Zoezi - 11. Elimu ni nini?2. “Sema, Je wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?...” (39:9)
Ni kwasababu gani wanaojua hawawi sawa na wasiojuwa?3. Unatoa maoni gani iwapo wanaojua na wasiojua wakawa sawa kiutendaji?4. Toa maelezo yenye ushahidi wa Qur-an kuonyesha kuwa:(a)Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa binaadamu na Mola wake.(b)Kutafuta elimu ni amri ya kwanza kwa bin a adam u.5. Onyesha kwa ushahidi wa Qur-an kuwa katika Uislamu mgawanyiko wa elimu katika “elimu ya dini” na “elimu ya dunia” haukubaliki.6. “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba.” (96:1) Kusoma kwa jina la Mola wako maana yake nini?7. “.... Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha mwanaadamu kwa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu mambo aliyokuwa hayajui”. (96:3-5)
Orodhesha njia tano anazozitumia Allah (SW) katika kuwasiliana na wanaadamu.8. Elimu yenye manufaa kwa binaadamu ni ile .................................9. Eleza sababu tatu zinazopelekea elimu kupewa nafasi ya kwanza katika Uislamu.
*******************************


Chanzo cha Elimu ni Allah (s.w) Kama tunavyojifunza katika surat ‘Alaq (96:4-5), chanzo cha elimu au mkufunzi wa binadamu ni Allah (s.w). Allah (s.w) huwasiliana na binadamu na kuwaelimisha kwa kutumia mojawapo ya njia zifuatazo zilizoainishwa katika aya ifuatayo: Na haikuwa kwa mtu kwamba Mwenyezi Mungu anasema naye ila kwa il-hamu (anayetiwa moyoni mwake) au kwa nyuma ya pazia au humtuma mjumbe (Malaika) naye humfunulia kiasi anachotaka kwa idhini yake (Allah), bila shaka yeye ndiye aliye juu mwenye hekima.” (42:51). Aya hii inatufahamisha kuwa binaadamu hupata habari kutoka kwa Allah (s.w) kwa njia tatu zifuatazo: (a)Il-hamu(Intution). (b)Nyu ma ya pazia. (c)Kutumwa Malaika na kufikisha ujumbe kama alivyotumwa. Pia katika Qur-an tunafahamishwa njia mbili nyingine anazozitumia Allah (s.w) katika kumfikishia binaadamu ujumbe kutoka kwake: (d)Ndoto za kweli (ndoto za Mitume).