Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini
عن أُمِّ المُؤمِنينَ أُمِّ عَبْدِ الله عائِشَةَ رَضي اللهُ عنها قالَتْ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ أَحْدَثَ في أَمْرِنا هذا ما لَيْسَ منهُ فَهُوَ رَد)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ : ((مَن عَمِلَ عَمَلاً لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ ))
Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini Ummu Abdillaah ‘Aishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayezusha katika jambo letu hili (la Dini) lolote ambalo halimo humo litarudishwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Muslim: ”Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika Dini) basi kitarudishwa.”
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-09-09