwanza.Hali ile ikazidi kuniogopesha zaidi pale niliposikia kuwa binti mafalme ameahidi kujiuwa kama nitamkataa. Nikaogopa zaidi niliposikia hivi. Nilijihisi uchovu na nikaelekea nyumbani kulala. Siku ilofata ilikuwa ndio siku ya ijumaa ambapo mfalme nimemuahidi kumpatia jibu juu ya kumuoa mwanae. Niliamka mapema sana siku ile na kuoga kisha nikaenda msikitini na kuwahi mstari wa mbele. Niliswali rakaa mbili na kufanya istikhara yaani kumuomba Mungu anipe majibu ya maswali yangu.
BINTI WA NDOTONI.
Baada ya kufikiri kwa kina na kumuomba mungu nilipitiwa na usingizi. Niliwa usingizini nikaota ndoto ya ajabu sana. Nilipokuja kuamka niliona watu ndo wanaanza kujaa msikitini lakini mfalme bado hajafika. Nikaanza kujiuliza maana na tafasiri ya ndoto ile ya ajabu. Nikiwa katika hali ya mawazo nilikuwa nikikumbuka machache kuhusu tafasiri za ndoto. Nikaanza kuichambua ndoto yangu nilioora. Nikiwa kwenye mawazo hayo nikaona kama kuna mtu amekuja na kuniuliza kuhusu ndoto yangu ili anitafasirie.Nimeota nipo safarini na binti mfalme akiwa kwenye safari ile. Tukiwa tupo kwenye jahazi kwa ghafla tulipatwa na ajali. Mule kwenye jahazi lile hakuna mtu ninayemjua asipokuwa ni binti mfalme tu. Katika ajali ile jino lanhu moja liling’oka na nikatumbukia ndani ya maji. Binti mfalme akaja na kamba na kunirushia nikaikamata kamba ile na kufika kwenye mbao kubwa ambayo binti mfalme alikuwemo. Kwa bahati mbaya bint mfalme aliteleza kwenye mbao ile na kuingia kwenye maji, niliwa sijui uogelea nilijitahidi kumuokoa bila mafanikio na akaniashiria kuwa niondoke niendezangu. Baada ya hapo nikashitukaKatika hali kama hiyo yule mtu akanieleza kuwa ndoto ile ni ya ukweli na kunajambo ninaelezwa kwenye ndoto ile. Yule mtu akaanza kunieleza maana ya ndoto ile. “kuhusu kuwa safarini wewe na bint mfalme ni ishara ya kushirikiana. Na kuhusu kupata ajali inamaanisha kuwa katika kushirikiana kwenu mtapatwa na matatizo lakini yeye ndiye atakayekuokoa.Na kwakuwa kwenye ndoto ni wewe ndiye uliyeokolewa inamaana wewe katika matatizo yako utapata njia kupitia kushirikiana nae. Na kuhusu yeye kushindwa kuokolewa na wewe na hatimaye akaishia majini inaonesha atapatwa na matatizo na atafariki bila ya wewe kufanikiwa kumuokoa. Ama jino linamaanisha kituchako cha karibi kama mke na ndugu. Hivyo jino lako lile linaonesha ni bint mfale atakuwa mkeo na kung’oka kwa jino ni ishara ya kufariki kwa mkeo. Hii ndiyo tafariri ya ndoto yako”Baada ya hpo yule mtu akatoweka, nilipokuja kupaa fahamu kutoka kwenye mawazo yale sikumuona yeyote. Nikutaka kutafuta zaidi nikaweka imani kuwa huenda ni malaika ametumwa kunisaidia kufasiri ndoto yangu. Basi nikaamuwa kumuoa bint mfalme kutokana na ndoto ile inaonesha yeye ataanza kufa na mimi nitaokoka. Hivyo nikaamini hii ni mipango ya mungu. Basi baada ya swala nikaende kwa mfalme na kumueleza kuwa nimekubai ombi lake.Nilipokuwa nazungumza na mfalme kumbe yele binti alikuwa akisikiliza mazungumzo yale na aliposikia nimekubali alipata furaha kubwa iliyopelekea akazimia. Tulishangaa kusikia kishindo nyuma ya mlango na kuenda kuangalia alikuwa ni binti mfalme aliyezimia pale chini. Moyowangu uliruka sana nikawa najiuliza ndo qadar zimeanza yaani atakufa kweli hapahapa na kuniacha mimi. Aliitwa muuguzi na kuanza kumpa tiba. Nilirudi nyumbani nikiwa nasikilizia kama atakufa au atapona maana akifa nitazikwa hatakama shererhe ya ndoa haijafanyika.Nikiwa na wasiwasi siku ilofata nilielekea kwa mfalme kwenda kujulia hali ya binti yake. Nilishangaa kuona mfalme akiwa na bashasha punde tu aliponiona “mwanangu, mwenzio amepata fahamu tayari na mama yenu anaandaa maandalizi ili wiki ijayo iwe ni sherehe ya ndoa yenu. Nilifurahi sana kuona kuwa binti yupo hai maana alikuwa amebeba dhamana ya uhai wangu. Nikawa najiambia moyoni kuwa wiki ijayo naingia maisha mapya na nitakuwa mfalme mtarajiwa. Sinbad mimi ndo utakuwa mwisho wa kuiona familia yangu.NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME.
