1.Zabibu (grapefruit).
Hili ni tunda ambalo lina historia kubwa kwenye maisha ya wanaadamu. Tunda hili linaweza kupatikana maeneo mengi duniani. Zabibu ni moja kati ya matunda yanayotambulika kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha Afya ya mwanadamu tka zamani sana.

Zabibu linatambuliwa kuwa ni chanzo kizuri sana cha vitamini na madini kwenye miili yetu. zabibu ni katika matunda ambayo yana vitamini kwa wingi kuliko mengi katika matunda ambayo tunayala. Itambulike kuwa vitamini na madini ni katika virutubisho muhimu vinavyofanya mwili wako kuwa madhubuti na afya njema sikuzote.

Tunda hili pia hitambulika kuwa na uwezo mkubwa wa kusaidia kupunguza uzito wenye madhara mwilini mwako. Itambulike kuwa uzito ukizidi mwilini kuna matatizo mengi ya kiafya unaweza ukayapata kama kupata maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Hivyo tunda hili husaidia katika kupunguza uzito mwilini mwako. Ni vyema ukala tunda hili kabla ya kula chochote.

Tunda hili pia linatambulika kuwa na uwezo wa kusaidia kuweka madhubuti insulini iwe katika hali ya kawaidi. Itambulike kuwa insulin ikisumbua huweza kusababisha ugonjwa wa kisukari. Pia tunda hili husaidia katika kudhibiti afya ya figo. Kwa mfano zabibu hupunguza hatari za kupata maradhi ya figo yanayoitwa kidney stone yaani vijiwe vinavyokaa kwenye figo.

2.Nanasi (pineplea)
Hili ni katika matunda yanayopatika na sana kwenye uoto wa kitropik. Tunda hili ni katika matunda yenye virutubisho vingi kuliko matunda mengi sana yanayopatikana katika maeneo yenye uoto huu. Kwa mfano kikombe kimoja cha nanasi (mililita 237) kinatosheleza uhitaji wa mwili wa vitamini C kwa siku nzima na asilimia 76 ya madini ya manganese.

Nanasi pia lina bromelain huu ni mchanganyiko wa enzymes ambayo inajulikana kwa kudhibiti uvimbe na kuwa na uwezo wa kumeng’enya protini mwilini. Tafiti nyingi za kisayansi zimeonesha kuwa bromelain husaidia kuzuia mwili kupata maradhi ya saratani na uvimbe amao ni katika viashiria vya saratani.

3.Palachichi (avocado)
Hili ni katika matunda yenye fat (mafuta). Itambulike kuwa si kila mafuta ni hatari ndani ya miili yetu. Tunahitaji vyakula vya fat yaani mafuta kwa ajili ya kutupatia joto kwenye miili yetu. Pia fati husaidia kuipa miili yetu nguvu. Katika tunda hili palachichi mafuta yake ni aina ya oleic acid yaani yapo katika aina flani ya asidi ambayo husaidia katika kupunguza uvimbe mwilini na kusaidia kuboresha afya ya moyo.

Palachici pia hutambulika kitaalamu kuwa lina lina madini ya potassium na magnesium kwa wingi sana. Pia ni katika vyakula vyenye kambakamba yaani fiber. Vyakula hivi vyenye fiber husaidia katika kuweka usalama wa tumbo yaani kuhakikisha chakula kinatembea ipasavyo ndani ya tumbo kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine mpaka kufika kwenye njia ya haja kubwa.

Pia tunda hili husaidia kupungusa hatari za kupata maradhi ya strokr yaani kupalalaizi kutokana na kiwango kikubwa cha madini ya magnessium ambayo husaidia katika kupunguza shinikizo kubwa la damu. Hivyo palachichi husaidia katika kudhibiti afya ya moyo. Palachichi moja linaweza kutoa 28% ya mahitaji ya mwili ya madini haya.

4.Buluu beri (blueberry)
Ni katika matunda yanayotambulika kuwa na virutubisho vingi mwilini.. Tunda hili hutambulika kuwa na vitamini c kwa wingi, vitamini K na madini ya manganese. Pia tunda hili lina kambakamba yaani fiber. Itambulike kuwa vitamini C ni katika vitamini vinavyofanya kazi kubwa sana kulinda afya na kuupa mwili uwezo wa kupambana na maradhi kuliko aina nyinginezo za vitamini.

Pia tunda hili lina antoxidant kwa wingi. Hii husaidia katika kupambana na maradhi ndani ya mwili. Antoxidant huzuia mwili usipatwe na maradhi hatari shambulizi kama shambulizi la moyo, kisukari na mengineyo.

Tunda hili pia husaidia katika kufanya madhubuti mfumo wa kinga wa mwili yaani immune system. Wataalamu wamegundua kuwa tunda hili husaidia katika kuuwa seli yaani natural killer cell hali hii husaidia mwili katika kupambana na athari za stress yaani msongo wa mawazo pamoja na mashambulizi ya virusi yaani viral infections.

Pia tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu. Husaidia tatizo la kupoteza kumbukumbu hasa kwa wazee. Tunda hili ni katika orodha ya matunda ambayo yanajulikana kwa uwezo wake wa kusaidia katika kutunza kumbukumbu na kuondoa tatizo la kusahausahau.