Jinsi ya kutoa salamu katika uislamu


image



MAkala hii itakwenda kukufundisha jinsi ya kutoa salamu kwenye uislamu

يُسْتَحَبُّ أنْ يَقُولَ المُبْتَدِئُ بالسَّلاَمِ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ . فَيَأتِ بِضَميرِ الجَمْعِ ، وَإنْ كَانَ المُسَلَّمُ عَلَيْهِ وَاحِداً ، وَيقُولُ المُجيبُ : وَعَلَيْكُمْ السَّلاَمُ وَرَحْمَةُ الله وَبَرَكَاتُهُ ، فَيَأتِي بِوَاوِ العَطْفِ في قَوْله : وَعَلَيْكُمْ .

Inapendeza aseme mwenye kuanza na salamu: "Assalaamu 'Alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh." kwa dhamiri ya wingi japokuwa mwenye kusalimiwa ni mmoja: Na mwenye kujibu atasema: "Wa 'Alaykumus Salaam wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh."

 

Hadiyth – 1

عن عِمْرَان بن الحصين رضي الله عنهما ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ ثُمَّ جَلَسَ ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( عَشْرٌ )) ثُمَّ جَاءَ آخَرُ ، فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ ، فَقَالَ : (( عِشْرُونَ )) ثُمَّ جَاءَ آخَرُ ، فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ الله وَبَركَاتُهُ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ ، فَقَالَ : (( ثَلاثُونَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema 'Imraan bin Al-Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akasalimia kwa kusema: "Assalaamu 'Alaykum." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na yule mtu akakaa chini. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Kumi." Kisha alikuja mtu mwingine akasema: "Assalaamu 'Alaykum wa Rahmatullaah." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na yule mtu akakaa, naye akasema: Ishirini." Kisha akaja mwingine, akasema: "Assalaamu 'Alaykum wa Rahmatullaah wa Barakaatuh." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na yule mtu akakaa, naye akasema: Thelathini." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عائشةَ رضي الله عنها ، قالت : قَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( هَذَا جِبريلُ يَقْرَأُ عَلَيْكِ السَّلاَمَ )) قالت : قُلْتُ : وَعَلَيْهِ السَّلاَمُ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Huyu Jibriyl anakusalimia." Akasema ('Aaishah): Nikasema: "Na juu yake Amani na Rehma za Allaah na Baraka Zake." [Al-Bukhaari na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أنسٍ رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا تكلم بِكَلِمَةٍ أعَادَهَا ثَلاثَاً حَتَّى تُفهَمَ عَنْهُ ، وَإِذَا أتَى عَلَى قَوْمٍ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ سلم عَلَيْهِمْ ثَلاَثاً . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akizungumza alikuwa akirudia maneno mara tatu mpaka afahamike. Na alipokuwa akija kwa watu na kuwasalimia alikuwa akirudia mara tatu (Alikuwa akifanya hivi ikiwa watu ni wengi). [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 4

وعن المِقْدَادِ رضي الله عنه في حدِيثهِ الطويل ، قَالَ : كُنَّا نَرْفَعُ للنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم نَصِيبَهُ مِنَ اللَّبَنِ ، فَيَجِيءُ مِنَ اللَّيْلِ ، فَيُسَلِّمُ تَسْلِيماً لاَ يُوقِظُ نَائِماً ، وَيُسْمِعُ اليَقْظَانَ ، فَجَاءَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَسَلَّمَ كَمَا كَانَ يُسَلِّمُ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Al-Miqdaad (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika hadiyth yake ndefu amesema: Tulikuwa tukimpelekea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) fungu lake la maziwa, kwa hiyo anakuja usiku anasalimia kusalimia kusikoamsha mwenye kulala, Anamsikizisha aliye macho, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja akasalimia kama alivyokuwa akisalimia." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن أسماء بنتِ يزيد رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ في المَسْجدِ يَوْماً ، وَعُصْبَةٌ مِنَ النِّسَاءِ قُعُودٌ ، فَألْوَى بِيَدِهِ بالتسْلِيمِ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Asmaa' bint Yaziyd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita Msikitini siku moja na kipote cha wanawake kilikuwa kimekaa, alitoa ishara ya kuwasalimia kwa kuinua mkono wake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي جُرَيٍّ الهُجَيْمِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : أتيت رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فقلتُ : عَلَيْكَ السَّلامُ يَا رسول الله . قَالَ : (( لاَ تَقُلْ عَلَيْكَ السَّلامُ ؛ فإنَّ عَلَيْكَ السَّلاَمُ تَحِيَّةُ المَوتَى )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) ، وَقَدْ سبق بِطُولِهِ .

Amesema Abu Jurayyi Al-Juhaymiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nikamwambia: "Alaykas Salaamu Yaa Rasuulallaah" "Amani iwe juu yako ee Rasuli wa Allaah." (Nabiy) Akasema: "Usiseme 'Alayka Salaam, kwani "Alaykas Salaam ni salamu kwa wafu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]



Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-07

RELATED POSTS

picture

AL-ARBA’UWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 1: NIA

huu ni mwanzo wa kitabu hiki cha Matn arbaina Naway
picture

AL-ARBA-UWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 5: KUJIEPUSHA NA UZUSHI KATIKA DINI

Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini
picture

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 6: UBAINIFU WA HALALI NA HARAMU

Post hii inakwenda kukupa tahadhari juu ya mambo ya halali na mambo ya haramu.
picture

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 4: UUMBWAJI WA MWANADAMU

HAdithi hii itakufundisha namna ambavyo mwanadamu anapitia hatuwa mbalumbali tumboni mwa mama yake
picture

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 3: NGUZO ZA UISLAMU

Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu
picture

AL-ARBA UWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 7: NASAHA KATIKA DINI

Post hii itakufundisha umuhimu wa nasaha katika dini
picture

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 2: UJIO WA JIBRIL KWA MTUME (S.A.W)

Hii ni hadithi ya pili katika kitabu cha Arbain Nawawiy