Katika hadithi hii utakwenda kujifunza nguzo za uislamu
Kutoka kwa Abuu Abdir-Rahmaan Abdillaah Ibn 'Umar Ibn Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zaka na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm Ramadhwaan.”
[Al-Bukhaariy na Muslim]
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-09-09