Siku hazikuenda kipolepole hatimaye wiki ikafika na harusi ikafanyika. Sherehe kubwa isiyo na kifani ilifanyika na hata wafalme wa jirani walihudhuria. Niliozeshwa binti yule na kukabidhiwa nyumba ndani ya ikulu. Nilipata kukabidhiwa na mali na mambo mengine kadhaa. Sherehe za kimila pia zikafanyika kwa ajili ya kukabidhiwa cheo cha mfalme ajae yaani baada ya kufa mfalme huyu nitakuwa mfalme mpya. Yote haya yalifanyika japo sikuwa na furaha nayo.Ni miezi miwili sasa imefika na mishaanza kuzoea mazingira ya kulinda muda wote na kuzungukwa na watu. Nilitembelea uwanja wa kujifunzia farasi nikakuta watu wanaendesha farasi bila ya kuweka kiti chha farasi. Basi nikatumia taaluma nilonayo na kuwatengezea viti vya farasi. Jambo hili lilifanya nipendwe sana na watu na mawaziri kwa kuleta kitu kipya zaidi. Mapenzi ya mfalme na mimi yalizidi kuongezeka siku hadi siku. Watu walikuwa wakinikubali sana hasa ninapokuwa nawasimulia hadithi za kuhusu baghadad na safari za majini na mikasa iliyowahi kunikuta.Ni miezi mitano sasa toka kumuoa binti mfalme. Binti mfalme alinipa habari za furaha kuwa ana ujauzito. Nilizipeleka habari zile kwa babamkwe na mama mkwe. Kwa hakika siwezi kusimulia namna ambavyo furahayao ilivyokuwa. Habari ziliwafikia mawaziri na watu wengine. Wote walikuwa wakiniupongeza. Binti mfalme alizidi kuniona mimi ni mtu muhimu sana kwenye maisha yake kwa kumfanya awe mama mtarajiwa wa familia ya mifalme.Hatimaye miezi ya kujifunguwa ya binti mfalme imefikia na sasa amepelekwa kwa wakunga. Nikiwa nipo mlangoni kusubiria habari za furaha nilishitushwa na kilio kikubwa sana kilichotoka ndani. “Innaa lillahi wa innaa ilaihi rajiun” niliposikia maneno haya yakisemwa nikajua mtoto wangu amefariki dunia. Nilianza kulia sana, na muda si mrefu mkunga mmoja akatokea nje na kuniambia kuwa binti mfalme amefariki dunia na mtoto wake amepona. Nililia zaidi na kutamani ardhi inifukie.Furaha za kupata mtoto sikuweza kuzipata kamwe nikikumbuka kuwa nakwenda kuzikwa na me wangu. Mila haikuwacha kufuata mkonowake sasa mwili wa marehemu ukawa unaanza kuandaliwa na nikamuona baba mkwe akija kwa unyonge na kunipa maelekezo na kunipatia nguo mpya na kuniambia hizi zitakuwa ndio sanda yako. Sina la kukusaidia lamba nitakuongezea mkate wa nane. Maana huwa aliye hai anapozikwa na mwenza anapewa kichupa cha maji na mkate mikate 7 hivyo nitakupendelea kukupa mikate nane.Maneno haya yaliendelea kuniumiza hasa pale watu walipokuja kunihani na kuniaga kwa mara ya mwisho. Sasa ndipo nikaanza kujuta kukubali kutembea majini safari hii. Nilitamani hata ningekuwa kama wale wenzangu nilowaaza kule wanachinjwa maana taabu nitakayoiona na kuzikwa nikiwa hai ni kubwa. Basi likaandaliwa jeneza moja kubwa sana na mimi na mke wangu tukaingizwa na kubebwa kuelekea mazikoni. Walikwenda kwa muda wa masaa 2 na nusu kisha wakaanza kupandisha juu kwa mwendo wa nusu saa. Nikawasikia wanazungumza kuwa wamefika tayari.NDANI YA PANGO LA MAKABURI
Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile.hatimaye n ikahisi jeneza limefika chini kutokana na kugonga chini. Nikalifungua jeneza lile na kutowa mikate yangu nane na maji yangu. Nikaangalia huku na huku hakuna pa kutokea. Nikaangalia juu ni mbali sana na tundu ni dogo na hata sauti haifiki. Nilizunguka mchana mzima sikupata pa kutokea. Sikuya kwanza, pili, tatu mpaka siku ya nne sikupata pa kutokea. Nilikata tamaa nikajua sasa huu ndio mwisho wa Sinbad.Nikaanza kula mikate yangu kwa kuilinda ili isiishe kwa araka. Sasa imefika siku ya sita nikiwa na mikate miwili mkononi. Ilipofika siku ya saba mida ya mchana nikasikia migongano. Nikasogea karibu kwenye lile tundu loo!! ni jeneza linakuja. Nilikuwa nikihisabu siku kwa kuangalia mwanga kwenye tundu lile dogo la kuingizia majeneza. Jeneza lile lilipofika chini nikaona mwanamke aliye hai amezikwa na mumewe. Mwanamke yule nikamsaidia kutoka pale nikiwa na imani kuwa ana mikate yake saba ambapo huenda akanisaidia pindi ya kwangu ikiisha. Nikamsaidia kutoka pale na kujanae pembeni kabisa ya lile pango ambapo harufu za wafu hazifiki kwa kasi.Siku ile usiku nilipolala ghafla nikasikia sauti ya mnyama anayechimba, nikasogea vizuri ila kwa kuwa ni kiza nisione vyema. Nikamwacha akaenda kule kwenye wafu