pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE

Basi tambueni enyi rafikizangu kuwa mimi na waziri wangu huyu hatutokani na familia za kifalme wala mimi baba yangu hahusiani hata kidogo na ufalme. Tumepata vyeo vyetu hivi wakati tukiwa katika hali ngumu ya maisha. Mimi na waziri wangu tulipata vyeo vyetu tulipojifanya tunaswali baada ya kukimbizwa kuwa wezi tulipokuwa tunaiba msikitini. Bila shaka hamjaelewa nini ninamaanisha. Ila kwa ukweli zaidi mambo yalikuwa hivi

Tulikuwa ni watoto yatima tuliofiwa na wazazi wetu tungali wadogo. Sikuzote tuliitegemea chakula kwa kuokota ama kuomba. Tulianza tabia ya wizi, ingali tunajuwa kuwa wizi ni haramu, na ukikamatwa utakatwa mkono kwa mujibu wa sheria za dini. Tukiwa hatuna jinsi ya kutupatia rizki tulikuwa tukiiba vitu kwa watu na kuuza kujipatika pesa.i mwingine tunanakosa hata cha kuiba hivyo tunalala bila kula. Wakati mwengine tulikuwa tukipigwa pindi tunapokwenda kuiba.

Tulianza kujishughulisha na shuhuli za kufanya biashara ndogondogo ijapokuwa hali haikuwa nzuri pia. Tuliamua pia kujikita katika kibeba taka majumbani hali ambayo pia haukuwa na uwezo wa kutufanya tupate riziki kwa unafuu. Kwa hakika maisha yetu yalikuwa ni magumu sana. Hatukujuwa kusoma wala kuandika. Na kwa bahati mbaya tulisomaga dini tukiwa watoto na kukimbia masomo hivyo tulifanikiwa kujuwa kuswali na mambo machache tuu.

Wakati mwingine tulijiingiza katika misafara ya walinganiaji dini na kujifanya na sisi tukilingania, ila lengo ni kupata unafuu wa maisha lakini tulipogundulika tulikuwa tukifukuzwa. Maisha yaliendelea kuwa ni magumu. Unapoingia mwezi wa ramadhani sisi kwetu ilikuwa ni kama sikukuu maana tuliweza kushiba kwa kufuturishwa na mabaki ya ftari kwa matajiri na wenye uwezo tuliweza kuyatumia. Ila mwezi unapoisha hali ilirudi vilevile.

Basi mambo yalikuwa hivyo na masiku yakawa yanaendelea. Ilitokea sikumoja tulikosa cha kukila na tukakosa hata nafasi ya kuiba kiti chochote cha kutuingizia kipato au kutunisha matumbo yetu. Basi siku ile tuliamua kuingia msikitini na kuanza kufungua vibubu na masanduku ya sadaka pale msikitini ili kuiba sadaka. Haikupita muda tukasikia miguu ya watu wanakuja hivyo tulishindwa kuwahi kujificha na tukaamua kujifanya tunaswali. Mimi nikiwa imamu na waziri wangu huyu alikuwa ni maamuma katika swala yetu feki.

Basi kundi lile likaja mpaka msikitini na walip[otuona tunaswali wakawa wanatunyooshea vidole na wengine wakawa wanasema hawa ndo wenyewe, hawa ndo wanafaa. Basi nikiwa imamu wa swala feki nilijitahidi kurefusha swala lakini wale watu hawakukata tamaa na wakaendelea kusubiri. Hatimaye nikakata tamaa na kumaliza swala ile. Basi tulipotoa salamu tu wale watu wakatuita na kutuchukuwa kwenda kwa mfalme na kutuambia kuwa mfalme anatuita.

Kwakweli hatujawahi kuiba kwa mfalme hata siku moja hivyo tulipata woga sana na kuhisi leo ndo mikono yetu inakwenda kukatwa. Tulipofika kwa mfalme wale watu mmoja wao akasema “muheshimiwa mfalme tumetafuta sehemu zote kwa siku nyingi lakini tumewapata hawa, na huyu alikuwa ndo imamu na mwenzie maamuma. Bale nilitamani kumwambia sisi sio wezi lakini nikasubiri kuona hatima yetu. Mfalme alifurahi kusikia vile na akaniambia ninakuozesha mwanangu. Nilishangaa kuona mfalme anasema maneno yale mbele ya wezi. Nikamuuliza sababu ya kufanya hivyo. Mafalme akanijibu kuwa yeye hana mtu wa kumrithi na ana mtoto wa kike tu, hivyo alikuwa akitafuta mtu wa kumuoa binti yake kwa sharti kuwa mtu hiyo awe anaswali hasa awe anaswali sunnah za usiku. Hivyo watu wake hawakupata mwenye sifa hiyo ila ameniona mimi,

Hapo nikamwambia mflme naomba muda kidogo, basi nikatoka nje na kuchukuwa udhu kisha nikasujudi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema alonipa. Yaani kwa swala feki ile amenipa neema ya kuwa mfalme je ingelikuwa ni swala ya kiukweli ni neema kiasi gani angenipa? Basi nikarudi kwa mfalme na kumwambia nimekubali. Na hapo ndoa ikapita na nikamuoa binti mfalme.

Kuanzia pale mimi na mwenzangu tukasahau wizi na haukupita muda mfalme alifariki na mimi nikawa mfalme wa nchi hii na rafiki yangu huyu nikamfanya kuwa waziri mkuu. Hivyo kwa kuwa tunatambua machungu ya maisha tumekuwa tukijitahidi kusaidia raia na tulikuwa tukitembea usiku kuona hali halisi ya maisha na kuwatambua wezi. Huwa tukiwapata wezi tunawapa kazi ili kuwasaidi. Hivyo imetokea jana tulipokuwa tukifanya uchunguzi wetu tukapita nyumbani kwenu. Hii ndio hadithi yangu na waziri wangu.