41..Dua ya kusema unapoanza kula Unapoanza kula hunabudi kusema: “Bismillaahi" “Kwa jina la Allah" Na ukisahau kusema hivyo wakati wa kuanza, ukikumbuka wakati unaendelea kula sema: “Bismillahi fiy awwalihi wa-aakhirihi" “Kwa jina la Allah katika mwanzo wake na mwisho wake" 24.Dua ya kushukuru baada ya kula “Al-hamdulillahilladhii atw-a'maniy hadhaa warazaqaniyhi min ghayri hawlin minniy walaa quwwatin" “Shukurani zote anastahiki Allah ambaye amenilisha chakula hiki bila ya uwezo wala nguvu yoyote kutoka kwangu."

42.Dua ya mgeni kumuombea mwenyeji aliye mlisha chakula “Allahumma baarik-lahum fiymaa razaq-tahum, wagh-fir lahum war-hamhum." 483 Ee Allah, wape baraka kwa hicho ulicho wapa,wasamehe na warehemu."

43.Dua ya kuleta baada ya kupiga chafya Unapopiga chafya hunabudi kusema: “Al-hamdulillaahi" “Sifa zote anastahiki Allah." Kisha ndugu zako Waislamu watasema: “Yar-hamuka llahu." “Allah akurehemu." Kisha utajibu kwa kusema: "Yah-diykumullahu wayusw-lihi baalakum." "Allah akuongozeni na kuwasahilishia mambo yenu." Kama anaeambiwa ni mwanamke
“Utasema yar-hamuki llahu”

44.Dua ya kuwaombea maharusi (waliooana) “Baarakallahulaka,wabaaraka a'layka,wajamaa'baynakumaa fiy khayrin" “Allah akubariki wewe na yeye (mkeo/mumeo) na awaunganishe katika kheri."

45.Dua ya kuleta unapoanza kufanya tendo la ndoa “Bi smi l lahi A l lahumma jannib-nashshay - twaana wajannibish-shytwaana maarazaq-tanaa". “Kwa jina la Allah, Ee Allah muweke shetani mbali nasi na muweke shetani mbali na hicho ulichoturuzuku."

46.Dua ya kuleta unapopandwa na hasira “Au'udhubillaahi minash-shaytwaani rrajiimi" “Najikinga kwa Allah na shetani aliyelaaniwa."

47.Dua ya kuleta mwisho wa kikao (mkutano) "Sub-haanaka llahumma wabihamdika, ash-hadu an-laa ilaha illa anta as-taghfiruka wa-atuubu ilayka." "Utukufu ni wako, Ee Allah, nakutukuza. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila wewe. Nakuomba msamaha na ninatubia kwako."

48.Dua unayomuombea yule aliyekufanyia jambo zuri “Jazaka llahu khayran" “Allah akulipe kheri."

49.Dua ya kuomba kuepushwa na shirk “Allahumma inniy au'udhubika an-ush-rika bika waanaaaa'lamu, wa-astagh-firuka limaa laa-aa'lamu." "Ewe Allah, najikinga kwako nisikushirikishe huku nikijua na naomba unisamehe kwa lile (baya) nitakalolifanya bila kujua."

50.33.Dua ya kupokelea sadaqa au zawadi "Baarakallahu fiykum." “Baraka za Allah ziwe juu yenu." Na aliyetoa zawadi/swadaqa na akaombewa hivi atajibu "Wafiyhim baarakallahu." "Pia Allah awabariki."