na kuanza kula mizogo. Aple nilipo nikajisemea kuwa sasa huenda hii ndio nusura. Mnyama yule akala mizoga na muda wake ulipofika akatoka. Mimi nikawa namfatilia kwa nyuma usiku ule, tukapita njia nyembamba sana hatimaye akatokea baharini. Basi nikarudi tena kule pangoni kwenda kumchukuwa yule mwenzangu na kuchukuwa mali ambazo watu wamekuwa wakizikwa nazo kama mikufu ya dhahabu na thamani nyinginezo.Nilibeba mzigo mkubwa sana wa mali za dhahabu na thamani nyingine nzuri. Tukatka mimi na mwenzangu yule na kwa bahati tukakutana na jahazi linaloelekea baghadad. Tulipanda mimi na mwenzangu yule. Tulipofika baghadad niliwahadithia kila kilichotokea na walishangaa sana kuniona nipo hai. Yule mwanamke nilompata kule nilisubiri eda yake ilipoisha kulingana na tamaduni za waislamu nikamwoamimi. Kwa hakika safari hii nimepata faida sana na mafunzo mengi.Sin bad alipomaliza hadithi hii ya safari yake ya nne akamwambia Sinbad mbeba mizigo kuwa awahikesho ajesikia yalompata kwenye safari ya tano. Safari hii ya tano kuna matukio kadhaa yalinikuta hivyo uwahi mapema. Kisha akampatia pesa kwa ajili ya matumizi ya siku ile na ijayo. Watu wote wakatawanyika.SAFARI YA TANO YA SINBAD
Baada ya watu kukusanyika siku ilofata sinbad akaanza kusimulia stori ya safari yake ya tano. Akaanza kusema kuwa “niliamua kutokuenda tena safari yoyote ya majini. Hali ilikuwa hivyo lakini baada ya miezi mingi nikapata wazo la kutengeneza jahazi langu ambalo litakuwa ni madhubutizaidi. Kwa mali nilizo nazo wakati huu nikaanza kuandaa jahazi kubwa na la kisasa lililo madhubuti sana. Muda ulitimia na jahazi kubwa na la kisasa zaidi lilikamilika.Nikaanza kualika wafanyabiashara wakubwawakubwa na walio wazoefu zaidi. Tuliandaa bidhaa zetu na tukamtafuta nahodha aliye mahiri na safari hizi. Maandalizi yalipokamilika tukaanza safari usiku kwa kulingana na uwepo wa upepo. Kwa hakika safari ilikuwa njema, tuliweza kupita kwenye mikondo mikubwa na tukaingia visiwa kadhaa. Kwa hakika nahodha huyu alikuwa ni hodari na ni mzoefu, kwani hatukupita kisiwa ila alikuwa akitueleza habari zake. Hata visiwa visivyoishiwa na watu alikuwa akitueleza habari zake. Tulipita kenye kisiwa cha mawe yanayolia. Tukamueleza nahodha atuambie habari za mawe yale kaanza kutusimulia hadithi hii;HADITHI YAKISIWA CHA MAWE YANAYOLIA.
Nimesimuliwa na manahodha wenzangu ambao walipata habari za kisiwa hiki kupitia mababu wa manahodha wenzao ambao walipata habari hizi kutoka kwa mababu wa zamani. Habari za kisiwa hiki ni kuwa, alikuwepo kwenye kisiwa hiki mfalme aliyekuwa anapendwa sana na watu wake. Alikuwa anaushawishi sana na ni mpenzi wa watu. Mfalme na watu wake walikuwa wakiabudia masanamu na kuyafanya ndio miungu yao mikuu. Bila ya kufahamu kama kuna Mungu muumba ambaye anatambulika kwa majina mengi kama Allah kwa waislamu lakini mfalme huyu aliamini kuwa masanamu yao ndio miungu mikubwa.Hali hii ilikuwa ni kawaida kwa mji huu na wananchi wake. Na Mwenyezi mungu aliwapa kila kitu wanachoihitaji. Ilitokea siku moja akaja mtu mkubwa sana akawa anazungumza habari juu ya Mungu Mmoja aliyeumba kila kitu. Habari hiki ziliwashituwa watu wa mji ule kwa tabia yao ya kuabudia masananmu. Mtu yyle alikaa nchini pale kwa muda wa mwaka mmoja akiwa anatoa habari zile na watu wasi mwamini. Mfalme wa nchi ile alikuwa akikasirishwa sana na uwepo wa mtu yule eneo lile.Baada ya mwaka kuisha watu kadhaa walianza kuelewa kuwa masananmu si miungu kwani yametengenezwa na mawe tu na ni kazi ya wafinyanzi. Fikra hizi zilipoanza kuelezwa na wananchi mfalme aliamrisha watu wote wanaomuamini mtu yule wakamatwe. Na mambo yakawa hivyo na walikamatwa watu wote waliomuamini maneno yake mtu yule. Walianza kuadhibiwa na kuuliwa ila yule aliyekubali kuabudu masanamu yao alikuwa akiachiwa. Basi waliuliwa wote hata yule mtu akauliwa pia.Baada ya kufanyika yalofanyika kwa muda wa siku tatu nchi ile ilikuwa na amani. Kuanzia siku ya nne amani ilitoweka kwani moshi mkali sana ulikuja na ukaanza kukausha watu wote na kugeuka mawe. Mashi ule ukauazunguka mawe yale, na kwa kuwa mawe yale ni watu wakawa wanalia kwa moshi ule na kuomba msamaha kwa Allah. Machozi yao ndo yanaendelea hadi leo kama mnavyoona mawe haya yanavyolia. Basi hii ndio hadithi ya mawe haya.
