Sura ya Pili
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA DINI


Maana ya Dini kwa Mtazamo wa Makafiri
Makafiri wanatafsiri dini kuwa ni:
(i)“Imani inayohusiana na mambo ya kiroho baina ya binaadamu na Mwenyezi Mungu au njia ya kuhusiana na Mwenyezi Mungu” (Kamusi ya Kiswahili sanifu)
(ii)“Imani juu ya kuwepo Mungu Muumba aliye muweza na mwenye nguvu juu ya kila kitu, Mmiliki wa ulimwengu, ambaye amempa binaadamu roho ambayo huendelea kuishi baada ya kifo cha mwili” (Oxford Advanced Learner’s Dictionary of Current English).Kutokana na tafsiri hii ya dini iliyonukuliwa kutoka kwenye kamusi ya Kiswahili na ya Kiingereza, tunajifunza mambo makubwa mawili:
Kwanza, kwa mtazamo wa makafiri dini inahusiana na imani ya kuwepo Allah (s.w).


Hivyo wenye dini ni wale tu wanaoamini kuwepo kwa Allah (s.w), na wale was ioamini kuwepo kwake hawana dini. Ni katika mtazamo huu V. I. Lenin katika kitabu chake “Socialism and Religion (Ujamaa na Dini) amedai:
“Everybody must be absolutely free to profess any religion he pleases or no religion whatever; i.e. to be an atheist which every socialist is as a rule...”
Tafsiri:
“Kila mtu hanabudi kuwa huru kabisa kufuata dini yoyote anayotaka au asiwe na dini kabisa, yaani awe kafiri, jambo ambalo inambidi kila mjamaa awe kama sheria...”
Pili, kwa mtazamo wa makafiri, dini inahusiana na mambo ya kiroho au ulimwengu wa kiroho tu, na haihusiani kabisa na


ulimwengu wa kimaada (wa vitu). Ni kwa mtazamo huu kwa makafiri, matendo ya wafuasi wa dini yamegawanywa katika sehemu mbili, matendo ya dini na matendo ya dunia. Katika mtazamo huu pia Waislamu hulaumiwa na makafiri kuwa wanachanganya dini na siasa, dini na uchumi; dini na utamaduni, na kadhalika.