Twahara na umuhimu wake katika uislamu


image



Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria. Pia utajifunza umuhimu wake

TWAHARA NA UMUHIMU WAKE

 

Maana Ya Twahara Katika Lugha Ya Kawaida:

 

Ni usafi na kuondosha uchafu au takataka za kihisia (kugusika) kama najsi ya mkojo au kinginecho, na za kidhahania kama kasoro (mapungufu) na maasi.

 

Kutwaharisha ni kusafisha, nako ni kupaweka mahala maalumu katika hali ya usafi. [Al-Libaab Sharhul Kitaab (1/10) na Ad-Durru Al-Mukhtaar (1/79)].

 

Ama kisharia (kitaaluma):

 

Ni kuondosha kinachozuia kuswali kama hadathi au najsi kwa kutumia maji (au kinginecho), au kuondosha hukmu yake kwa mchanga. [Al-Mughniy cha Ibn Qudaamah (1/12)].

 

 

Hukmu ya twahara:

 

Kutwaharisha najsi na kuiondosha ni jambo la wajibu ikiwa mtu atakumbuka na ataweza. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Anasema:

((وَثِيَابَكَ فَطَهِّر))

((Na nguo zako zitwaharishe)) [Al-Muddath-thir (74:4)]

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala):

((أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ))

((Ya kwamba itakaseni Nyumba Yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu na wanaojitenga humo kwa ‘ibaadah, na wanaoinama na kusujudu)). [Al Baqarah (2:125)]

 

Ama kujitwaharisha na hadathi, hilo ni lazima ili ruhusa ya kuswali ipatikane kwa neno lake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

(( لَا تُقْبَلُ صَلَاةُ بغير طهور))

 

((Swalaah haikubaliwi bila ya wudhuu). [Swahiyh Muslim 224]

 

 

Umuhimu Wake:

 

 

1- Twahara ni sharti ya kusihi kwa sala ya mja. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((لَا تُقْبَلُ صَلَاةُ مَنْ أَحْدَثَ حَتَّى يَتَوَضَّأَ ))

((Haikubaliwi Swalaah ya mtu mwenye hadathi mpaka atawadhe)). [Imepasishwa na Al Bukhaariy (135), Muslim (225].

 

Kuswali na twahara ni kumtukuza Allaah. Na hadathi na janaba – ingawa si najsi zenye kuonekana – lakini hata hivyo ni najsi za kidhahania zenye kukifanya kilichoingiwa navyo kuonekana kichafu. Hivyo basi, kuwepo kwake huteteresha utukuzo kwa Allaah, na huenda kinyume na msingi wa usafi.

 

 

2- Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Amewasifu wenye kujitwaharisha. Anasema:

 

((إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ))

((Hakika Allaah Anawapenda wenye kutubia mara kwa mara na Anawapenda wenye kujitwaharisha)). [Al Baqarah 2:222]

 

Akawasifu watu wa Masjid Qubaa kwa Neno Lake:

 

((فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُواْ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ))

((Ndani yake kuna watu wanaopenda kujitwaharisha, na Allaah Anawapenda wenye kujitwaharisha)). [At Tawbah 9:108]

 

 

3- Kutojali au kutotilia maanani kujitakasa na najsi, ni moja kati ya sababu za kuadhibiwa watu makaburini. Imepokelewa na Ibn 'Abbaas akisema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita kwenye makaburi mawili akasema:

 

(( إِنَّهُمَا لَيُعَذَّبَانِ وَمَا يُعَذَّبَانِ فِي كَبِيرٍ، أَمَّا هذا فَكَانَ لَا يَسْتَنزه مِنْ بَوْلِهِ، ))

((Kwa hakika wawili (hawa) wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. (la kuwashinda kutekeleza au kujiepusha nalo). Ama huyu, alikuwa hajitakasi na mkojo wake)). [Abu Daawuud (20), An Nasaaiy (31-69), na Ibn Maajah (347) kwa Sanad Swahiyh].

 



Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-09-11

ZOEZI

Jaza maswali yote ama baadhi kisha bofya kitufe za kutuma majibu hapo chini.



1 : Ni kitugani utatumia kujitwaharisha kama huna maji? ____





2 : Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) Amewasifu wenye ___________





3 : Najisi za kidhahania ni zipi?_________





4 : Kutokujisitiri na kujiepusha na najisi kunaweza sababisha kupata adhabu __________





5 : watu wa Masjid Qubaa walisifiwa kwa sababu ipi ? ________





6 : _________ Ni kuondosha kinachozuia kuswali kama hadathi au najsi





7 : Moja kati ya zifuatazo ni najisi za dhahania ______





8 : Najisi za kihisia ni zile ambazo _________





9 : Neno la kiswahili lenye maana ya twahara ni ________





10 : Twahara ni sharti la ibada gani? ________







RELATED POSTS

picture

JE MANII NI TWAHARA AU NAJISI?

Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis
picture

MAMBO YANAYOWEZA KUTOA UDHU WAKO

Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu.
picture

JINSI YA KUTAWADHA KAMA AALIVYOTAWADHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume
picture

JINSI YA KUTWAHARISHA AINA MBALIMBALI ZA NAJISI

Kila najisi ina namna yake ya kutwaharisha, hata hivyo namna hizo hufanana. Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutwaharisha najisi mbalimbali.
picture

MAMBO YALIYO HARAMU KWA MWENYE HEDHI NA NIFASI

Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi
picture

FADHILA ZA UDHU YAANI FAIDA ZA UDHU

Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu
picture

AINA ZA NAJISI NA TWAHARA KATIKA UISLAMU

Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu
picture

ZIJUWE NGUZO TANO ZA UISLAMU NA MAANA ZAKE KATIKA SHERIA YA UISLAMU

Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.