Safari yetu iliendelea tukafanya biashara maeneo kadhaa. Tukiwa njiani maji yalituishia hivyo tukamwambia nahodha atupeleke kwenye kisiwa chochote jirani na tulipo ilo tulapate maji ya kunywa. Nahodha alifanya hivyo na akatupekeka kwenye kisiwa flani ambacho hakikuwa kikishi watu ala alitutahadharisha kuwa eneo lile linaishi wanyama wakari hivyo tufanye tufanyayo na tuwahi kutoka. Basi tukaanza kuchota maji na tulipomaliza wenzangu wakaanza kuzunguka kwenye kisiwa kile waone kama kuna chochote wanaweza kukichukiwa wakauze mbele ya safari.Walizunguka na baada ya muda wakaona kuna kitu kama jiwe kubwa sana jeupe. Wakalisogelea wakidhani inaweza kuwa madini. Walipofika karibu niligunduwa kuwa lile ni yai la ndege mkubwa sana anayeitwa rock. Kwani nilishakumbana na hali kama hii huko nyuma. Basi nikawaambia wenzangu yai hili ni la rock hivyo tuondokeni kwa haraka hapa akitukuta tutauliwa wote. Wenzangu walinibishia na wakalipasua, na kulikaanga wakaanza kulila hata kulibakisha kidogo. Mara tukaona kufuli kikubwa kinakuja nahodha akatuambia tuwahi kuondoka.Kwa umahiri alio nao nahodha aliweza kuweka jahazi sawa na kuanza kuondoka wale ndege walikuwa ni wawili na walipogunduwa kuwa yai lao limeliwa walipiga kelele sana na wakaondoka. Kwa muda hatukuweza kuwaona kabisa tukadhani kuwa tuposalama. Baada ya muda kidogo tukaona kundi kubwa la ndege aina ile linakuja na kila mmoja akiwa amebeba jiwe tayari kutupiga. Na mawe walobeba yalikuwa ni makubwa sana kiasi kwamba kama wawili yanapiga jahazi hakuna atakayepona.Basi ndege wale wakaanza kutupa mawe yale na kwa bahati mbaya jiwe moa likapiga jahazi letu kwa mbele. Kwa umadhubuti wa jahazi lile liliweza kupasuka na kufanya maji yaingie. Jahazi likaanza kuenda hovyo na kukagonga mwamba na kupasuka kabisa. Mimi niliponea kupata ubao nikaukamata kikwelikweli na nikaenda nao hadi ufukweni. Niifika eneo lenye ufukwe mzuri uliopandwa bostani nzuri na ya kivutia. Bila ya kujali ni ya nani nilianza kula matundwa kwa njaa nilonayo. Niliposhiba nikaingia ndani ya bostani ili niweze kuomba msamaha kwa madunda nilokula.Niulimkuta mwenyewe na akaniambai ili anisamehe ni lazima nifanye kazi ya kumuuzia matinda yake sokono kwa muda wa mwezi mzima. Kwa kuwa mimmi ni mfanya biashara sikuona jambo lile ni adhabu. Nilimuuzia matunda yake na alishangaa kuona kuwa kila siku faida ilikuwa ikiongezeka maradufu. Alinipenda sana mzee yule na akaniamini zaidi. Alinifanya kama mtoto wake. Kwa biashara ile na mimi nilipata mtaji na kuanza bishara ndogo ndogo na hatimaye nikapata mtaji wa kuweza kuanza biasha ra za kusafiri. Lengo langulilikuwa ni kurudi kwetu Baghadad.Ilitokea sikumoja nikapata habari kuwa kuna jahazi la wafanyabiashara kutoka Baghadad limekuja na linatarajia kurudi baghadad baada ya wiki moja. Nilimuomba ruhusa yule mzee nieze kurudi nyumbani na alikubali kwa unyongesana. Siku moja akaniita usiku na kuniambia kuwa alinithamini kama mtoto wake na kwa kuwa yeye hana mtoto hata mmoja alitowa hazina ya mali zake ikiwemo madini ya dhahabu, almasi na thamaqni nyinginezo na pesa nyingi sana. Akanikabidhi na aliniambia kuwa anatarajia kuuza shamba lake lile ali arudi nami Baghadadi nilimkubalia na alifanya hivyo.Baada ya maandaizi yalipokamilika tulianza safari ya kurudi na tulifika Baghadadi kwa salama na amani. na hii ndio stori yangu ya safari yangu ya nne. Baada ya kuzungumza haya Sinbad akampatia Sibdad wa nzhikavu pesa kadhaa kwa ajili ya kufidia muda wake wa kukaa naye. Pa akamwahidi kesho aje tena kusikiliza yalomkuta kwenye safari yake ya sita.SAFARI YA SITA YA SINBAD.
Walipokusanyika watu wote akaanza kusimulia kuhusu safari yake ya sita. Nilipookoka na safari ya tano sikutamani tena kusafiri kwa njia ile. Hali hii haikudumu kwa muda mpaka nilipoamua kufanya safari ya mwisho kwani nilikuwa uymri umeshakwenda sana. Nikaamini kuwa faida nitakayoipata safari hii sitafanya safari nyingine yeyote ya majini. Basi nilianza kujiandaa kwa ajili ya safari hii. Hata hivyo maandalizi yalichukuwa muda kwani umri ulikuwa umeshakuwa mkubwa. Baada ya maandalizi safari ikaanza.Safari hii ilikuwa mbaya sana, maana hata hatukuweza kupata siku mzima iliyo salama. Mara tuu baada ya kuanza safari kwa muda wa masaa kama nane kwa makadirio upepo uliharibika na kuwa mkali sana. Jahazi lilikuwa likipelekwa tusukokujuwa kwa muda wa siku tano. Siku ya sita upepo ulitulia katika sehemu ambayo hata hatuijui kabisa. Nahodha baada ya kuangalia zaidi eneo hili alilitukusanya karibu na akatuambia kuwa hapa tulipo tupo katika mkondo hatari sana baharini na hakuna jahazi lililokuja mkondo huu na kupona.
