2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZI
Uumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababu
maalumu ili tipate mazingatio. Kwani kila kitu ALLAH amejaalia kukiwekea sababu na
ndivyo atuambiavyo katika quran;- ‘’.. .na tukampatia njia ya kupatia kila kitu’’ [18:84].
Baada ya binadamu wa kwanzqa kuumbwa kwa ugongo allah akajaalia binadamu waliofuata
kuwaumba kwa mchanganyiko wa maji ya uzazi. Katika sehemu hii tutaona jinsi maji haya
yalivyoelezewa katika kupatikaniwa umbo la binadamu. Maji haya yanapatikana kwa baba na
kwa mama pia kama tutakavyoona katika kurasa za mbele.
Maji haya yapatikanayo kwa baba ndio yatachukuwa nafasi kubwa katika maelezo ya
uumbwaji wa mwanadamu. Kwa ufupi manii ambayo kitaalamu huitwa semen ambapo ndani
yake ndo kuna mbegu za uzazi ambazo kitaalamu huitwa spermyamezungumziwa katika
quran kwa namna mbalimbali ambazo zitatupatia mazingatio. Kwa mfano ALLAH ametaja
kuwa;-
1; maji yatokayo kwa kuchumpa
Miongoni mwa sifa za maji haya ya uzazi ALLAH ameyataja moja kwa moja katika quran
pale aliposema;-
‘ ameumbwa mwanadamu kwa maji yatokayo kwa kuchumpa. Yatokayo katikati ya na mifupa
ya mgongo mbavu ’ ’ [86:6-7].
hivyo maji haya yametajwa kuwa
1; yanatoka kwa kuchumpa
2; yanatoka katikati ya mifupa ya uti wa mgongo na mbavu.
Kwa ufupi maji yaliyotajwa hapo ni manii yaani semen ambayo ndani yake ndo kuna mbegu
za uzazi ambazo ni sperm. Pia itambulike kuwa maji yalayotajwa hapo yanatoka kwa
mwanaume na si kwa mwanamke
Uthibitisho wa kisayansi
Uchunguzi unaonesha kuwa 95% ya manii[semen] ni majimaji yatokayo kwenye tezi zilizopo
karibu na kibofu cha mkojo ambazo ni kama seminal vesicles, prostate na tezi zilizopo
kwenye mrija wa mkojo [urethra]. Tezi hizi ambazo hutoa manii ni sawa kabisa kusema zipo
katikati ya uti wa mgongo na mbavu.
Siotatizo kusema tezi hizo zipo katikati ya uti wa mgongo na mbavu kisa mbavu zipo juu
kwani hata kichwa kipo katik\ati ya mabega ijapokuwa kichwa kipo juu.
Pia uchunguzi wa kisayansi unathibitisha kuwa 2% ya manii ni mbegu za uzazi yaani sperm
ambazo hupatikana kwnye korodani[testes] na wakati wa kufikia ‘'ejaculation'' sperm
husafiri kutoka kwenye korodani na kuelekea kwenye hizo tezi na kuchasngsnyika pamoja na
kupatikana manii kisha manii husafiri kuelekea nje.
Manii kutoka kwa kuchumpa wakati wa ‘ejaculation na hukadiriwa yakiwa na mwendokasi
[speed] wa maili 28 kwa saa wakati sperm zenyewe husafiri kwa mwendokasi wa nchi 8 kwa
saa au 4 mphr.