Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu.
Udhu unaweza kuharibika kwa sababu ya Moja kati ya mambo yafuatayo:-
KUSINZIA HAKUHARIBU UDHU
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضى الله عنه قَالَ: {كَانَ أَصْحَابُ رَسُولِ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى عَهْدِهِ يَنْتَظِرُونَ اَلْعِشَاءَ حَتَّى تَخْفِقَ رُؤُوسُهُمْ، ثُمَّ يُصَلُّونَ وَلَا يَتَوَضَّئُونَ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ
وَأَصْلُهُ فِي مُسْلِمٍ
Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), katika zama zake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) walikuwa wakingojea Swalaah ya ‘Ishaa hadi wanainamisha chini vichwa vyao (kwa kusinzia), kisha wanaswali bila kutawadha upya[3].” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ad-Daaruqutwniy]
DAMU YA UGONJWA INAHARIBU UDHU
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {جَاءَتْ فَاطِمَةُ بِنْتُ أَبِي حُبَيْشٍ إِلَى اَلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! إِنِّي اِمْرَأَةٌ أُسْتَحَاضُ فَلَا أَطْهُرُ، أَفَأَدَعُ اَلصَّلَاةَ؟ قَالَ: "لَا. إِنَّمَا ذَلِكَ عِرْقٌ، وَلَيْسَ بِحَيْضٍ، فَإِذَا أَقْبَلَتْ حَيْضَتُكِ فَدَعِي اَلصَّلَاةَ، وَإِذَا أَدْبَرَتْ فَاغْسِلِي عَنْكِ اَلدَّمَ، ثُمَّ صَلِّي} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِلْبُخَارِيِّ: {ثُمَّ تَوَضَّئِي لِكُلِّ صَلَاةٍ}
وَأَشَارَ مُسْلِمٌ إِلَى أَنَّهُ حَذَفَهَا عَمْدًا
Kutokwa kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: Faatwimah bint Abiy Hubaysh alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Mimi ni mwanamke nakuwa na istihaadhwah (damu[5] ya haikatiki hata baada ya muda wa hedhi kumalizika) hivyo huwa sitohariki, je, niache kuswali?” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Hapana kwani huo ni mshipa wa damu, wala si hedhi, hivyo, ukiingia katika hedhi, sitisha kuswali, na hedhi ikiisha, osha damu huko iliko, kisha uswali.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Al-Bukhaariy ameongezea: “Kisha tawadha kwa kila Swalaah[6].”
MADHII YANAHARIBU UDHU
وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رضى الله عنه قَالَ: {كُنْتُ رَجُلاً مَذَّاءً، فَأَمَرْتُ اَلْمِقْدَادَ بْنَ اَلْأَسْوَدِ أَنْ يَسْأَلَ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَسَأَلَهُ فَقَالَ: "فِيهِ اَلْوُضُوءُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
Kutoka kwa ‘Aliy bin Abuu Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilikuwa mtu wa kutokwa na madhiy (majimaji yatokayo katika dhakari), nikamuamrisha Miqdaad bin Al-Aswad[8] amuulize Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), akamuuliza.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Anapaswa atawadhe.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
[Na tamshi hili ni la Al-Bukhaariy]
KUJAMBA KUNAONDOA UDHU
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِذَا وَجَدَ أَحَدُكُمْ فِي بَطْنِهِ شَيْئًا، فَأَشْكَلَ عَلَيْهِ: أَخَرَجَ مِنْهُ شَيْءٌ، أَمْ لَا؟ فَلَا يَخْرُجَنَّ مِنْ اَلْمَسْجِدِ حَتَّى يَسْمَعَ صَوْتًا، أَوْ يَجِدَ رِيحًا} أَخْرَجَهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mmoja wenu akipata kinachomtia shaka katika tumbo lake kuwa anatokwa kitu au la, basi asitoke Msikitini hadi amesikia sauti yake au ahisi harufu[10] yake.” [Imetolewa na Muslim]
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-09-03
Jaza maswali yote ama baadhi kisha bofya kitufe za kutuma majibu hapo chini.