9.UTARATIBU WA LISHE KWA WAGONJWA
Wagonjwa. Wagonjwa wapewe vyakula vyenye viinilishe vyote ili kuwezesha miili yao kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi Hasa hasa vitamini kwa wingi Matunda na mboga za majani ni muhimu kwa wagonjwa iliwaweze kupata madini na vitamini muhimu kwa ajili ya miili yao. Wagonjwa pia wapewe maji ya kutosha ili kuwezesha miili yao kufanya kazi vizuri.

Matunda yatamuwezesha pia kupambana na maradhi au kupunguza uwezekano wa kuendelea kuuguwa. Wagonjwa wapate muda wa kutosha kwa ajili ya kulala na wafanye mazoezi kulingana na hali zao.

Pia kuna vyakula maalumu vinapendelewa kwa kulingana na aina ya ugonjwa alionao. Muone daktari akushauri vyakula vya kuvila kulingana na ugojwa ulonao.