6.UTARATIBU WA LISHE KWA WATOTO
Kila mtu anatkiwa ale chakula kwa kulingana na mahitaji ya mwili wake. Motto anatakiwa ale vyakula maalumu kwa ajili ya kumuwezesha kukuwa vizuri umbo na kiakili. Halikadhalika mama wajawazito wanatakiwa wale vyakula maalumu kwa ajili ya kuwezesha afya ya mama na motto. Wazee, vijana, wafanyakazi na wagojwa wanatakiwa wale vyakula kulingana na hali zao. Hapa tutakuletea lishe kwa kulingana na makundi ya watu.
Watoto wanatakiwa kula vyakula vya protinikwa wingi ili kuwezesha ukuaji wao wa mwili na tishu. Upungufu wa protini unaweza kumpelekea mtoto awe na ukuaji hafifu. Kwa ukuaji mzuri wa meno na mifupa mtoto anatakiwa apewe vyakula vya madini kama madini ya kashian(calcium) upungufu wa madini haya huenda mtoto akawa na ukuaji mbaya wa mifupa. Madini ya zink ni muhimu pia katika ukuaji wa mtoto.
Vitamini B12 ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha utengenezwaji wa seli nyekundu za ndamu. Pia ijulikane kuwa ukuaji mzuri wa mtoto unategemea kuwepo na damu ya kutosha mwilini ili kuweza kusafirisha gesi ya oxygeni pamoja na viinilishe(nutrients) ndani ya mwili.
Vitamini ni muhimu sana katika ukuaji wa mtoto. Watoto wapewe vyakula vyenye vitamini C kwa wingi kama machungwa, mapapai. Vitamini hivi vinamuwezesha mtoto kutengeneza kinga ya mwili ili kuweza kupamabana na maradhi. Watoto pia wanatakiwa wapewe vyakula vya wanga kwa wingi ili waweze kupata nguvu ya kutosha kuweza kufanya shughuli zao kama mazoezi ya kutambaa, kukumbia, kusimama n.k.