(i) Wana yakini kuwa Allah (s.w) yupo
Waumini wa kweli huwa na yakini nyoyoni mwao juu ya kuwepo Allah (s.w) na Mtume wake. Yaani wanashuhudia kwa
dhati nyoyoni mwao kuwa Allah (s.w) ni Mola wao pekee na
53
Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake wa mwisho na katika matendo yao yote huishi kwa kufuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na daima hukumbuka msisitizo wa aya ifuatazo:
“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini,Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa).” (33:36)