Ghafla maji yaendayo kwa kasi yakatuchukuwa na kutupeleka kwenye ufukwe wa kisiwa tusichokijua. Tulipofika pale nahodha akatuambia tuchuke sisi na mizigo yetu kisha akagawa chakula tulicho nacho sawa kwa sawa kwa kila mtu. Kisha akatuambia kuwa hapa tulipo hakuna upepo unaotoka kuelekea kokote. Maji yote yanavutwa kuelekea hapa. Na eneo hili kama mnavyoona lina mlima huu ambapo hata ukipanda sauti haitafika popote wala kusikiwa na mtu.Kisha akatuambia kuwa hakuna yeyote atakuja kutuakoaa hapa hivyo maisha ya mtu kuishi yatategemea kuisha kwa chakula chake. Wakati anazungumza maneno yale mimi nilikuwa nawaza yalonikuta kule kwenye mapango. Basi hali ikawa hivyo kwa hakika hakuna pa kutokea. Nilizunguka kuangalia eneo li;le nikagunguwa kuwa kuna mto ambao umetokea mlimani kisha ukakunja bila ya kuingua baharini ukarudi upande wa bondeni kudogo pembeni mwa ufukwe na ukapotelea kwenye pango ililo jembaba.KWISHA KWA CHAKULA
Watu waliaanza kumaliza vyakula vyao na wakaanza kufa baada ya siku kadhaa. Tulianza kuwazika mpaka wenzangu wote wakaisha hata nikamzika mwenzeu wa mwisho pekeangu na kubakia mimi tu. Nikiwa na mkate mmoja tu wa ngano ulobakia nikaaza kulia na kijuta kuwa bora nisingesafiri. Nilikata tamaa na nguvu ziliniishia nikajua sasa ndo nakufa mimi. Wakati nilipokuwa nimekaa pale niliona ndege akinywa maji ya kale kajimto. Nilitamani nimuuwe ndege yule nipate chakula.Nilianza kumvizia ndege yule na hata nikamrushia jiwe, na kwa kiwewe ndege yule akaingia kwenye lile pango ambalo kale kajimto kamepotelea. Nilimsubiri nje ya pango ili atoke lakini hakuweza kutoka hata ikafika jioni. Nikala kipande cha mkate na kubakiwa na kipande kimoja. Ilipofika asubuhi nikapata akili luwa kama yule ndege hakuweza kutoka kwenye [pango lile kutakuwa na mabo makuu mawili yanaweza kutokea, moja huenda ameliwa au ametokea nje ya pango sehemu nyingine. Hapo nikajipa matumaini kuwa mto huu utakuwa umetokea eneo jingine.Basi nikaanza kuunganisha mabao kisha nikajilaza kifudifudi na kukusanya mali za dhahabu, almasi na mali nyinginezo za madini katika eneo lile na kulweka mabao yangu kwenye mto ule ambao ulinichukuwa na kupotea nami kwneye pango. Niliweza kupitishwa sehemu nyembembe sana ambapo niliumia sana. Nilimaliza kipande cha mkate wangu hata nikawa sina chochote. Nikawa nawaz anaweza kufa humu kabla hata sijaliona jua. Kwa njaa na mawazo na maumivu ya kugongwa nilipoteza fahamu na nisijue kinachoendelea kwenye mto ule.Nilipokija kuzinduka nikakuta nimezungukwa na watu wengi sana na ni wakubwa zaidi. Wakawa wananiuliza mimi ni nani na nimefika vipi pale kwenye eneo lile. Kabla sijaeleza chochote kwani sikuwa na uwezo wa kusema hivyo nikaomba wanipatie chakula na maji. Nikapewa na kuanza kuridhisha tumbo langu hata nikashiba na kumshukuru Mwenyezi Mungu. Nikawaeleza habari yangu na walishangaa sana. Wakaamuwa kunipeleka kwa mfalme wao ili apate kujuwa yalonikuta.Walinichukuwa mimi na mabao yangu yale na mali zangu na ku nipeleka kwa mfalme wao wa kisiwa hiki kiitwache Serendib. Kwa heshima na taadhima nikamsalimia mfalme na kumueleza kila kilchotokea bila hata ya kuficha. Mfalme alishangaa sana na kuniona nimezaliwa na nyota ya ajali inayoambatana na uokovu. Mfalme akamumu habari yangu iandikwe kwa maandishi ya dhahabu na iwekwe kwenye hifadhi ya kifalme kwa vizazi vijavyo.Nilikaa pale Serendib kwa muda wa mwezi mmoja na nikamuomba ruhusa mfalme niweze kurudi nyumbani. Alikubali na kunipatia malinyingi kisha akanipatia barua ili nikampe Sultan Harun Rashid wa Baghadad. Barua ilikuwa imeeandikwa kwenye karatasi cha bluu zilizotengenezwa na ngozi ya nyok. Maadhishi yalikuwa ni ya dhahabu yaliyochovywa na mafuta ya misk. Mfalme pia alinipatia zawadi nyingi sana kwa ajili ya familia yangu na kwa ajili ya Sultani Harun Rashi. Barua ilikuwa na lengo la kuomba urafiki kati ya vuiongozi wawili hawa.Nilisafiri kwa amani hata nikafika kwenye bandari ya Balsora na kufika nyumbani na mali mengi sana. Niliwaeleza ndugu zangu yalonikuta na safari hii nikaadidi kuwa sasa sitosafiri tena kibiashara. Siku ilofuata nikaongozana na familia yangu na kuelekea kwa Sultan kwenda mpatia barua yake. Sultani alifurahi sana na alipenda zawadi alopewa. [ia aliniuliza habari nyingi kuhusu mfalme wa Balsora na kumridhisha maswali yake. Nikaondoka na kurudi kwangu. Baada ya hapa nikaanza kutengeneza maisha yangu na sikutaka tena kusafiri majini.Baada ya kumaliza kusimulia hadithi hii ya safari hyake ya sita Sinbad alimpatia Sinbad wa nchikavu pesa kiasi kadhaa kama fidia ya kupoteza muda wake na kumsikiliza. Watu wakatawanyika pale na akamuahidi Sinbada awahi kesho ili asikilize kilichotokea kwenye safari yake yta saba na kwa nini alivunja ahadi yake mara hii.SAFARI YA SABA YA SINBAD
