(xii)Huepuka zinaa na tabia za kizinifu

(xii)Huepuka zinaa na tabia za kizinifu

Waumini wa kweli waliofuzu hujihifadhi na zinaa au hujiepusha kufanya jimai nje ya mipaka aliyoiweka Allah (s.w).


Hatua ya kwanza ya kujilinda na zinaa ni kujiepusha na vishawishi vyote vinavyokurubisha watu kwenye zinaa.


Muumini wa kweli hutekeleza pasina kusita ile amri ya Allah(s.w) ya katazo kuwa: Wala usiikaribie zinaa; kwa hakika huo ni uchafu na ni njia mbaya kabisa (17:32)