8.Tikiti (watermelon).
Tunda hili pia ni katika matunda yenye vitamin C na A kwa wingi. Tafiti za kisayansi pia zinaonesha kuwa tunda hili lina antioxidant ambazo ni pamoja na lycopene, carotenoid na cucurbitacin E. Hizi husaidia katika kuzuia mwili usipate saratani au kupunguza athari za saratani.

Antioxidant zilizopo kwenye tunda hili husaidia kuzuia saratani ya mfumo wa mmengenyo wa chakula na kuota kwa vimbe ambazo ni viashiria vya saratani. Lycopene husaidia katika kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa zina uwezo wa kupunguza cholesterol na shinikizo la damu. Katika matunda yote tikiti linajulikana kuwa ndio tunda lenye maji mengi. Lina asilimia 92% ya maji.

Zaituni (olive).
Ni katika matunda yaliyojulikana toka zama za zamani sana. Tunda hili lina kiwango kikubwa cha cha vitamini E na madini ya copper na calcium. Pia tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa tunda hili lina antioxidantan ambayo husaidia katika kuimarisha afya ya moyo na ini na pia husasidia katika kuzuia uvimbe.

Pia tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya zaituni yana oleic acid yaani asidi ya oleik ambayo husaidia katika kuimarisha afya ya moyo pamojha na kuzuia kupata saratani. Pia tafiti zinaonesha kuwa tunda hili lina chembechembe ambayo husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa osteoporosis. Huu i ugonjwa wa unaowapata sana wazee, na huathiri mifupa na kuifanya dhaifu.

9.Chungwa (orange).

Embe ni katika matunda maarufu sana duniani kote. chungwa lina kiwango kikubwa cha vitamini C na madini ya potassium (potashiam). Pia embe ni chanzo kizuri cha vitamini B kama vile thiamine na folate.

Katika chungwa. kuna vitu vingi ambavyo husaidia sana katika afya. Kama vile flavonoid, carotenoid na citric acid. Citric acid husaidia katika kupunguza uwezekano wa kuweza kupa kupata matatizo ya figo (kidney stones). Embe pia husaidia katika kuzuia kupata maradhi ya anaemia.

10.Ndizi (banana).
Ndizi zina vitamin na madini, ndizi zina madini ya potassium kwa kiasi kikubwa sana. Moja katika sifa kuu ya ndizi ni kuwa na carb makeup. Carb ni ukijani uliopo kwenye ndiri ambayo haijaiva. Ukijani huu una starch kwa wingi ambao husaidia katika kuthibiti sukari kwenye damu. Na kuimarisha mmeng’enyo wa chakula.

11.Papai (papaya)
Papai ni katika matunda yanayoingiza afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina vitamin C na vitamini A kwa wingi pia kuna potassium na folate. Pia tafiti zinaonesha kuwa antioxidant aina ya lycopene iliyomo kwenye papai husaidia katika kuzuia kupata saratani.

Pia papai lina vitamin B, vitamin E na vitamin K. Pia lina madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper. Pia punje za papai ni dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo. Pia kwenye papai kuna protelytic enzymes hawa husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kum eng’enya chakula).