Walipokusanyika siku ilofata Sinbad akawaambia kuwa kilichofanya nikavunja ahadi yangu ya kutosafiri tena ni kauli ya Sultani Nilipopunzika kwa muda wa miezi miwili nilipata habari kuwa Sultani ananiita. Nilipokwenda alinieleza kuwa anataka nipeleke barua yake kwa mfalme wa Serendib ya kumjibu kuwa ameridhika na urafiki. Nikamueleza kuwa nimeweka ahadi ya kutousafiri tena kutokana na yalonikuta. Sultani alisisitiza sana mimikwenda na akaniambia kuwa mimi ndie mtu nafaa zaidi kwani mfalme wa Serendib ananijua.Basi nilikubaliana na amri ya Sultani na ikaandaliwa safari ya kifalme na jahazi lililo madhubuti zaidi na la kisasa liliandaliwa na Sultani mwenyewe. Baada ya maandalizi kukamilika mali nyingi kama zawadi ziliandaliwa kwa ajili ya mfalme. Safari ilianza salama na tuliwasili Serendib kwa amani muda wa jioni. Mfalme wa Serendib alinipokea mwenyewe na kunikumbatia na kunivika joho lenye ukosi ulochovywa kwenye dhahabu nyekundu.Mfalme alilidhika na zawadi zile na alifurahi sana kwa kuniona. Mfalme alifurahi zaidi kuona barua ile imejibiwa kama atakavyo. Mafalme wa Serendib akaniozesha mtoto wake kama takrima ya udugu wetu. Ndoa ilifanyika salama na baada ya kukaa pale kwa muda wa mwezi mmoja nilipewa ruhusa ya kuondoka mimi na mkewangu na zawadi nyingi kwa ajili yangu na kwa ajili ya Sultani wa Baghadad.Mfalme mwenyewe aliandaa jahazi na kulimadhiubutisha na safari iliandaliwa kifalme kwani ndani mlikuwa na mkwe na mtoto wa mfalme. Tuliwasili Baghadadi baada ya mwe ndo wa siku kumi na tano. Na Sultani alitupokea kwa heshima zote na kukutana na binti wa Mfalme wa Serendib. Sultani alitufanyia sherehekubwa kama ile ilofanyika wakati wa harusi kule Sererndib. Kwa hakika ilikuwa ni furaha kubwa zaidi. Na huu ndio mwisho wa safari zangu saba za majini.Mpaka sasa nina wake watatu mmoja nilishamuoa nilipokuwa kijana na mwingine ni yule nilookoka nae kwenye makaburi na wa tati ni huyu. Na nimebahatika kuoa mabinti wawili wa wafalme. Kisha Sinbad akawaomba wakezake wote waje ili Sinbad wa nchikavu awaone, kisha akamkutaninisha na yule mzee wa bostani alokuja nae Sinbad. Kisha Sinbad wa baharini akamuuliza Sinbad wa nchikavu “je! Unafikiri sistahiki kupata maisha haya kwa sasa?, je! Kuna yeyote unayemfahamu amepata taabu kama mimi?” majibu ya maswali haya alibakia nayo Sinbad moyoni kwa mshangao.Baada ya pale Sinbad wa majini akamwambia Sinbad mbeba mizigo kuwa sasa tumeshakkuwa marafiki. Kwa siku saba hizi umekuwa kama ni ndugu yangu sasa. Naomba uje na familia yako tukae hapa kama ndugu. Sindab mbeba mizigo akakubaliana na ombi lile na waliishi na Sinbad kwa muda mrefu sana. Waliishi kama kaka na ndogoake. Hata alipofariki Ndugu wa Sinbad wakamchagua kijana Sinbad mbeba mizigo awe ndiye msimamizi mkuu wa mali za mzee Sinbad. Kwa hakika maisha yao yalikuwa mazuri sana na mahusiano yao na ya Sultani wa Baghadad na mfalme wa Serendib hayakukoma.Mpaka kufikia hapa Schehrazade akamaliza hadithi hii ya Sinbad, na tayari miezi mingi ilishapita bila ya kuuliwa na Sultani Shahariyar. Baada ya hapa Sultani Shahariyar akauliza “hatujajua kilichomkuta mtoto wa Sinbad aliyemzaa kutoka kwa ‘Aisha mtoto wa mfalme” Dinarzade akamwambia “ni hadithi ya kusisimua sana” na kama utaniongeza muda zaidi wa kuishi nitakusimulia hadithi nzuri zaidi ya yalomkuta mtoto wa Sinbad.
NA HUU NDIO MWISHO WA HADITHI ZA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA. KUPATA MUENDELEZO WA HADITHI DOWNLOAD APP YETU YA ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI.KUPATA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NAMI KWA
EMAIL: rajabumahe@gmail.com
PHONE:+255712939055
YOOTUBE:www.youtube.com/c/Rajabu Athuman.

KITABU CHA PILI
HADITHI ZA ALIF LELA U LELA
UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA.Katika nchi za China, Hindi, Uarabuni na Uajemi alikuwepo mfalme aliyefahamika na kuheshimika sana kwa uhodari wake na utawala wake mzuru. Mfalme huyu alikuwa na watoro wawili ambao ni Shahariyar na Shahzaman. Watoto hawa walikuwa mahodari na walifahamika sana. Alipofariki baba yao mtoto mkubwa alitawala kiti cha baba yake kuanzia makao makuu na mdogo wake akaendelea kutawala maeneo ya Samarqand.Baada ya kutengena kwa muda ndugu wawili hawa walipanga kukutana. Makutano yao yalifanikiwa kupangwa na hatimaye wakakutana. Katika wakati kama huu wa kukutana kwa ndugu wawili hawa kulitokea hali za kusalitiwa na wakezao. Shahariyar alikuwa na mkewake aliyempenda sana na hakuamini kuwa inaweza kutokea siku akasalitiwa na mkewe. Baada ya usaliti huu aliamini kuwa hakuna tena mwanamke mkweli duniani kote. Hivyo akaweka nadhiri ya kuoa mke mpya aliye kigori na kumuuwa kila ifikapo asubuhi.Kiapo hiki cha Sultani huyu kilikuwa kweli na alikuwa akifanya hivyo yaani anaowa jioni na asubuhi anauwa. Hali ilikuwa ngumu kiasi kwamba watu wakawa wanawakimbiza mabinti zao mjini. Sifa zote nzuri za Sultani huyu