Khalid Ibn al walid katika vita vya Muta


imageYiomyokea khalid Ibn al walid katika vita vya Muta

Khalid Ibn al walid kwa mara ya kwanza akiwa Muislamu alishiriki vita vya Muuta. Hivi ni vita vilivyopiganwa kati ya waislamu na watu wa Peshia wakichanganyika na Sasanid mwaka 629 mwezi wa 9 katika kijiji kilichoitwa Mu'ta

 

 

 

Sababu ya vita vya muuta ni kulipiza kisasi cha muislamu aliyeuliwa wakati akitekeleza majukumu aliyopewa na Mtume Muhammad. Mtume Muhammad (s.a.w) alimtuma Al-Harith bin Umair Al-Azdi (R.A.) kwenda Basra kupeleka barua ya kuwalingania katika dini ya Uislamu. Lakini akiwa njiani alikamatwa na Shurahbil bin Amrul-Ghassani ambaye ni gavana wa Balqa. Katika wakati huo kumuuwa mjumbe ni katika makosa makubwa na ni sawa na kutangaza vita.

 

 

 

Jeshi la waislamu lilikuwa na askari 3000 huku jeshi la makafiriblikawa na idadi kubwa sana ya askari. Baadhi ya wanahistoria wa kiislamu wametaja kuwa makafiri walikuwa na jeshibkatibya askati 100000 hadi 200000. Hata hivyo wanahistiria wa leo wanataja kuwa wanajeshi wa kikristo walikuwa 10000 ama chini ya hapo. 

 

 

 

Makamanda wa kikosi cha waislamu walikuwa ni Zayd ibn Haritha, Ja'far ibn Abi Talib, na Abd Allah ibn Rawahah na wote walikufa vitani. Makamanda hawq walichaguliwa na Mtume mwenyewe. Pia aliwapangilia kwa myiririko kuwa atanza Zayd akifa atachukuwa uongozi Ja'far na akifa atachukuwa Ibn Rawah. 

 

 

 

Makamanda walipigana kiume hadi wote wakauwawa kwa mpangilio huo huo. Baada ya kuuliwa makamanda wote jeshi la waislamu lilipata mtafaruku na hapo Thabit ibn Aqram akachukuwq bendera kuwa kama kiongozi. 

 

 

 

Baada ya hapo akampatia uongizi khalid Ibn al walid. Sasa Khalid kwa mara ya kwanza anapewa kazi ya kuongoza jeshi la waislamu. Baada ya kuoigana kiume khalid akagunduwa kuwa waislamu wamezidiwa na hivyo watafute njia ya murudi nyumbani salama. 

 

Khalid alilipanga vyema jeshi lake katika muonekano kuwa wataonekana kama nj wageni. Yaani kumfanya adui ahisi kama jeshi la waislamu limeongezeka. Hivyo akawapanga katika swafu tifauti na walivyokuwa siku chache zilizopita. Mfano waliokuwa wanapigana uoande wa kulia wapelekwe nyuma kushito na wanyuma kushito wapelekwe mbele kulia. 

 

Basi makafiri wqlivyoona vile wakapata mshangao na kuhisi kuwa wenzetu wamepata nguvu mpya. Khalid alipoona makafiri wamepata woga ndipo akaamrisha jeshi lishambukie kwa nguvu zote na japo makafiri wakapata mvurugiko kwenye safu zao na wengi waliuliwa hapo. 

 

Khalid akatumia mvurugiko huo na kuanza kurudi nyuma kidogo kidogo. Huku makafiri wqkiogopa kuwafatilia wakidhani wanaweza kuzungukwa. Hatimaye khalid aliweza kulirudisha jeshi la Waislamu salama. 

 

 

 

Waislamu 12 tu waliweza walikufa mashahidi. Makafiri waliokufa kwenye vita idadi yao haijulikani, ijapokuwa inasemekana ni kubwa sana. Hata hivyo baadhi ya nukuu zinasema idadi yao ni kubwa kuliko idadi ya waliokufa katika waislamu. Wanahistoria wa leo wanakataa kuhusu idadi ya walokufa katiika jeshi la waislamu kuwa ni ndogo ukilinganisha na wingi wa jeshi la adui pamoja na njia iliyotumika kupigana. Hata hivyo bado hakuna ushahidi wa kuthibitisha idadi wanayoikubali.

 

Kwa maelezo zaidi ya vita hivi tafadhali rejea makala yetu ya vita vya Muta

https://www.bongoclass.com/madrasa/historia-ya-vita-vya-mutaImeandikwa na Rajabu Terehe 2023-09-05

ZOEZI

Jaza maswali yote ama baadhi kisha bofya kitufe za kutuma majibu hapo chini.1 : Ni Sahaba gani alikatwa mikono yote? _____

2 : Jeshi la waislamu katika vita vya mu'uta lilikuwa na watu wangapi? ____

3 : Ni sahaba gani aliuliwa na Shurahbil? ____

4 : Vita vya mu'uta ilipiganwa katikab kijiji cha ____

5 : Ni waislamu wangapi walikufa katika vita vya mu'uta? _____

6 : Shurahbil bin Amrul-Ghassani alikuwa ni gavana wa eneo gani ______ ?

7 : Nini hasa ilikuwa ni sababu ya vita vya mu'uta? _____

8 : Ni makafiri wangapi walikufa katika vita vya mu'uta? ____

9 : Ni nani alikabidhiwa uongizi wa jeshi baada ya kufariki kwa Abd Allah ibn Rawahah ____

10 : Vita vya mu'uta vilitokea mwezi gani? _____RELATED POSTS

picture

HISTORIA YA VITA VYA MUTA

hii ni historia ya vita vya Muta. Katika makala hii utajifunza sababu ya vita hivi na yaliyojiri katika uwanja wa vita.