2; mbegu ya uhai uliyo changanyika Umbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuona lakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakini umbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLAH anavyotueleza;-

‘‘ kwa yakaini umbo la mbingu na ardhi ni kubwa kuliko umbo la mwanadamu’’[40:57]
Allah anatueleza kuwa amemuumba mwanadamu kwa mbegu ya uhai iliyochanganyika yaan ‘’nutfatin amshaaj ’ ’kama alivyosema
‘kwa hakika tumemuumba mtu kwa mbeguya uhai iliyo changanyika ’ ’ [76:2]

Kwa ufupi katika aya hii tunaelezwa kuwa mwanadamu ameumbwa kwa maji ya uzazi yaliyo changanyika. Wafasiri wa quran wamejaribu kuichambuwa vizuri aya hii kwa namna ambavyo Allah aliwajaalia. Tutaona pia jinsi gani aya hii invyolingana na uchunguzi wa kisayansi.

Uthibitisho wa kisayansi
Sayansi inakubaliana juu ya machanganyiko huu katika namna zifuatazo;-
1; uchunguzi wa kisayansi unaonesha kuwa ;-
Manii ni mchanganyiko wa mbegu za kiume yaani sperm na majimaji yatokayo katika tezi kama tulivyotaja hapo nyuma.
Mbegu sperm huchanganyika na majimaji hayo yenye mchanganyiko wa citric acid, prostaglandin, flavin, ascobic acid, ergothioneine, cholesterol, phosphase, hyaluronidase na sperm.

Kwa ufupi manii ni mchanganyiko wa mbegu za kiume yaani sperm ambazo hutengenezwa kwenye korodani na kisha husafiri wa kati wa ‘’ejaculation”kuelekea kwenye zile tezi ambazo zinazalizha yale majimaji mengine na kupatikana manii yaani semen. Kisha manii haya hutoka nje kupitia urethra wakati wa ‘’ejaculation’’na kama yataingia katika mji wa mimba yaani uterus na kufika katika mirija ya falopia huko mchanganyiko wa pili unatarajiwa kutokea kama tutakavyoona.

2; uchunguzi wa kisayansi pia unaonesha kuwa;-
Yai la mwanamke yaani ovumhutengenezwa kwenye ovary kisha baada ya kukomaa huingia katika mirija ya falopia kitendo hiki kinaitwa kitaalamu ovulation. Huko katika mirija ya falopia yai hili hukutana na sperm amazo ni mbegu za kiume na hapa ndo tunapata mchanganyiko wa pili.

Pia yai hili la mwanamke huwa linapatikana likiwa katika majimaji fulani kama zilivyo mbegu za kiume ambazo nazo hupatikana katika majimaji fulani. Ili mimba iweze kutungwa ni mpaka pale mbegu ya kiume sperm itakapochanganyika na yai la mwanamke yaani ovum tukio hili lote hutokea katika mirija ya falopia na kitaalamu kitendo hiki huitw ‘’fertilization’’

Yai la mwanamke huweza kusubiri mbegu ya kiume kwa muda wa masaa 48 tu likingoja kukutana na mbegu ya kiume katika mirija ya falopia. Na mbegu za kiume zinaweza kusubiri kwa muda wa masaa 78 zikisubiri kukutana na yai la mama katika mirija ya falopia. Endapo mbegu ya baba yaani sperm haitachanganyika na yai la mama yaani ovum mimba haiwezi kutokea yaani mtoto hawezi kupatikana lamda kwa njia ya miujiza. Kitendo hiki cha kukutana hizi mbegu mbili ndo fertilization au fusion. Kwa hali kama hii mchanganyiko usipopatikana tukio muhimu la menstrationlinatarajiwa kutokea kwa wanawake walio katika umri wa kupata mimba.

Kwa ufupi maelezo haya yanatupa ufahamu juu ya pale alipotuamb ia Allah kuwa ametuumba kwa maji yaliyochanganyika ili atujaribu. Bila shaka quran imeendana sahihi na uchunguzi wa kisayansi juu ya maelezo ya aya hii