zikaanza kuwa mbaya kwa kitendo chake cha kuuwa watoto wa kike. Kazi yote ya kutafuta mabinti wa kuolewa na mfalme pamoja na kazi ya kutekeleza ahadi ya mfalme kuwauwa mabinti hawa alipewa mmoja katika mawaziri wa Sultani huyu.Sultani huyu alikuwa na mabinti wawili ambao ni Schehrazade na Dinarzade. Mabinti hawa walikuwa ni wazuri sana na walipendana na hata hivyo walipata upendo mkubwa sana kutoka kwa mbaba yao. Schehrazade ambaye ndiye mkubwa alikuwa ni mrembo zaidi na alikuwa na taaluma mbalimbali na alikuwa na elimu za mambo mengi hata ya kisayanzi na masimulizi ya fasihi. Watu wa nchi hii waliamini kuwa uzuri alonao Schehrazade anafaa kuilewa na mfalme au mtoto wa mfalne na si mtu mwingine.Sikumoja katika mazungumzo ya kifamilia kati ya waziri na watoto wake Schehrezade alitowa ombi la kushangaza kwa baba yake na kumwambia kuwa anatakakukomesha tabia ya mfalme ya kuuwa mabinti hivyo anataka siku ifiataya aolewe yeye. Waziri alishangaa na kumuonya mwanae lakini hakusikia. Akajaribu kumtisha na akamsimulia hadithi ya mfugaji na mkewe lakini msmamo wake hauku badilika. Basi harusi ikafanyika na Shehrazadw akapanga mpago na Dinarzade juu ya kutaka kukomesha tabia ya Sultani.Usiku nyumbani kwa mfalme Dinarzade alisikika akimuamsha dadayake Schehrazade ambaye anatarajiwa kuuliwa ifikap asubuhi. Dinarzade alimwambia dada yake apigie hadithi nzuri iwe kama ndio mazungumzo ya kuagana. Schehrazade aluimtaka idhini mfalme na kukubaliwa. Akaanza kumsimulia hadithi ya mfanya biashara na jini. Masimulizi ya hadithi hii yalionekana kumvutia na Sultani pia. Schehrazade kwa ufundi wake wa kusimulia hadithi aliikata hadithi hii na kumwambia Sultani akimuongeza siku zaidi ya kuishi ataimaliza.Sultani alimpa siku zaidi Schehrazade ili amalizie hadithi zake. Utamu uliendelea kumpanda Sultani na kila siku hadithi zilikuwa zinaishia patamu. Hivyo Schehrazade akaendelea kupata muda zaidi wa kuishi. Dada huyu alisimulia hadithi ya mvuvi na jini, hadithi ya chongo watatu na mabinti wa baghadad na nyinginezo hata akafikia kwenye hadithi ya Sinbad. Dada huyu alipomaliza hadithi hii akabakiwa na kuelezea yalotokea kwa mtoto wa Sinbad.Basi siku ilofata baada ya kuisha kwa hadithi ya Sinbad Scheherazade akaanza kusimulia kilichotokea kwa mtoto wa Sinbad alozaliwa na bint ‘Aisha mtoto wa mfalme. Scheherazade akamueleza kuwa atahaya ya msimulia hadithi nzuri zaidi ya ile a mtoto wa Sinbad. Hapo Sulltani akamwambia asimulie hiyo hadithi nzuri zaidi ya mtoto wa Sinbad. Hapo Scheherazade akaanza kusimulia hadithi ifuatayo.
KIFO CHA MTOA BURUDANI WA SUKLTAN.
Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani. Kijana huyu alizoeleka sana na mfalme kiasi kwamba mfalme hakuwea kumkosa hata kwa siku moja. Siku moja kijana huyu akiwa kwenye dimbwi kubwa la mawazo alitembea maeneo kadhaa katika mji huu na akakutana na Mshona nguo. Alikaa sana kwenye eneo hili nje ya ofisi ya mshona nguo.Muda wa kufunga ofisi ulipofika mshonanguo alimchukuwa kijana huyu na kwenda naye nyumbani kwa lengo la kufurahi nae na kula chakula. Alipofika nyumbani mkewake alimpokea kwa ukarimu kijana huya. Na kwa ufundi na uwezo wa kutoa burudani alio nao kijana huyu aliweza kuchangamsha nyumba hii. Mke wa mshonaji alianza kuandaa chakula kizuri sana na nyama ya samaki. Aliandaa ndizi na vyakula vizurivizuri kwa ajili ya mgeni wao.Huku burudani zikiendelea mke wa mshonaji aliendelea kupika. Mshonaji alikwenda kuchukuwa vinywaji kadhaa na kuvileta pale nyumbani kwao. Muda wa chakula ulipofika walikusanyika na kuanza kula. Katika kufanya manyonjo na furaha mke wa mshonaji akachukuwa nofu la nyama na kuliiweka kwenye mdomo wa kijana yule na kumwambia meza. Kijana alimeza na kwa bahati mbaya kwenye nofu lile kulikuwa na mwiba mkubwa sana. Mwiba ule ukamkaba kijana yule na kupoteza maifahamu.Mshonaji baada ya kuangalia hali ile akagunduwa kuwa kijana amekufa. Kuona hivyo akaogopa sana maana ataambiwa amemuuwa kijana wa watu. Wakashauriana na mkewake nini wafanye. Baada ya muda wakaamuwa kumchukuwa marehemu waendenae kwa tabibu ili wamuachie msala wote tabibu. Hali ikawa hivyo na wakambeba hadi mlangoni kwa tabibu kisha wakamlaza pale.Waligonga hodi akatoka kijana wakamueleza amuite abibu harakwa kuna mgonjwa ana hali mbaya. Alipoingia ndani yule mtto kwenda muita tabibu mshonaji na mkewe wakakimbia. Tabibu alitoka na kiza cha usiku ule na akamkanyaga huyo aloambiwa mgonjwa. Ikawa tabibu akafikiri yeye ndo alomuuwa mgonjwa. Akanza kushauriana na familia yake wajue namna ya kujinusuru na janga lile. Mke wake akamshauri mumewe kwa kumwambia kuwa wamueke kwenye ukuta wa jirani yao.Jirani yao alikuwa ni muuza nyama hivyo kulikuwa na wezi wanakuja kuiba nyamma pale kwake. Hivyo walifikiria huenda akampiga na kujuwa amemuuwa yeye. Basi wakamfunga kamba karehemu yule na kumpenyeza