SURA YA KWANZA

Unawaza huna kitu cha kutumia ili ule asali. Unajichunguza unagunduwa kuwa umevaa nketi ndefu na jacket la mikono mirefu na lenye kofia ngimu. Unajidundua ndani ya jacketi kuna kiziba pua ulichokitumia wakati unazibua choo. Hamu ya kula asali inakujia, unajiridhisha kuwa kwa mavazi uliyo nayo nyuki hathubutu kukuuma.

Kabla hujafanya chochote unagundua kuwa kuna kitu kigumu kwenye sidiria yako. Unatowa unakuta ujumbe wenye mistari kama minne uloandikwa kwa wino mwekundu. Wakati unataka kuusoma ghafla ndege wawili wanaopigana huku wanaelekea karibu na pale ulipo mbele ya mzinga. kwa umakini unashikwa na butwaa kisha unaamua ku..

Soma ujumbe     subiri kwanza