ukiwa na kisanduku chako mkononi unatoka kwenye kichaka. Kwa hakika umechoka sana. Kitu cha kwanza ni kufungua ile
barua. Kwa taratibu unaanza kuifungua. Unakutana na wino mwekundu unawaza unajipajibu kuwa
:BARUA IMEANDIKWA KWA KUTUMIA DAMU".
Ni maneno machache tu yaliyoandika. Kwani barua ilisomeka hivi:-
KWAKO KIJISU WA MSUSILE
BABA YAKO NINAYE NA NINAHITAJI PESA YANGU. NI MUDA MCHACHE NINAOKUPA
KABLA YA JUWA KUPOTEA LETA PESA YANGU UOKOE SHINGO YA BABA YAKO
FROM: NGARIAMBO, MAFIA WA LUTENYE
Kijisu wa msusile ni jina lako linaloambatana na mila za kabila lenu. unashangaa kuona kuwa huyu mtekaji
Hakukuita jina lako bali ametumia jina la kimila. Hapa unajipa matumaini kuwa huyu ni mtu anaye kufahamu.
"KIJISU WA MSUSILE" unaamuwa kulikubali jina hili na kuendelea kujiita hivyo.
Ukiwa katika hali ya kutafakari, unaona muembe wenye maembe yaliyowiva. ijapokuwa chini hakuna embe
lililoanguka, lakini juu uanashuhudia maembe kadhaa yakining'inia. Ukiwa na njaa na uchovu unakaa chini kwenye
kivuli cha mti mdog karibu na muembe.
Unaweka chini kisanduku na kuamua:
Kutungua maembe
kufungua kisanduku