Je manii ni twahara au najisi?


image



Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis

Wanazuoni wamehitilafiana juu ya suala hili kwa kauli mbili:

 

Kauli ya kwanza:

 

Inasema kwamba manii ni najsi. Kauli hii ameisema Abu Haniyfah na Maalik, nayo ni riwaya iliyopokelewa toka kwa Ahmad. Wamelitolea dalili hilo kwa Hadiyth ya 'Aaishah alipoulizwa kuhusu manii yaliyoingia kwenye nguo akasema:  "Nilikuwa nikiyaosha kwenye nguo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kisha anatoka moja kwa moja kwenda kuswali huku athari ya doa la maji  ikiwa katika nguo yake". [Imepasishwa na Al-Bukhaariy (230) na Muslim (289)].

Na kuosha hakuwi ila kwa kitu najsi.

 

 

Kauli ya pili:

 

Wenye kauli hii wamesema kuwa manii ni twahara. Kati ya waliolisema hilo ni Ash-Shaafi'i na Daawuud. Hii ni riwaya Swahiyh zaidi kati ya riwaya mbili zilizopokelewa toka kwa Ahmad. Wamelitolea dalili hilo kwa Hadiyth ya 'Aaishah kuhusu manii, aliposema: "Nilikuwa nikiyakwangua kuyatoa kweye nguo ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)”. [Hadiyth Swahiyh: Muslim (288)].

 

Na kwa Hadiyth yake nyingine kwamba mgeni alishukia kwa 'Aaishah na akawa anaiosha nguo yake. 'Aaishah  akamwambia: "Ilikuwa inakutosha tu ikiwa utayaona, uoshe mahala pake, na ikiwa hukuyaona, unyunyizie maji kuzungukia hapo. Na bila shaka umeniona nikiyakwangua kwa umakini kwenye nguo ya Nabiy wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na yeye akaiswalia". [Hadiyth Swahiyh: Muslim (288)].

 

Na kutosheka kuyakwangua, kunaonyesha kuwa manii ni twahara.

 

Wenye kusema kuwa manii ni najsi, wamejibu kuwa kukwangua  hakuonyeshi kuwa manii ni twahara, bali kunaonyesha namna ya kuyatwaharisha kama vinavyotwaharishwa viatu kwa kuvipangusa katika mchanga.

 

Hili linajibiwa  kwa kusema kuwa 'Aaishah  alipoyakwangua manii mara moja na kuyaosha mara nyingine, hilo halihukumii kuwa ni najsi, kwani nguo inaoshwa kwa kuingia makamasi, mate au uchafu. Na hivi ndivyo walivyosema baadhi ya Maswahaba kama vile Sa'ad bin Abiy Waqqaasw, Ibn 'Abbaas na wengineo. Wamesema:

"Manii ni kama makamasi na mate, jisafishe uyaondoshe japokuwa kwa kijiti." [Majmuu Al-Fataawaa (21/605)].

 

Na kwa hili, inadhihiri kuwa kitendo cha 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa), kinaingia katika mlango wa kujichagulia namna ya kusafisha. [Sharhu Muslim].

 

Hukmu ya kuwa manii ni twahara inapata nguvu tunapojua kwamba Maswahaba walikuwa wakiota wakati wa enzi ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na manii hayo yalikuwa yakiingia katika miili na nguo za baadhi yao. Na lau kama yangelikuwa ni najsi, basi ingelikuwa ni lazima kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) awaamrishe wayasafishe kama alivyowaamrisha wastanji. Na kwa kuwa hakuna yeyote aliyelinukuu hili, inajulikana kwa yakini kuwa kuyaondosha hakukuwa ni jambo la lazima.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi. [Majmuu Al-Fataawaa (21/604)].



Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-09-28

ZOEZI

Jaza maswali yote ama baadhi kisha bofya kitufe za kutuma majibu hapo chini.



1 : Maswahaba kama vile Sa'ad bin Abiy Waqqaasw, Ibn 'Abbaas wanakubaliana kuwa manii ni __________





2 : Abu Haniyfah na Maalik wamekubaliana kuwa manii ni ___________





3 : unaweza kuondoa manii kwa njia zifuatazo isipokuwa __________





4 : "manii ni twahara" kauli hii imekubaliwa na maimua wafuatao ________





5 : "Manii ni kama makamasi na mate" kauli hii inamaanisha kuwa manii ni _________







RELATED POSTS

picture

MAMBO YALIYO HARAMU KWA MWENYE HEDHI NA NIFASI

Katika post hii utakwenda kujifunza mambo ambayo ni haramu kwa mwanamke aliye na hedhi na nifasi
picture

AINA ZA NAJISI NA TWAHARA KATIKA UISLAMU

Post hii inakwenda kukufundisha aina za najis. Pia utajifunza aina za twahara katika uislamu
picture

JINSI YA KUTAWADHA KAMA AALIVYOTAWADHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume
picture

JINSI YA KUTWAHARISHA AINA MBALIMBALI ZA NAJISI

Kila najisi ina namna yake ya kutwaharisha, hata hivyo namna hizo hufanana. Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutwaharisha najisi mbalimbali.
picture

TWAHARA NA UMUHIMU WAKE KATIKA UISLAMU

Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria. Pia utajifunza umuhimu wake
picture

MAMBO YANAYOWEZA KUTOA UDHU WAKO

Post hii itakufundisha mambo ambayo yanabatilisha udhu.
picture

ZIJUWE NGUZO TANO ZA UISLAMU NA MAANA ZAKE KATIKA SHERIA YA UISLAMU

Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake.
picture

FADHILA ZA UDHU YAANI FAIDA ZA UDHU

Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu