Unashuka juu ya mti kisha unaelekea moto ulipo. Unajaribu kukoleza moto zaidi na kuongeza miti ya moshi. Unaanza kutoa miiba ya nyuki
mgongoni na kichwani. Baadhi ya sehemu za mwili wako tayari zimeanza kuvimba. Umeshapata nguvu baada ya mapumziko.
Unachukuwa mwenge mkubwa wa moto na unakwea mti, unaendelea kuchoma. nyuki kadhaa wanafanikiwa kukuuma, lakini unavumilia. Hatimaye unafanikiwa kutoka
na malala matatu yalojaa asali. Unajisemea sasa njaa utakwenda kwisha. Unashuka na kuuendea moto wako, unaonja unakundua ni asalinzito sana
na iliyo bora.