(iii)Huongezeka imani yao kwa kusoma na kufuata Quran Wanaposoma aya za Mwenyezi Mungu huwazidishia imani. Kwa maana nyingine, waumini wa kweli hufuata mwongozo wa Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Hawako tayari kufanya jambo lolote kinyume na mwongozo wa Allah (s.w).