kwa nje ya nyumba yao kupitia paani. Aliposimama sawa kwenye ukuta wa jirani yao kwa nyuma wakaitowa kamba ile. Ilipofika usiku sana yule muuza nyama alirudi nyumbani na alipoona mtu kasimama kwenye ukuta wake akajuwa ni mwizi amekuja. Hivyo akachukuwa fimbo kubwa na kuanza kumtandika sawasawa. Hatimaye mtu yule alianguka na alipomgusa akahisi ameshakufa.Kwa woga akafikkiria kuwa ameuwa mtu. Akaanza kushauriana na familia yake namna ya kujinusuru na mkasa huu.wakaamuwa wambebe maiti yule kisha wakamsimamishe kwenye moja ya kuta za sokoni, huenda akakumbana na walinzi wakampiga na hapo itakuwa ameuliwa mwizi na esi itaishia hapo. Wakafanya hivyo na baada ya muda mmoja katika walevi akapita eneo lile na alipoona mtu kajibanza akajuwa ni wale watu wanaomnyemelea siku zote na kumuibia pindi akilewa.Mlevi yule alinyata pale karibu na kumpiga chupa ya mgongoni mtu yule. Hatiumaye kwa pigo moja la mlevi mtu yule akaangunga na m;evi kuangalia vile akajuwa kuwa ameuwa. Palepale walinzi walifika na kumkamata mlevi yule kwa kosa la kuuwa mtu. Basi kesi ile ikapelekwa kwa kadhi ili hukumu itolewe, na hukumu ikapita kuwa mlevi ni muuwaji hivyo naye auliwe. Mlevia akapelekwa katika uwanja wa mauaji na kuwekwa tayari kuuliwa.Wakati hukumu inataka kupitishwa ghafla akatokea yule muuza nyama na kusema “ewe ndugu hakimu tafadhali niuwe mimi kwani ndiye nilomuuwa huyo kijana na si huyo mlevi” basi pale pale akaondolewa mlevi na muuza nyama akatiwa kitanzi tayari kwa kuchinjwa. Kabla hajachinjwa akatokea tabitu na kusema yeye ndiye muuwaji hivyo achinjwe yeye. Na alipotaka kuchinjwa tabibu alikuja mshona charahani na kusema yeye ndiye muuwaji halisi na wote hawa hawahusiki. Kitanzi kilipokuwa kwa mshona charahani. Kabla ya kufanya zoezi hakimu akaanza kushauriana na wenzie nini wafanye maana muuwaji halisi hawamjui.NANI MUUWAJI?
Mfalme alipoamka alitaka kumuona kijana wake lakini asimuone. Akauliza habari za kijana yule na akaelezwa kuwa amefariki lakini muuwaji hajulikani, mpaka sasa kuna wauwaji wanne na kila mmoja anadai yeye ndio muuwaji halisi. Mfalme akaamrisha wote waitwe na waje mbele yake na amtafute muuwaji halisi wa kijana wake yeye mwenyewe.Mfalme aliogopa sana asije fanya kosa kama lile alolifanya kwenye kesi ya kifo cha mtoto kwenye ndoo ya maji ambapo mtu asiye na hatia aliuliwa. Walinzi wa mfalme wakamuuliza kwani ni kitu gani kilitokea kuhusu kesi ya mtoto huyu. Akawasimulia kwa ufupi habari hii kuwa alikiwepo mama mmoja aliyekuwa na mtoto anayeanza kusimama dede. Pale ndani palikuwepo na mfanya kazi wao. Mtoto yule alizoeshwa kuogeshwa kwenye ndoo ya maji na mama yake a alikuwa akifurahia sana anapotiwa kwenye ndoo ya maji.Siku moja mama yule alipata safari ya ghafla na kumuacha mtoto wake kwa jirani maana mfanyakazi hakuwepo alikwenda kuchota maji mbali kidogo. Mtoto yule akiwa kwa jirani alitoroka na kyurudi kwao. Na kwa kuwa milango ilikuwa wazi aliingia ndani na kukuta ndoo za maji zipo wazi. Mtoto yule akaingia kwenye ndoo zile na kupitiwa na usingizi. Dada mchota maji alipokuja hakuangalia vizuri kwenye ndoo akajaza maji na kuondoka kwa haraka ili akawahi foleni ya maji.Mtoto mule kwenye ndoo alipiga kelele na kayanywa maji zaidi na hatimaye akapoteza maisha. Akaja dada wa kazi na kujaza ndoo ile kisha akaifung bila ya kuangalia nddani. Akazipandanisha ndoo kama tatu. Mama aliporudi alimtafuta mtoto kwa jirani bila ya mafanikio. Juhudi za kumtafuta ziliendelea ndani ya siku tatu bila hata kufanikiwa. Majirani wakamuonea huruma mwenzao na wakaamua kumpikia apate kula, wengine wakaanza kufua nguo zake na kudeki nyumba maana ndani ya siku tatu hakukuwa kukipikwa wala kufagiliwa wala kudekiwa.Maji yalipobakia ndoo moja wakamkuta mtoto amshakufa kwenye maji. Mama yule kwa hasira alimpeleka mfanyakazi wa hakimu na hatimaye mfanyakazi akauliwa kwa kosa la kumuuwa mtoto kwenye maji na kumficha na ndoo. Kumbe mfanya kazi hana hatia maana ni mama aliyemzoesha mwanae kuingia kwenye ndoo na nikosa la jirani kutomuangalia vizuri mtoto. Kosa la mfanyakazi kuweka maji bila ya uangalifu. Hivyo nahofia kesi hii isijekuwa na mfanano na hii. Basi kwa haraka akaagiza waletwe wat wote wanaohusika mbele yake.Watu wote wakapelekwa kwa mfalme pamoja na maiti wao. Falme akaanza kuuliza mmoja mmoja ataje amemuuwa vipi. Hapo mlevi akasema namna ambavyo tukio limetokea, kisha muuza nyama akaeleza tukio lilivyotokea kwa upande wake kisha tabibu kisha mshona nguo. Baada ya kiusikia maelezo ya kushangaza mfalme akaamuru habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na iwekwe kwenye kumbukumbu za kifalme. Kisaha mfalme akauliza je kuna mwenye hadithi inayoshangaza zaidi ya hii ya kijana wangu huyu? Hapo mlevi akasema yeye ana hadithi ya kushangaza zaidi ya hii. Na akaanza kusimulia kama ifuatavyo;-ENDELEA KITABU CHA PILI