Al-Arbauwn An-Nawawiyyah hadithi ya 6: ubainifu wa halali na haramu


image



Post hii inakwenda kukupa tahadhari juu ya mambo ya halali na mambo ya haramu.

 عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُما قَالَ : سمعتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:  ((إن الْحَلالَ بَيِّنٌ وَإنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ وَبَيْنَهُما أمورٌ مُشْتَبِهَاتٌ لا يَعْلَمُهُنَّ كَثيِرٌ مِنَ الناسِ، فَمَنِ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ فَقَد اسْتَبْرَأَ لِدِينِهِ وَعِرْضِهِ، وَمَنْ وَقَعَ في الشَّبُهاتِ وَقَعَ في الْحَرَامِ، كالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى يُوشِكُ أَنْ يَرْتَعَ فِيهِ، أَلا وَإنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمىً أَلا وَإنَّ حِمَى الله مَحَارِمُه، أَلا وَإنَّ في الجَسَدِ مُضْغَةً إذَا صَلَحَتْ صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ وإذَا فَسَدَتْ فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلا وَهِيَ الْقَلْبُ))  رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ  وَمُسْلِمٌ

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu  ‘Abdillaah An-Nu’umaan bin  Bashiyr  (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alisema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika halaal imebainika na haraam imebainika na baina ya mawili hayo mna yenye kutia shaka. Wengi miongoni mwa watu hawayajui. Basi atakayejiepusha yenye kutia shaka, atakuwa amejiepushia shaka katika Dini yake na heshima yake. 

 

Na Atakayetumbukia katika yenye kutia shaka, ataingia kwenye haraam. Kama mchunga anayechunga kando ya mipaka, ni haraka kulisha humo (mpaka mwingine wa watu). Zindukeni!  Kila mfalme ana mipaka. Zindukeni! Kwa yakini mipaka ya Allaah ni haraam Alizoziharamisha. 

 

Zindukeni! Kwa yakini katika mwili mna kinofu cha nyama, kinapokuwa salama, mwili wote unakuwa salama. Kinapoharibika, mwili wote unaharibika. Zindukeni! Kinofu hicho ni moyo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 



Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-09-09

RELATED POSTS

picture

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 4: UUMBWAJI WA MWANADAMU

HAdithi hii itakufundisha namna ambavyo mwanadamu anapitia hatuwa mbalumbali tumboni mwa mama yake
picture

AL-ARBA UWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 7: NASAHA KATIKA DINI

Post hii itakufundisha umuhimu wa nasaha katika dini
picture

AL-ARBA-UWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 5: KUJIEPUSHA NA UZUSHI KATIKA DINI

Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini
picture

JINSI YA KUTOA SALAMU KATIKA UISLAMU

MAkala hii itakwenda kukufundisha jinsi ya kutoa salamu kwenye uislamu
picture

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 3: NGUZO ZA UISLAMU

Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu
picture

AL-ARBA’UWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 1: NIA

huu ni mwanzo wa kitabu hiki cha Matn arbaina Naway
picture

AL-ARBAUWN AN-NAWAWIYYAH HADITHI YA 2: UJIO WA JIBRIL KWA MTUME (S.A.W)

Hii ni hadithi ya pili katika kitabu cha Arbain Nawawiy