5.VYAKULA NA UGONJWA WA KISUKARI

Chakula; mgonjwa wa isukari anatakiwa ale chakula kisicho na mafuta mengi, ckisicho na chumvi wala sukari nyingi. Kuala matunda na mboga za majani. Hakikisha unakula katika muda maalumu siku zote pia angalau upate chakula mara tatu kwa siku kula chakula kisicho kobolewa. Pia hakikisha unakunywa maji mengi zaidi kwa siku Mazoezi; hakikisha unafanya mazoezi si chini ya mara tatu kwa wiki.

Hii huenda ikasaidia kupunguza usito na kuthibiti kiasi cha sukari ndani ya mwili wako. Pia kufanya mazoezi ni muhimu kwa afya yako kwa ujumla. Mazoezi yanaweza kupunguza mlundikano wa mafuta kwenye ngozi na mishipa yta damu. Hali hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa kuapata strock na shambulio la moyo.

Dhibiti uzito wako; hakikisha kuwa hauna uzito usio wa kawaida. Yaani hakikisha kuwa unapunguza uzito kama uzito wako ni mkubwa. Pata ushauri wa daktari kuhusu uzito wako kama unakufaa au umezidi kulingana na afya yako. Zipo njia nyingi za kupunguza uzito kupitia vyakula, mazoezi na nyinginezo. Muone daktari au pata ushauri kwa walio na ujuzi wa njia salama ya kupunguza uzito.

Tumia dawa; kama kisukari kimeshindikana kuthibitiwa kwa nyia hizo hapo juu anza kutumia dawa. Zipo dawa maalumu kwa wagonjwa wa kisukari. Pia inashauriwa kuwa mtu aanze kutumia dawa za kumeza kabla ya zile za sindano. Muone daktari atakupatia dawa hizo kulingana na afya yako. Watu wengi wanakuwa wavivu wa kunywa dawa lakini kwa baadhi ya magonjwa uvivu huu ni hatari zaidi kwa afya zao.